Polisi apata kichapo

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,591
POLISI mmoja kati ya watatu waliokuwa kwenye doria, amepigwa na kujeruhiwa na mtuhumiwa walipokwedna nyumbani kwake (mtuhumiwa) kumkamata.

Tukio hilo lilitokea saa 1:00 usiku wa kuamkia jana Mtaa wa Mbagala Mlandizi, wilayani Kibaha, mtuhumiwa aliyempiga askari huyo anadaiwa kulawiti alifuatwa kupelekwa kituoni cha polisi.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ernest Mangu, alisema askari aliyejeruhiwa ni E. 4420 Sajini Dady, huku mtuhumiwa akitajwa kuwa ni mkazi wa Mbagala, Mlandizi.


Mangu alisema wakati wa ukamataji huo, mtuhumiwa alikataa kutii sheria na kusababisha vurugu zilizopelekea kumjeruhi kichwani polisi kwa kitu chenye ncha kali.


Alisema askari aliyejeruhiwa alipelekwa Hospitali Teule ya Tumbi, alipatiwa matibabu na kuruhusiwa na hali yake inaendelea vizuri.

Hata hivyo, polisi walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituoni na kwamba, zaidi ya kulawiti amefunguliwa kesi nyingine ya kumjeruhi askari wakati akitekeleza majukumu yake.

E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
walimwonyesha kitambulisho? Halafu mambo ya kukamatana usiku usiku,labda alijua ni majambazi!

Ila acha akatumikie mvua yake,jitu zima linalawiti!
 
walimwonyesha kitambulisho? Halafu mambo ya kukamatana usiku usiku,labda alijua ni majambazi!

Ila acha akatumikie mvua yake,jitu zima linalawiti!

Jamaa sio mzima. Mimi nahisi atakuwa na mapepo tu. Mbona mademu wapo wa kumwaga. Imekuwaje hadi alawiti?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom