Polisi awapa wanafunzi silaha na kupiga nayo picha, ni dalili za matumizi ya sigara kubwa?

kwitega

Senior Member
Apr 10, 2012
166
49
Wakuu,

Nimeshangazwa na kitendo cha askari mmoja jijini Mwanza mwenye cheo cha Konstebo kuwapa wanafunzi bunduki kisha kupiga picha wakiwa wamebeba silaha hiyo kwa kupokezana huku wengine wakiwa wameishika mithili ya askari walioko kwenye mafunzo ya kulenga shabaha.

Kitendo hicho kilitokea juzi kwenye shule ya msingi Tambukareli iliyoko kata ya Butimba jijini Mwanza mara baada ya wanafunzi hao kumaliza mitihani yao ya darasa la saba.

Binafsi nimeziona picha hizo huku askari huyo akiwa amesimama pembeni huku akiwa amelegeza macho hali ambayo kwa haraka haraka unaweza kusema huenda alikuwa ametumia sigara kubwa. Ninavyofahamu mimi, askari haruhusiwi kutoa silaha kwa mtu awaye yote.

Wakuu, kumekuwapo matukio mengi ya Polisi kutumia silaha ovyo na kusababisha mauaji ya raia wasio na hatia. Je, kitendo cha askari kutoa silaha kwa wanafunzi na kupiga nayo picha, yaweza kuwa moja ya uthibitisho kuwa baadhi yao wanatumia sigara kubwa na kuna umuhimu wa kupimwa akili kabla ya kuajiriwa kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama? Tujadiri kwa hoja.
 
Ngoja tusubili taarifa ya kamisaa kisha tutaangalia adhabu ya kumpa huyo police,nadhani tutamfungia mwaka1 asiguse bunduki.
 
Mkuu uwezekano wa picha zenyewe km upo weka tujionee wenyewe pia tuje na michango isiyoegemea upande wowote kupitia picha.
 
Hawezi kuwajibika, kwani ametenda kosa gani? Yeye alikuwa anatekeleza sheria ya utii bila shuruti hivyo hawezi kujiuzulu ng'o! Mmeelewa? Kuna swali la ziada kwangu mimi kamanda Kamu....?
 
si zilinunuliwa kwa kodi ya wazazi wao? acheni watoto waenjoy jasho la wazazi wao
 
"Hilo sio kosa la Kamuhanda kujiuzulu".....kosa la kujiuzulu ni lipi?maana kuua au kutoa uhai wa mtu.....sidhani kama lina mjadala!
 
Ukivuta kile kitu bila kusema Bangi nibangue akili yangu niachie umekwisha
 
Huyo polisi nadhani hakuwahi kuhudhuria mafunzo ya upolisi pale chuoni moshi bali aliletewa cheti cha kuhitimu mafunzo nyumbani kwa sababu ni mtoto wa afande Kamu.......! Kwani si unaona mwenyewe akili zake ni kama za babake?
 
hao ndio polisisiem, mtajibeba na ukimfatafata anakulipua kamanda atasema umepigwa na kitu chenye ncha kali
 
Back
Top Bottom