Polisi awania uongozi NEC ya CCM, akamatwa...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Polisi anaswa akiwania uongozi UVCCM

24 October 2012 | Imeandikwa Lilian Lucas, Morogoro

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma, linamshikilia askari wake, F 7961 PC Stanley Mdoe wa Kituo cha Polisi Mvomero kwa tuhuma za kujihusisha na masuala ya siasa na kushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Nec) kupitia kundi la vijana.

Askari huyo pia anatuhumiwa kutumia ubini wa jina la Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kama baba yake.

Habari zilizopatikana kutoka mjini Dodoma zinadai kuwa askari huyo aliyejitambulisha kuwa yeye ni mtoto wa mkuu huyo wa mkoa, akijitambulisha kwa jina la Stanley Bendera, alikamatwa juzi jioni wakati wa uchaguzi wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ukiwa unaendelea mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, askari huyo akiwa amevalia sare za chama hicho tangu siku ya kwanza ya mkutano huo alikuwa akiomba wajumbe wa mkutano huo wampigie kura katika nafasi ya ujumbe wa Nec kupitia Mkoa wa Morogoro akiwa na wapambe wake ambao wengi wao walitokea mkoani humo.

Ilidaiwa kuwa askari huyo alikuwa amepamba gari lake kwa picha zake zilizokuwa zimeandikwa Stanley Joel Bendera jambo lililosababisha baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaomfahamu kutoa taarifa kwa maofisa usalama waliokuwapo eneo hilo na Polisi Mkoa Dodoma ambao waliweka mtego wa kumkamata.

Mbali ya kukamatwa, askari huyo hakushinda katika nafasi hiyo. Awali, ilidaiwa kuwa askari huyo aliomba likizo isiyokuwa na malipo ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi huo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema: "Sina taarifa ya askari huyo kujihusisha na siasa."

NAONA SASA POLISI WAMETAKA KUDHIHIRISHA WAO NI POLICCM
 
kazi kwelikweli. kila siku watu tuna sema lisemwalo lipo, sasa watu wameshuhudia kwa macho yao kuwa hili ni jeshi la ccm, POLICCM.
 
Labda ni mtoto wa nyumba ndogo ya Joel Bendera. Bendera ni mwanamichezo na kada wa CCM, sifa tosha kumiliki nyumba nyingi. Mkuu weka picha yake tuwafananishe na J Bendera
 
Wapo wangapi wa aina yake ambao wamepita katika chaguzi zetu. Huyo amebainika kwa kuwa mjinga na kuanza kutumia na majina ambayo siyo yake. Huko NEC kuna nini ambacho huku nje hatukijui hadi mtu aamuwe kuacha kazi yake ili aweze kuwa mjube wa NEC?
 
Kila kitu sasa kipo wazi. Hata SAID MWEMA, SULEIMAN KOVA, DCI MANUMBA, FAUSTINE SHILOGILE na MICHAEL KAMUHANDA wana kadi za ccm
 
Nope. Siasa zinalipa kuliko ajira aliyonayo, ni hilo tu. Otherwise hata akina Mh. Kigwangala wangekuwa wanakamata mikasi.
 
sasa wanataka yeye atokeje.....kila siku wao watifua raha kila siku.
 
Ndio ujue siasa ni ajira inayolipa tz ndio maana watu wanauwana wakiangia huko.
 
James Kombe je? Jiulize kadi ya CCM aliipata lini?

Swali la msingi sana maana kujihusisha kwenye siasa kwa viongozi wetu wameangalia tu wakati mtu yupo katika cheo flani wakati kiukweli kuna wastaafu wengi wa jeshi wameshiriki kwenye chaguzi za CCM nyingi kiasi kwamba binafsi ninaamini walikuwa wanachama wa CCM pindi walipokuwa na cheo kwa sababu mpaka unateuliwa na chama una uzoefu katika chama kwa miaka kadhaa na ndio maana wengine wakaachwa ukachaguliwa wewe.

Inanikumbusha kuna kanuni moja watu elimu huitumia kuwaadhibu waalimu though kwa maadili ya siku hizi sidhani kama inatumika maana ilikuwa mwalimu kama atakuwa na mahusiano na mwanafunzi wake mwaka mmoja baada ya kumaliza shule ilikuwa by assumption kwamba alikuwa anamchukua even alipokuwa shule. Hivyo inabidi hata kwenye hili WALE WATU WOTE HASA WALIOPO KWENYE TAASISI NYETI KAMA MAJESHI KUTOJIHUSISHA KWENYE SIASA PINDI WAWAPO MADARAKANI PIA INCASE WAMESTAAFU WAJIHUSISHE KWENYE SIASA MIAKA 5 BAADA YA KUSTAAFU. Ona tulikuwa na mwanasheria (Chenge) wa serikali ambae tunaambiwa anatakiwa awe neutral lakini baadae tukasikia mbunge Bariadi
 
Wanamuonea huyu sababu ni cheo kidogo yale mabazazi...TIBAIGANA,MBOMA, na KOMBE wao hawakuchukuliwa hatua tena TIBAIGANA alikuwa anajinadi kuwa ni kada wa siku nyingi wakati anaomba kura za wajumbe wa CCM kule MULEBA....shame on this poor democratic goverment.
 
Ni kweli mkuu inabidi hawa jamaa tuwapige pini wajihusishe kwenye siasa miaka 5 baada ya kustaafu ili waweze kuwajibika kwa wananchi.
 
Nope. Siasa zinalipa kuliko ajira aliyonayo, ni hilo tu. Otherwise hata akina Mh. Kigwangala wangekuwa wanakamata mikasi......

Ni kweli maana siku hizi dhana ya uongozi ni kujitolea imekufa hivyo tutaendelea kupata viongozi wabovu mpaka basi maana watu wanaingia kwenye siasa kama ni sehemu ya NITOKI VIPI hivyo kunakuwa na ushindani mkubwa mno.
 
Hii sasa imekuwa sera yao ukitaka uongozi CCM lazima uwe na JINA au PESA basi. Mwenzangu na mimi mhh!!!
 
Huu ni uonevu mbona hata John Tendwa ni kada mwaminifu wa CCM na anayo kadi? sikubaliani na hizi Double Standard.
 
Wamemuonea tu huyu, wangeanza kuwakamata kina Mwema, Kamuhanda, Kova, Andengenye na wenzao wote kwanza. Maana wao wanatekeleza majukumu ya chama kwa nafasi zao bila kipingamizi.
 
Kitu kingine cha kufanyia marekebisho MAKUBWA ni hilo li PGO lao.Ni bovu mno,kwa sasa mie naona huyo dogo kaonewa tu.Namba yake ni F 7961 PC na bado ana cheo hicho wakati kama sikosei sasa wapo hadi wenye H.Hapo ndo tatizo lilipo.Dogo kala lindo hadi kazidiwa.Lol
 
Back
Top Bottom