Polisi Anapoua Raia Sheria Inasemaje?

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Wakuu, hasa mliobobea kwenye fani ya sheria, naomba tuelimishane katika hili.

Mimi katika kupitia pitia vitabu vya sheria nimeona haya, naamini kuna mengine.


Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 20 ibara ya 21
21.-(1) Afisa polisi au mtu mwingine hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kutumia nguvu zaidi au kuvunja utu wa mtu huyo zaidi ya ilivyo lazima kufanikisha ukamataji au kumzuia utorokaji wa mtu baada ya kukamatwa.
(2) Bila kupunguza matumizi ya kifungu kidogo cha (1), afisa polisi hatatakiwa, wakati wa kumkamata mtu, kufanya kitendo kinachoweza kusababisha kifo kwa mtu huyo, isipokuwa kama afisa polisi anaamini kwa sababu za msingi kwamba kufanya kitendo hicho ni muhimu katika kulinda maisha au kuzuia madhara makubwa kwa mtu mwingine.


Sheria ya Kanuni za Adhabu Sura ya 4 ibara ya 18B.-
(1) Katika kutumia haki ya kujilinda mwenyewe au kumtetea mtu mwingine au kutetea mali, mtu atatakiwa tu kutumia nguvu za kiasi zinazostahili ulinzi husika.

(2) Mtu atawajibika kuwa ametenda kosa la jinai kwa kosa lolote litakalotokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda au anapomlinda mtu mwingine au anapolinda mali.
(3) Mtu yeyote atakayesababisha kifo cha mtu mwingine kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi katika kujilinda, anakuwa ametenda kosa la kuua bila kukusudia.

Karibuni tuelimishane
 
Simu ya Tundu Lisu nimeipoteza, naamini hili liko wazi katika sheria zetu tulizorithi kwa wakoloni waingereza isipokuwa sisi tumezifanya kama furniture hatuzitumii.
 
Simu ya Tundu Lisu nimeipoteza, naamini hili liko wazi katika sheria zetu tulizorithi kwa wakoloni waingereza isipokuwa sisi tumezifanya kama furniture hatuzitumii.

Kwa kulindana, wakati mwingine uwezo mdogo wa mahakimu/majaji, kwa kuchaguana kwa vigezo visivyoeleweka.
 
Back
Top Bottom