Polisi: Maandamano ya Novemba 26 marufuku!

Hii ni taarifa ya habari kutoka redio yenye spika.
kwanza habari kwa ufupi.
BINGWA mwenye shahada ya juu iliyoukuka ya utaahira ulio sababisha macho yake yawe macho kumchuzi amepiga marufuku maandamano ya tarehe 26-11-11 kwa kisingizio cha ali shababu.
mimi nimegundua wale jamaa wenye mbuti na vilungu na mabomu ya machozi ndio ali shababu wenyewe.
HATA KWA KITISHO GANI, LAZIMA TUTAANDAMANA KUILILIA KATIBA.
ZE END
 
Amiri Jeshi mkuu Dr Dr Dr Dr Dr Jakaya Kikwete atutangazie rasmi kuwa nchi iko katika tishio la ughaidi hivyo watu wachukue tahadhari wasikusanyike kama kwenye harusi, mpira, maandamano na shuguli yoyote inayohusisha watu zaidi ya watano. Bila hivyo tutaandamana at our own risk polisi watuache tu wasitupige mabomu, mabomu wawapige Al Shabaab

Nimeipenda. Wawaache watu waandamane tena wasiende kuwalinda wao wabaki wapigane na Alshabab kama ni wabaya wao
 
Mimi binafsi sitashangaa waliombele yetu kudai Katiba hii wakiingia mitini kisa eti makengeza kasema Al-shabab wapo kwani kama makengeza anasema wapo si anajua walipo? Watu wamekuwa wakisema serikal inamkono mrefu hata uwe wapi watakukamata iweje anatueleza wananchi habari hizo za kupinga maandamano ili hali amekaa tu bila kutueleza wamekamata wangapi. Kwa wingi tulionao tunaomba tujitokeze kwenye maandamano tuone makengeza atatufanya nini jamani.Kumbukeni woga wetu ndiyo umaskini wetu.
 
Kelele za vyura hazinyimi ng'ombe kunywa maji mwaacheni Kova apige kelele maana lazima tuandamane
 
andamaneni tu ila kumbukeni field force unity wapo mzigoni kama kawaida yao,mi sisutu kutoka jamani nasikia jamaa wamejiandaa kinoma ni ayo tu wakuu jioni njema
 
kova amapiga marufuku maandamano ya wanaharakati na vyama vyote ambavyo vina mpango wa kuandamana
tarehe 26.11.2011 kwa sababu ya kuwepo alshabab nchini
images
images


hapa tumpongeze sana kova kwa kazi nzuri

mytake

1.clouds fm wanaanda tamasha la usiku 26.11.2011( wapigwa marufuku na wao)
2. Sugu anaandaa tamasha la usiku 26.11.2011 ( nayeye apigwa marufuku)
3.

hawa alishaabab tunawatumia kama kisingizio kuzuia mikutano na mikusanyiko siku wakitia timu kiukwelii hatutawaita kwa jina jepesi hivo
 
kitendo cha kuzuia maandama ni cha ukiukaji wa haki ya kikatiba.
Al shabaab kama watakuja kwenye maandamano basi njoo uwakamate. Maana ni msomali gani anayelilia katiba ya tanzania?
Siku hiyo kuna matamasha mawili makubwa, moja wanakuja wamarekani, namshauri kova alifute kwa usalama wa wageni na wa tz.

Pia ikumbukwe kuwa hii sio mara ya kwanza kwa kova kuzuia maandamano ya amani kwa kisingizio cha al shabab.

Nchi ikichafuka, kova atakuwa mgeni wa nani?
na asiyekuwa na upanga na auze kanzu moja anunue upanga
 
hayo maanadamo ni ya tanzania nzima
je hao alshabaab wametapakaa mikoa yote?

maana hata huku kwete tunaandamana na tayari tulisha jua wapi tunaanzia
 
IGP Ni mteule wa rais hana maamuzi yoyote zaidi ya kufanya kazi kwa maelekezo toka kwa waziri wa mambo ya ndani na rais,
Katika hili tusiwalaumu polisi nao ni ma victim wa hali mbaya ya nchi kama sisi sema hawana pa kusemea.
 
