POLISI Mwanza Wapiga STOP Mkutano wa Hadhara wa CHAGULANI: Hofu ya makundi yatanda CDM

Ccm igeni cdm.waloshindikana fukuza.chagulani ana uroho wa madaraka.amia kwa nape

Mhh Fikara za haraka kidogo hizi...Hebu tuzame zaidi. ANC walimwona Julius Malema kama Individual character kumbe haikuwa kweli Malema is a deadly leaving society.
 
Ni kweli jana mkutano ungefanyika kungechafuka mwanza.Zitto alikimbia kamati kuuu hakuwepo kwa nini?

Tunaziwakeje pamoja kambi hizi mbili zenye nguvu kubwa na kila moja na utashi na vipaumbele vyake vinavyokinzana?
 
A HUGE NUMBER ON BOARD SUGGEST SOLUTION PLEASE, BUT DONT DICTATE COZ HII SI KAMATI KUU INAYOJADILI HAPA ILA WATASOMA NINI HASA WANACDM NA WANASIASA NJE YA UWANJA WANAWAZA.

There are currently 116 users browsing this thread. (24 members and 92 guests)

Nashangazwa na jambo moja! Kwanini CDM wanashindwa kuvunja migawanyiko kama hii mapema? Tunadhani 2015 ni mbali? Viongozi wanaposhindwa kuchukua hatua mapema kwa wanachama wasio waaminifu watafanya nini tukiwapa serikali? Huu mwendo huu mbona unataka kufanana na CCM iliyolea madogo kwa muda mrefu sasa yameisambaratisha.

Kwanza maamuzi ya kamati kuu yamechukua muda mno kwa mambo yaliyo wazi kikanuni! Si ndio haya haya ya tume za CCM tunazopigia kelele?

Kufukuza wanachama haitoshi,lazima ufanyike usafi kweli kweli kuelekea 2015 otherwise tutawakatisha tamaa wananchi!

Nini muarobaini wa hii saratani ndani ya CDM?
 
wakati mwingine tuwe watu wakutafakari sio maamuzi ya cc yanafaa sioni sababu ya kufukuzwa uwanachama mtu anapokosea. Hii ni sababu ya vyeo vya juu kugombaniwa, maslahi ya mtu binafsi Hapo mbele sana kuliko taifa ubabe nao uwahadaa walio cc, wanatoa maamuzi ya ubabe sababu ya nafasi walizopo, kama kweli mnatimua vijipandikizi vya ccm anza na shibuda mbowe, yeye amewapinga hadharani tena maamuzi ya chama mf bungeni Hapo ndo ntaamini hamna uchu wa madaraka ila mnajenga nchi, binafsi ni follower wa highness na wenje na nipo ilemela ila haya maamuzi sijaridhika nayo. tafakarini
 
Inasadikiwa Mikutano Mingi ya ndani ya CDM Mza ilikuwa inafanyika MAGNUM Hotel ambayo inamilikiwa na aliyekuwa kamanda wake kata ya Kitangiri Henry Matata. Hii ina maanisha ramani zote za vita zilipangwa hapa, kwa hiyo hii hali na uvujifu wa mipango hii ya ndani inadhibitiwaje kutotoa mwanya kwa mahasimu wa kisiasa kukihujumu Chama?

Unahitajika mkakati wa ziada ya maamuzi ya Kamati kuu ikiwa ni pamoja na another version of M4C Mza tena katika kuclear out hii uncertain political atmosphere.
 
Siasa smtms lyk mathematical Calculations. Haijalishi formula gani umetumia kuderive kwenye kusaka solution kinachomata ni jibu and viceversa kwani wakati mwingine jibu linaweza lisiwe na maana kama formula iliyotumika ni batili.
 
Chagulani anafanya mkutano kwa chama kipi? Si amefutwa uanachama na hivyo kapoteza nyadhifa zake zote alizokuwanazo ndani ya CDM ikiwa n pamoja na udiwani.Ni mkutano kama mwanaharakati au mchungaji?
 
Chagulani anafanya mkutano kwa chama kipi? Si amefutwa uanachama na hivyo kapoteza nyadhifa zake zote alizokuwanazo ndani ya CDM ikiwa n pamoja na udiwani.Ni mkutano kama mwanaharakati au mchungaji?

Kutokuwa na Chama hakumyimi Nafasi ya kufanya Mkutano wa Hadhara, Anataka kuhutubu nini hii ndio hadidu muhimu.
 
POLISI Mwanza Wapiga STOP Mkutano wa Hadhara wa CHAGULANI:
  • Hofu ya makundi yatanda CDM
  • Kambi za wanasiasa wenye uchu na mapandikizi Kukitafuna Chama

Kuna kila dalili za wazi kuwa zile kambi mbili ambazo zimekuwa zikitajwa kuitafuna CDM katika Mkoa wa Mwanza zinaendelea kuimarika hasa baada ya maamuzi ya kuondosha mapandikizi kulikofanywa na kamti kuu.

