Polisi arusha kuna-ni......?

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Hivi karibuni walikamata fedha zilizoibwa (mamilioni), juzijuzi wakakamata shehena ya mahindi zaidi ya tani 600, cha kushangaza vitu hivi vyote vimeyeyuka mikononi mwao, huko mpakani polisi hao hao wamekamata maroli yakitaka kuvuka mpaka yakiwa na mahindi hayohayo ambayo yalikuwa chini ya ulinzi wao. inakuwaje polisi arusha .........?
 
Nchi yetu ni zaidi ya tuijuavyo!

Hasa ikiongozwa na mikoa hizi:

1) Arusha
2)Mbeya
3)Moshi
4)_
5)_
6)_
Hebu endelezeni hapo pa wazi wadau!
 
ongeza kuwa waliwaua vijana wawili wasio na hatia (wakidai ni cdm)
wakamkamata Mh. Lema na kumfanyia waliyomfanyia.

wengine walisema na kueleza kuwa hakuko sawa lakini wasiopenda kusikia wakapuuza, na waendelee kupuuza mpaka mwisho wa dunia
 
Ndio wauza mirungi wakubwa Arusha tena kwa bei chee mbaya hivyo kuwasabashia wajasiriamali wengine wa mirungi hasara.
 
Hivi karibuni walikamata fedha zilizoibwa (mamilioni), juzijuzi wakakamata shehena ya mahindi zaidi ya tani 600, cha kushangaza vitu hivi vyote vimeyeyuka mikononi mwao, huko mpakani polisi hao hao wamekamata maroli yakitaka kuvuka mpaka yakiwa na mahindi hayohayo ambayo yalikuwa chini ya ulinzi wao. inakuwaje polisi arusha .........?

Hawa wamegeuka mbuzi wa kafara tu. Kazi yote wanatumwa na wakubwa zao Dar kisha wanagawana. Ni bahati mbaya kwa haya wamekamatwa. Pia wapo askari wa Moshi. Kupangwa kazi mikoa hiyo ni lazima ununue nafasi hizo kama hamjui.
 
Nadhani askari wa Moshi wanaweza kuwa wanaongoza kwa rushwa na wizi wa mali za watu,pale kituo kidogo cha polisi Himo, polisi walitokomea na zaidi ya tani 30 za sukari iliyokamatwa ikielekea Kenya.
 
Kwani polisi sio watu. Polisi pia ni wezi. Ndiyo wanaongoza hata kwenye kupokea rushwa. Just immagine. Kama wakubwa wanaiba utadhani wataweza kuwakanya wadogo?
 
Kwani polisi sio watu. Polisi pia ni wezi. Ndiyo wanaongoza hata kwenye kupokea rushwa. Just immagine. Kama wakubwa wanaiba utadhani wataweza kuwakanya wadogo?

Umenena Mkuu!!!! Ila upande wa kuongoza kupokea rushwa nadhani ni Wanasiasa wetu...Makatibu wakuu...wakurugenzi..
Makamishna...ndipo unawakuta Polisi, mahakimu, madaktari na manesi, PCCB, Uhamiaji, ardhi...na wengineo
 
ongeza kuwa waliwaua vijana wawili wasio na hatia (wakidai ni cdm)
wakamkamata Mh. Lema na kumfanyia waliyomfanyia.

wengine walisema na kueleza kuwa hakuko sawa lakini wasiopenda kusikia wakapuuza, na waendelee kupuuza mpaka mwisho wa dunia

kwani police walimfanyaje uyo lema?au ndio tayariiii washamgusa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom