Sina hakika kama kuna mtu humu Jf anaunga mkono Rais kutishwa kwa namna yoyote ile; lakini unaonaje kama zitafanyika jitihada za kuondoa mapungufu na kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano? Hivi kutakuwa na vitisho vyovyote kwa Rais? Kutakuwa na maandamano? Hebu tusaidiane njia ya kufika huko.
Njia ya kufika huko ni kuwepo na watu kama Mwanakijiji na wengineo sote kwa pamoja na vyama vya upinzani ambao kazi yetu ni kukosoa. Vile vile kama nilivyosema mwanzo kuandamana ni haki yetu ya msingi hata kama serikali ikitumia mabavu dunia ya sasa ni ya uwazi na kama serikali ikiwa inatumia nguvu basi wafadhili wapo watawazuia na ICC vile vile.
Kama serikali haitaki kutusikiliza watanzania dunia itatusikiliza na mfano mzuri ni Syria Bashir Al-Assad katumia mabavu mwisho amesalimu amri ya kuleta mabadiliko. Ndio demokrasia inavyokwenda kwa akili na maarifa ndugu zetu wazanzibari ni wazoefu katika kudai haki ya kidemokrasia labda tukajifunze kutoka kwao.