GR anaendelea kusaka kiini cha kambi hizi na athari zake katika majaaliw ya CDM mwanza (tutakutana katika thread nyingine juu ya hili)

Hadhari kubwa na mashaka yanaelekezwa kwa Viongozi wa CDM ambao mara kadhaa wameshutumiwa hapa jamvini kwa kuendekeza makundi na kuonyesha dhahiri ulafi wa madaraka ambao umeendelea kuwa kansa inayoutafuna umahiri na kasi ya CDM katika baadhi ya maeneo Nchini ambayo mtandao wao unaonekana kushamiri huku Mwanza ikiwa moja ya vitovu vya uasi huu.

Mdi haya ambayo yamekiwa yakipuuzwa au hata kupewa majibu mepesi wakti mwingine sasa ni wazi kuwa hatua za madhubuti zinahitajika kama ninavyojidhihiri kwenye my take hapo chini.

Hapa tunaguswa na uamuzi huu wa siku chache Baada ya kuenguliwa uanachama wa CDM kwa madai ya kukiuka kanuni na miongozo ya Chama, Chagulani Ibrahim Adam pamoja na Henry Matata walipanga kufanya mkutano wa hadhara jijini Mwanza kuelezea mustakbal wao baada ya uamuzi wa kamati kuu ya CDM.

Chanzo cha GR kutoka Jeshi la Polisi Mwanza(Jina linahifadhiwa) kililazimika kusitisha mkutano huo kutokana na kuwepo na tetesi za kugawanyika kwa makundi ya wafuasi wa CDM huku kundi jingine linalomuunga mkono Mmoja wa Viongozi wa Chama hicho (jina linahifadhiwa hadi kukamilika kwa uchunguzi wa madai haya) anayedaiwa kuwa na bifu la muda mrefu na kambi inayomuunga mkono Chagulani.

Katika hatua nyingine inasemekana kuwa wanasiasa hao waliopokwa uanachama watakutana leo na mwanasheria wao kujipanga kufungua madai ambayo GR na wanyetishaje wake huko mza hawajayabaini ila harakati zikifanikiwa tutakutana nayo hapa jamvini.

My Take

  1. CDM msiridhike na maamuzi ya kamati kuu fuatilieni matokeo baada ya maamuzi haya kuepusha dalili za makundi katika chama kama ambayo yanawatafuna nyinyiemi kwa sasa.
  2. Chagulani sijui kama uamuzi huu ulikuwa wa busara kwa sasa?

ADIOS

GR asante kwa baadhi ya mambo ambayo yana uhalisia (si lazima yawe kweli though, reality vs truth), lakini at least moja kwa sasa, umeweza kujiuliza hao watu waliomba kufanya mkutano wa hadhara au maandamano kama nani?

Waliomba/aliomba kupitia Ofisi ya Diwani...ama hawakujua au walisahau kuwa udiwani wao ulikoma pale pale walipovuliwa uanachama. Mpaka hapo si taasisi tena. Wanahangaika kutafuta forum ya kufanya propaganda.

It is so sad kwa kijana mdogo kama Chagulani, ambaye angeweza kabisa kuwa na very promising future kwenye siasa, kuanza kujitafutia misukosuko na migogoro, tena kwa kukiuka katiba, kanuni, miongozi na taratibu za chama ambacho kinataka kutoa utumishi kwa wananchi wenye matumaini makubwa.

Tunajua nguvu kubwa ya watu wa Mwanza inaunga mkono maamuzi ya chama chao kupitia Kamati Kuu kwa kuwavua udiwani akina Chagulani na Matata na kuvunja uongozi wa mkoa. Sasa watulie. Wasikilize chama chao, kuanzia ngazi ya chini kabisa kwenye misingi na matawi, kinasema nini. Wanajua kuwa hiki ni chama chao, kinafanya uamuzi kwa maslahi yao, kulinda matumaini ya Watanzania wengi.

Samaki hana ujanja akiwa nje ya maji...ofcourse hata kiboko mwenyewe!

wakati mwingine tuwe watu wakutafakari sio maamuzi ya cc yanafaa sioni sababu ya kufukuzwa uwanachama mtu anapokosea. Hii ni sababu ya vyeo vya juu kugombaniwa, maslahi ya mtu binafsi Hapo mbele sana kuliko taifa ubabe nao uwahadaa walio cc, wanatoa maamuzi ya ubabe sababu ya nafasi walizopo, kama kweli mnatimua vijipandikizi vya ccm anza na shibuda mbowe, yeye amewapinga hadharani tena maamuzi ya chama mf bungeni Hapo ndo ntaamini hamna uchu wa madaraka ila mnajenga nchi, binafsi ni follower wa highness na wenje na nipo ilemela ila haya maamuzi sijaridhika nayo. tafakarini