Kweli hiyo ni Al sababu! Ngoja tuone kama hakutakuwa na maandamano ya kuingia uwanja wa taifa tar 9 dec.
Tena umenikumbusha juzi makamu wa raisi alijaza watoto pale Sheikh Amri Abed lakini hatukuwaona Al-Shabab....kama vipi tuingie vitani kupambana na hili kundi maana watanzania kumbe hatuko huru kama kuna mambo hatuwezi kuya fanya kwasababu ya Al shabab wakati katiba yetu inaturuhusu kufanya hivyo sasa kwanini tusikiangamize ili tuwe huru.....
 
Sijawai sikia serikali hii ya Tanzania hisiyopenda kufanya kazi.
Hipo tu kwa hisia na kuwaragai watu na tishio la alshabab.
Himeonyesha jinsi gani hatuna ulinzi hapa kwetu,kama ndo hivyo tuajiri masai watulinde.
Hiii inakela mpo tu kazi kuvuaa magwanga.
Woga huu alshabab awajatupiga mkwara JE wakitupiga mkwara natumaini wote na Rais wetu tutajifungia kabatini.
'Tz tunalindwa na Mungu"
Week end nilikuana jamaa mmoja Dreva wa malori ya kwenda Burundi na Congo.Tukiwa tumekaa tunapata moja baridi moja moto,mara akatoka kupokea simu,aliporudi akanisimulia mkasa wa jamaa waliokuwaa wamempigia simu.Hao jamaa ni warundi walikua wamempigia simu kumuomba walau shillingi elfu themanini maana ndio walikua wameachiwa baada ya mahakama kuwaona hawana hatia.
Kisa ni kwamba,Hao jamaa ni wanajeshi wa Burundi walikua wanapigana na waasi.sasa walipowazidi wasasi nguvu waasi wakawa wanakimbilia TZ, waliwatimua mpaka wale wanajeshi wakajikuta wamefika pale mpakani kigoma,huku wale waasi wakiwa washaingia TZ.Kuona vile wale wanajeshi wakaenda moja kwa moja kwa askari waliokuwa pale mpakani kigoma na kuwakuta askari wetu wamelala fofofo,wakawaamsha na kujitambulisha pamoja na kukabidhi silaha zao.Sasa walinzi wetu walipowasiliana na Burundi serikali ya kule ikasema hao watakua ni waasi tu.Hivyo wakawekwa ndani na kupelekwa mahakamani.Mahakama iliwaachia kwa sababu hao jamaa walipofika kwetu waliripoti kwa mamlaka husika na kukabidhi silaha zao,kwa hiyo hawakuwa na nia mbaya kwetu.Lakini jamaa walicheka sana wakasema tz Tunalindwa na Mungu.
 
Hivi hao Alshabib wamesambaa kila kona ya nchi yetu ama. Kama siyo kweli basi waruhusu kwenye ile mikoa ambayo haina tishio la hao jamaa tuone!!!
 
Maandamano yaliyotaka yafanywe na asasi zisizo za kiserikali kudai marekebisho ya mswada wa katiba yamekwaa kisiki kikuu cha alshababu, Mpaka nawasilisha nikuwa kutokana na Tishio la alshabab hakutakuwepo kwani ni gharama na kazi kubwa kuhakikisha usalama katika maandamano yao.

Atakaye andamana kukutana na nguvu ya dola.


Naomba kuwasilisha


My Take:

Mbona mkuu wa kaya alikaa na wazee

umeitoa wapi aiseee...
 
Wakati sasa umefika kuzipima nguvu hizi za "dola", isije ikawa mikwara ya akina Sadaam mbele ya majeshi ya Marekani, au hata zile za Mubarak mbele ya watu wake.Na siku tutakapowadhihirishia kuwa sisi tuna nguvu nyingi kuliko huyo "dola" ndipo watajuta kwa nini walitutishia nguvu ambazo huyo "dola" hana bila sisi kumuunga mkono
 
Back
Top Bottom