POLISI DODOMA YAWASHIKILIA AKINA SANGOMA a.k.a LAMBA LAMBA GROUP KWA UTAPELI

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=3][/h]

Baadhi ya watuhumiwa wa utapeli wa kufanya waganga wa kienyeji wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi wakiwaonyesha waandishi wa habari pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen hawapo pichani. Kutoka kushoto waliovaa kawaida ni Mkude S/O Mwenda 32 yrs, Mkulima, na Joseph S/O John miaka 27, Mkulima, wote wakazi wa Mkoka – Kongwa na SALEHE S/O OMARI, mwenye umri wa miaka26, mkulima wa Songe Kilindi Mkoani Tanga aliyevaa lubega nyekundu kwa nyeusi na ndani ana fulana mistari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani vyeti feki vya watuhumiwa wa kundi la Matapeli la LAMBA LAMBA vyeti hivyo ni vya (UMAWATI )– cha mtuhumiwa DK. Shabani R Kisoma amacho kirefu chake ni UMOJA WA WAGANGA WATAFITI WA MAGONJWA SUGU UKIMWI NA TIBA ASILIA TANZANIA, na (CHAUMUTA) – Cha mtuhumiwa anayejiita DK. Hussein Shomari Mabogo, ambaye amekamatwa , kirefu chake ni CHAMA CHA UTAFITI WA MAGONJWA SUGU NA UKIMWI KWA TIBA ASILIA.



Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa tisa wa utapeli wanaojifanya Waganga wa Jadi na Tiba Asilia kwa kuwalaghai wananchi katika vijiji mbalimbali kisha kuwatapeli na kusababisha hofu, na uvunjifu wa Amani miongoni mwa wanakijiji mkoani humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alisema watuhumiwa hao wanajiita LAMBA LAMBA walikamatwa juzi katika Wilaya ya Kongwa, katika kijiji cha Mkoka baada ya Polisi kupata taarifa kuwa, wanakijiji hicho kuwavamia katika nyumba waliyofikia na kutaka kuwauwa.

”Matapeli hawa wametokea Mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na Marogoro, na kuvamia mkoa wetu, kisha kufanya utapeli wao na kuzusha hali ya hofu na isiyo ya kawaida kwa wanakijiji wa maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma”. Alisisitiza Kamanda Zelothe Stephen.

Aidha Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema, Kundi hilo la LAMBA LAMBA limekuwa likichochea Chuki na Uadui miongoni mwa wanajamii kwa kufanya vitendo vya kupandikiza vitu nyakati za usiku, halafu baadae mchana wanakwenda kuvifukua na kudai wanabaini wachawi na kutoa uchawi katika kila nyumba kwa madai ya kualikwa na wazee wa Kimila.

Kamanda Zelothe Stephen alisema Matapeli hao, wamedai kualikwa na wazee wa kimila chini ya Mwenyekiti na Katibu waitwao SAMANDARO S/O? Na CHIPENDWA S/O? Na kupewa makazi katika nyumba mbili za ukoo wa MAPUGA S/O? Ambazo zinasimamiwa na Bw. SOSPETER S/O MAPUGA.

Akizungumza moja ya tukio lilozua hofu na kusababisha uvunjifu wa amani alisema katika shuguli zao walipita kila nyumba katika kijiji walichodai kualikwa na wazee hao lakini walipofika katika nyumba ya MESHACK s/o MAPUGA aliwakatilia kuingia kwake hivyo waliondoka kwenda katika vijiji vingine.

Alisema Baada ya kuondoka hapo Mtoto wa Mzee MESHACK S/O MAPUGA aitwaye MARTHA S/O AINEA MAPUGA MIAKA (34) mgogo mkazi wa kijiji cha Mlanje alianza kuumwa tumbo kisha kupelekwa zahanati ya Mkoka na hatimaye Hospitali ya wilaya Kongwa ambapo madaktari walithibitisha kifo cha binti huyo kutohusiana na imani za kishirikina lakini kwa bahati mbaya alifarikia dunia usiku wa tarehe 10/06/2012 akiwa Hospitalini hapa.

”Kifo hicho kilileta sintofahamu katika familia hiyo, iliyopelekea kufikiri kwamba kikundi cha LAMBA LAMBA walihusika na kwamba ndio tatizo kwa sababu za imani kishirikina.”aliongeza Bw, Zelothe Stephen.(Na Na. Luppy Kung'alo, Polisi Dodoma na Full Shangwe Blog)

 
Back
Top Bottom