Fered Mbataa, namna ulivyoweka maelezo yako inaonesha hujui what actually was at the centre. Nafikiri itakuwa vyema ukichukua muda wa kupata taarifa juu ya suala zima ili ujue kwa kina, naweza kuona kabisa mchango wako hautakuwa sawa na huu ulioutoa hapa. Fanyia kazi ushauri huo kadri iwezekanavyo kamanda.Lakini pia nimeshtuka kusoma kuwa wewe ni mfuasi wa watu binafsi, sidhani kama ni sahihi sana au...anyway subjected to debate.
 
wakati mwingine tuwe watu wakutafakari sio maamuzi ya cc yanafaa sioni sababu ya kufukuzwa uwanachama mtu anapokosea. Hii ni sababu ya vyeo vya juu kugombaniwa, maslahi ya mtu binafsi Hapo mbele sana kuliko taifa ubabe nao uwahadaa walio cc, wanatoa maamuzi ya ubabe sababu ya nafasi walizopo, kama kweli mnatimua vijipandikizi vya ccm anza na shibuda mbowe, yeye amewapinga hadharani tena maamuzi ya chama mf bungeni Hapo ndo ntaamini hamna uchu wa madaraka ila mnajenga nchi, binafsi ni follower wa highness na wenje na nipo ilemela ila haya maamuzi sijaridhika nayo. tafakarini
CHADEMA siyo chama kina cho kurupuka mkuu....hao watu unao watetea walisha onywa mara kibao lakini hawataki kijirekebisha ulitaka shama kiendelee kuwa bembeleza...kuhusu Shibuda mara nyingi shibuda anatoa kauli zake akiwa na kofia ya ubunge siyo huyo anae zunguka vijiweni na kwenye vyombo vya habari kuinanga chadema....
 
GR asante kwa baadhi ya mambo ambayo yana uhalisia (si lazima yawe kweli though, reality vs truth), lakini at least moja kwa sasa, umeweza kujiuliza hao watu waliomba kufanya mkutano wa hadhara au maandamano kama nani?

Waliomba/aliomba kupitia Ofisi ya Diwani...ama hawakujua au walisahau kuwa udiwani wao ulikoma pale pale walipovuliwa uanachama. Mpaka hapo si taasisi tena. Wanahangaika kutafuta forum ya kufanya propaganda.

It is so sad kwa kijana mdogo kama Chagulani, ambaye angeweza kabisa kuwa na very promising future kwenye siasa, kuanza kujitafutia misukosuko na migogoro, tena kwa kukiuka katiba, kanuni, miongozi na taratibu za chama ambacho kinataka kutoa utumishi kwa wananchi wenye matumaini makubwa.

Tunajua nguvu kubwa ya watu wa Mwanza inaunga mkono maamuzi ya chama chao kupitia Kamati Kuu kwa kuwavua udiwani akina Chagulani na Matata na kuvunja uongozi wa mkoa. Sasa watulie. Wasikilize chama chao, kuanzia ngazi ya chini kabisa kwenye misingi na matawi, kinasema nini. Wanajua kuwa hiki ni chama chao, kinafanya uamuzi kwa maslahi yao, kulinda matumaini ya Watanzania wengi.

Samaki hana ujanja akiwa nje ya maji...ofcourse hata kiboko mwenyewe!

Nakubaliana na wewe mkuu
 
Siasa smtms lyk mathematical Calculations. Haijalishi formula gani umetumia kuderive kwenye kusaka solution kinachomata ni jibu and viceversa kwani wakati mwingine jibu linaweza lisiwe na maana kama formula iliyotumika ni batili.
Hebu funguka zaidi mkuu...
 
Kimsingi Tunakubaliana katika jambo moja kama mwanabodi Yahya M alivyochanga mawazo hapo juu ya falsafa yake ya mahesabu, japo sina hakika sana kama Yahya M ni mwanamahesabu.

Mkuu Makene T Kamati kuu ni vema ikatazama aftermath ya maamuzi yake kwa kina na kuhakikisha hakuna mwanya wa siasa za makundi rika kutawala mfumo wa kanuni na taratibu za maongozi ndani ya CDM. Picha inayojengeka; moja ni kuwepo na kundi lisilohitaji kukosolewa ambalo mie binafsi siamini sana, pili; vijana hasa wale wanaohisiwa kuwa na nasaba ya mtandao uliojigubika upandikizi ndani ya CDM kufutwa kabla ya 2015, tatu ni hila za Nyinyiemi kusaka samaki watakaoenguliwa kuipa nguvu ADC

kwenye bold bado sijasomi vizuri...
 
