Polisi aliyekataa Rushwa apewa zawadi 4m

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
pix%2Bb.JPG
pix%2Bc.JPG

  • Askari namba E. 7235 PC John Anthony Mwesongo wa kituo cha polisi cha Polisi Kiwanja cha ndege cha Mwalimu Julius Nyerere ambaye ni mtunza vielelezo wa kituo hicho, akionyesha hundi ya T. Sh. 4,000,000 motisha baada ya kukataa rushwa ya dola za kimarekani 3,000 na watu waliokamatwa na madawa ya kulevya waliomtaka abadilishe vielelezo hivyo.
  • Hundi hiyo alikabidhiwa na Inpekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema Jana (13/3/2010) katika ukumbi wa maofisa wa polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam. (Picha Na Hassan Mndeme- Jeshi la Polisi)
  • Hongera PC John Anthony Mwesongo. Wewe ni mfano wa kuigwa!
 
I hope ni kweli isiwe ni mchezo wa kuigiza!!! Kama ni kweli hongera sana afande.
 
Mi naona kama wanawapima imani tu...Sasa wakikutana na mtu aliyekataa rushwa ya 50ml watampa ngapi?? Naona mambo mengine ni kujifunga vitanzi tu. Mi nadhani suala kubwa hapa walitakiwa kuboresha mazingira ya kazi ya polisi kama vile mishahara, marupurupu, makazi na huduma nyinginezo. Mbona JWTZ wanawekwa vizuri tu kulinganisha na hawa Polisi wetu??! UKienda pale lugalo kwenye super market ya jeshi vitu viko bei chini ajabu kulinganisha na mtaani, acha dula lao lingine pale kambi ya Twalipo achilia mbali bia, sigara na vinywaji vingine ambavyo bei zake ziko chini sana. Sijui kwanini isiwe na polisi nao.
 
Naungana na wewe kimsingi kwamba ukimlipa mshahara mzuri mtumishi atajenga tabia ya kuheshimu kazi yake na kuepuka vitu vinavyoweza kuhatarisha kuikosa kazi hiyo. Wakati huo huo watumishi ambao wanakwenda kinyume na kanuni na maadili ya kazi wakiwa wanawajibishwa ipasavyo na siyo kuhamishwa kupelekwa sehemu nyingine (mfano Trafiki kupelekwa kuwa FFU)
 
Huu ndo mfano wa kuigwa kama ni kweli, hongera sana mzeia, kaza buti, songa mbele tumtokomeze huyu mdudu Rushwa.
 
Kama ni kweli na sio kiini macho hongera ila isiwe ni nguvu ya soda tu na kupima imani kwa maafande wengine.
 
mmh kumpa hadharani hawa wanataka apate "New best friends and long lost relatives"

Vizuri hii yatia moyo.
 
Hiri riafande narijua.... ni kweli hii ilitoke Dar Airport! HONGERA sana... Wote tukiwa kama hiri riporisi.. angalau tutawin.
 
Hongo ilikuwa kidogo ukilinganisha na issue yenyewe, huenda alitaka apewe zaidi ndo maana kaitolea nje hiyo.
 
hongera zake lkn ni wajibu wake na wa kila mtanzania kutopokea wala ktoa rushwa bila kutegemea kupewa zawadi!
 
Big Up kamanda... ila nna wasi wasi sio siku nyingi tutakusikia maeneo Sumbawanga,,, au Chanjamjawiri Pemba, tena ukiwa mkuu wa kituo..
nji hii
 
kweli ni wakwanza kama ni kweli pia naona hana njaa kama wengine maana hawa jamaa kwa supu na coka noma wanamaliza ishu kiulaini
hongera mjeda
Conquest -ikwaju chachandu au juice
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom