Polisi Kupiga Raia ni Halali?

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Polisi wamshushia kipigo mwandishi
Na Mwandishi wetu


Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Ali Lityawi, juzi alipata kipigo kikali kutoka kwa askari wa jeshi la polisi wilayani hapa na kunyang’anywa kamera yake ya kazi kwa madai ya kupiga picha mahabusu aliyetoroka rumande.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:45 jioni katika mtaa wa Lumelezi karibu na Hospitali ya Magai ambapo alikutana na askari hao wakiwa katika jitihada za kumkimbiza mahabusu huyo aliyewatoroka kituoni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lityawi alisema kuwa baada ya mahabusu huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja kukamatwa na polisi kwa kushirikiana na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo, alianza kupiga picha za tukio hilo.

Alisema katika harakati za kupiga picha, alijitokeza askari mmoja na kuanza kumshambulia kwa kumpiga kisha kumnyang’anya kamera aliyokuwa nayo na katika jitihada za kuigombania, ilidondoka ndani ya mtaro wa maji.

Lityawi alisema wakiwa katika purukshani hizo, alijitokeza askari mwingine na kumsaidia mwenzake kuendelea kumshambulia.

Alisema katika jitihada za kugombania kamera, hiyo askari hao walifanikiwa kuichukua huku wakimkamata na kwenda naye kituoni ambapo walifika na kumweleza Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD), George Simba,, aliyeamuru kuwekwa mahabusu kwa muda kwa kosa la kuwapiga askari picha bila kibali maalum.

“Aliniamuru kufuta picha hizo haraka kwenye kamera na baada ya kukataa na kutaka anionyeshe ni kifungu gani cha sheria kinachompa mamlaka ya kunizuia kufanya kazi zangu, aliamuru itolewe kadi ya kumbukumbu iliyohifadhi picha hizo na kunitaka niifuate kesho yake kituoni hapo,” alisema.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani, amelaani kitendo hicho kilichofanywa na askari wa jeshi lake na kumtaka OCD kuangalia jinsi ya kumtengenezea kamera yake mwandishi huyo na kumwomba msamaha.

“Ni sera ya jeshi kusaidiana na waandishi wa habari na vyombo vyao kuwaelimisha wananchi utendaji kazi wa jeshi na kuwapa elimu inayohusiana na usalama wa raia na mali zao. Kama waliona kuwa picha anazopiga si nzuri kwao, wangemwomba asizitumie badala ya kumshambulia, kumharibia kamera yake, lakini pia kumweka mahabusu kwa muda,” alisema.

CHANZO: NIPASHE

Matukio mengi yanaripotiwa ya polisi kupiga watu kinyama. Wanajamvi mnasemaje kuhusu hili?
 
Hakuna sheria inayompa nguvu au inayotoa mamlaka ya kutoa kipigo kwa wananchi.hayo ni matumizi ya nguvu yanayoenda kinyume na haki za binadamu.polisi kupiga watu ni kukosa busara na ustaarabu.kama wanachi wameomba kuandamana sababu wanaona haki yao inachezewa waachwe waandamane sababu ni yaki yao ya kikatiba ilimradi hawvunji sheria.la msingi linaloonekana hapo ni kuwa jeshi letu la polisi lapaswa kufanyiwa reforms ili liendane na wakati uliopo sasa hivi vinginevyo litaleta mkanganyiko ktk jamii.
 
Ninakubaliana nawe Katitu. Kinachoonekana ni kwamba Jeshi hilo sio usalama wa raia tena bali lipo kwa ajili ya masilahi ya watu binafsi au mabosi. Kama pale Arusha walivyofanya, Mkuu wao anasema hana polisi wa kutosha kwa ajili ya kulinda mkutano wakati polisi wamejazana kwenye magari kila kona ya mji.

Jeshi kama halitumiki kwa busara ya Usalama wa Raia, jeshi hili litakuwa limekosa makusudi ya kuwepo kwake hapa nchini. Kikosi cha Fanya Fujo Uone, inaonekana wao ndio waanzisha fujo katika matukio mengi. Na IGP inaonekana anafurahia matukio yote hayo ya jeshi lake kuanzisha fujo.
 
Back
Top Bottom