Inasadikiwa Mikutano Mingi ya ndani ya CDM Mza ilikuwa inafanyika MAGNUM Hotel ambayo inamilikiwa na aliyekuwa kamanda wake kata ya Kitangiri Henry Matata. Hii ina maanisha ramani zote za vita zilipangwa hapa, kwa hiyo hii hali na uvujifu wa mipango hii ya ndani inadhibitiwaje kutotoa mwanya kwa mahasimu wa kisiasa kukihujumu Chama?

Unahitajika mkakati wa ziada ya maamuzi ya Kamati kuu ikiwa ni pamoja na another version of M4C Mza tena katika kuclear out hii uncertain political atmosphere.

Mkuu GHOST RYDER mimi binafsi siko Mwanza lakini kwakuwa nina ndugu zangu wa damu hapo mwanza, wanaishi Mkuyuni, Kirumba, Kitangiri na wengine Kilimahewa siasa za Mwanza nazifuatilia na kuzipata kwa ukaribu sana.

Chagulani na Mwenzake Matata kilichowakuta walijitakia wenyewe, Chagulani kwa kiburi na jeuri ya kujifanya much know na kuleta siasa za uanaharakati wa chuo kikuu katika siasa halisia za mtaani, Henry Matata alikuwa anatafuta upenyo wa kuweka sawa mambo yake, ameshajipatia viwanja kadhaa hapo jijini Mwanza na wala hafichi kulisema hilo.

Kwa ujumla wote wawili waliingia katika anga za ccm, na kama unavyojua ccm kwa kumwaga noti hawajambo kwahiyo wakikugundua kwamba wewe ni mpenda chapaa hawachelewi kukutupia ndoano. Chagulani na Matata walitupiwa ndoano ya fedha na ccm kwa kupewa kazi maalum ndani ya Chadema nao wakakubali.

Intelijensia ya chama ilifanikiwa kupata taarifa zote hizo na watuhumiwa wakaitwa mara kadhaa na kuonywa, na viongozi wa kitaifa walifika mara kadhaa mkoani Mwanza kujaribu kutuliza hali ya mambo na wakati mwingine hao watu waliitwa dsm kwenye vikao vya chama na kupewa maelekezo ya namna ya ku-behave kwa mujibu wa katiba yetu pamoja na maonyo kadhaa ili warudi katika mstari lakini hawakutaka kusikia la mkuu.

Uamuzi wa kamati kuu wa kuwafutia uanachama haukuja ghafla ama kwa bahati mbaya, walipatiwa nafasi ya kutosha ya kujirudi lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo wanachama wenyewe wa mkoa wa Mwanza walielezea kutoridhishwa kwao na mienendo ya madiwani hao pamoja na uongozi wa mkoa, hivyo ngazi za juu za uongozi wa chama walitakiwa kuchukua hatua ya kukisafisha chama na kukinusuru na mgogoro au mgawanyiko uliokuwa unakinyemelea, na kwa kutambua hilo kamati kuu baada ya kujiridhisha kwa ushahidi uliopatikana na baada ya kupata maelezo ya kina toka kwa matata, chagulani na uongozi wa mkoa walichukua hatua muafaka ya kuwavua uanachama chagulani na matata huku wakiuweka kando uongozi wa mkoa.

Baada ya uamuzi huo, wanachama wengi wameipongeza kamati kuu kwa kukinusuru chama mkoani humo na sasa wanaona mwanga mbele yao kwakuwa sasa mshikamano uliokuwa umeanza kutetereka utarejea. Sasa hao madiwani waliotemwa kama wana makundi maadamu wako nje ya chama hawawezi kuwa na madhara makubwa kama ambavyo wangeachwa waendelee kutumia mwavuli wa chama kukihujumu. Kwahiyo sasa wanaChadema mkoa wa mwanza watakuwa tayari kupambana na adui zao ambao wako nje na ambao ni rahisi kuwatambua na kukabiliana nao.

Nimalizie mchango wangu kwa kusema kwamba bado uungwaji mkono Jijini Mwanza ni mkubwa sana tofauti na baadhi ya watu(hasa mahasimu wetu) wanavyodhani ama kuombea iwe. Chagulani atafukurukuta kwa muda mfupi tu lakini atatulia na atasahaulika. Kwani wale madiwani watano wa Arusha wako wapi? nani anawajadili tena sasahivi? nani anawaulizia tena sasahivi? katika hili namhurumia zaidi chagulani kwakuwa bado ni kijana mdogo sana, na amekubali kujulikana bei yake.
 
Last edited by a moderator:
Ccm igeni cdm.waloshindikana fukuza.chagulani ana uroho wa madaraka.amia kwa nape

nyie mnatofauti gani na Ccm ambao kila tatizo wanasingizia Chadema, sasa kila tatizo mnamsingizia Zitto, huko ni kujipofusha mkidhani mnatatua kumbe mnayaahirisha matatizo!
 
Back
Top Bottom