Polisi feki adakwa Mwanza

wang'ambo

Senior Member
Nov 29, 2015
113
27
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Ahmed Gabo umri wa 22 kwa tuhuma za kukutwa amevaa sare za jeshi la Polisi kinyume na sheria, Gabo anadaiwa kuiba sare hizo, millardayo.com na Ayo TV imempata Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza, Ahmed Msangi na amezungumza haya………

>>‘Kwa jinsi alivyovaa sare za Polisi kofia, mkanda mpaka viatu na hali aliyokuwa nayo ni kinyume na askari anavyotakiwa awe na maadili aliyokuwa anaonyesha sio ya Kipolisi

>‘Tumemhoji kwa haraka na amekiri ni kweli hizi sare sio zake na wala hajawahi kuwa kwenye mafunzo yeyote ya kijeshi bali ameiba begi la muumini ambae alikuwa anaswali katika msikiti siku nne zilizopita huyu muumini ni Askari Polisi wa hapa mkoani;- Ahmed Msangi
mi.png

Source Millardayo

mi.png
 
Amejipa kesi kwa gharama nafuu kabisa, kwa muonekano wake ilikuwa lazma akamatwe mapema sana baada ya kuzivaa hizo sare
 
Hawa police naona wako tofauti na wajeda,wajeda wakikukamata na sare zao wanakutifua vibaya sana wakikuachia hurudii tena kutinga sare zao
f7ce842da85a258e0733de28b46603ad.jpg
b812121469af052071c7cab5756640c3.jpg


-Nyerere-
 
wapeni watu ajira aya mambo yatapungua hakika.!!
Wewe nawe hebu achwa ujinga hapa, huyo hata kama ajira zinatoka atapata ajira gani? Maana inaonesha kabisa ni std 7 failure, yaani nguo za Polisi unavalia suruali ya kiraia ndani? Unatupia kwenye kiatu chochote tu? Mkanda unafunga tambara? Mwacheni akanyee debe tena wawahishe hiyo kesi hakuna cha upelelezi eti haujakamilika! Alifikri nguo za Polisi huwa zinatupiwa tu?!!
 
Back
Top Bottom