Polisi kaniharibia siku yangu

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Nikiwa naenda kazini kwa kutumia daladala, mara akapanda askari polisi, gari ilikuwa na nafasi kadhaa za kukaa, na miongoni mwa nafasi hizo ni nafasi iliyokuwepo jirani na nilipokaa.
Baada ya kituo kimoja tokea alipopandia, akatoa kipisi cha sigara kutoka kwenye mfuko wake wa shati, akakiwasha na kuanza kukivuta.
Abiria na wqahudumu wa daladala tulimsihi azime kwa kuwa anahatarisha afya zetu, akagoma na akawa akiporomosha matusi kwa sauti ya ulevi.
Nimekereka kwelikweli, na nimeamua kuteremka kwenye hilo gari kabla sijafika kule niendako.
Kweli Tanzania hamna polisi, ila yunifomu za polisi
 
Pole sana, mlipaswa kumnyang'anya hiyo sigareti na kuizima.
 
mmmh, pole ndo tulivyo maporishi, tena ukute kalewa gongo ndo utajibeba.
 
mngemkoromea au hata kumpiga ngumi kama akizingua..

Nifikiri uamuzi nilio uchukua wa kuteremka garini ulikuwa wa busara zaidi, kuliko kumpiga.
Waswahili wanasema bora nusu shari kuliko shari kamili.
Biblia inasema, tafuteni kuwa na amani na watu wote.
 
ungevizia namba yake kwenye guanda lake
ili tumuanike hapa jamvini.

asikali wa siku hizi hawavai namba.kwa sababu wanabebana. ndo maana siku hizi polisi wengi unakuta wana undugu, halafu usifikili wanaichukulia hiyo kazi kivilee.ndo maana siku hizi kukuta polisi kavaa mlegezo au kukaa baa na kunywa pombe na magwanda ni kitu cha kawaida sana. mia
 
wananifurahisha tu pale nilipoenda kureport tukio la wizi wakadai mpaka niwapelekee uthibitisho wa kuibiwa ndo wataandika report yangu. labda mnisaidie ndugu zangu utathibitisha vipi polisi kuwa umeibiwa?
 
hehehehehe hiyo kali
 
Nifikiri uamuzi nilio uchukua wa kuteremka garini ulikuwa wa busara zaidi, kuliko kumpiga.
Waswahili wanasema bora nusu shari kuliko shari kamili.
Biblia inasema, tafuteni kuwa na amani na watu wote.
we jamaa vipi wewe bana!!
mngemchapa bana!! hana adabu huyo!
 
hapo kwenye red pameniacha hoi mkuu! Ina maana hawa wenzetu hawana hata pesa ya kununua sigara nzima!?
Nikiwa naenda kazini kwa kutumia daladala, mara akapanda askari polisi, gari ilikuwa na nafasi kadhaa za kukaa, na miongoni mwa nafasi hizo ni nafasi iliyokuwepo jirani na nilipokaa.
Baada ya kituo kimoja tokea alipopandia, akatoa kipisi cha sigara kutoka kwenye mfuko wake wa shati, akakiwasha na kuanza kukivuta.
Abiria na wqahudumu wa daladala tulimsihi azime kwa kuwa anahatarisha afya zetu, akagoma na akawa akiporomosha matusi kwa sauti ya ulevi.
Nimekereka kwelikweli, na nimeamua kuteremka kwenye hilo gari kabla sijafika kule niendako.
Kweli Tanzania hamna polisi, ila yunifomu za polisi
 
asikali wa siku hizi hawavai namba.kwa sababu wanabebana. ndo maana siku hizi polisi wengi unakuta wana undugu, halafu usifikili wanaichukulia hiyo kazi kivilee.ndo maana siku hizi kukuta polisi kavaa mlegezo au kukaa baa na kunywa pombe na magwanda ni kitu cha kawaida sana. mia

na hiyo jeuri aliyokuwa nayo inaonyesha ndo hao hao wa kubebwe na mbereko za jamaa zao.
 
wananifurahisha tu pale nilipoenda kureport tukio la wizi wakadai mpaka niwapelekee uthibitisho wa kuibiwa ndo wataandika report yangu. labda mnisaidie ndugu zangu utathibitisha vipi polisi kuwa umeibiwa?

walikuwa wanakuomba rushwa, hawana lolote
 
Nikiwa naenda kazini kwa kutumia daladala, mara akapanda askari polisi, gari ilikuwa na nafasi kadhaa za kukaa, na miongoni mwa nafasi hizo ni nafasi iliyokuwepo jirani na nilipokaa.
Baada ya kituo kimoja tokea alipopandia, akatoa kipisi cha sigara kutoka kwenye mfuko wake wa shati, akakiwasha na kuanza kukivuta.
Abiria na wqahudumu wa daladala tulimsihi azime kwa kuwa anahatarisha afya zetu, akagoma na akawa akiporomosha matusi kwa sauti ya ulevi.
Nimekereka kwelikweli, na nimeamua kuteremka kwenye hilo gari kabla sijafika kule niendako.
Kweli Tanzania hamna polisi, ila yunifomu za polisi

Mngempeleka kituo cha polisi
 
kama ni ng'ekuwa mimi ning'e izima hiyo sigara na siyo kushuka kwasababu hata kisheria anamakosa...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom