Police Iringa yaikaribisha CHADEMA kwa ajili ya M4C

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
TANZANIA DAIMA:

Polisi waikaribisha M4C

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP), Michael Kamuhanda, amesema hawatakuwa na sababu ya kuzuia mikutano ya CHADEMA baada ya shughuli za sensa kumalizika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamuhanda alisema tangu siku ya kwanza CHADEMA walipoingia mkoani humo hali ya utulivu ilikuwa ni nzuri na hakukuwa na matatizo yoyote mabaya waliyosababisha.


"Tunajua watafanya mkutano wao Septemba 2, mwaka huu, wilayani Mufindi, hatuna sababu ya kuzuia hilo labda ijitokeza sababu ya kiusalama, kwa kuwa hata Dk. Slaa nimezungumza naye na akaniambia wako salama na amefurahia walivyopokewa kifalme katika mkoa huu," alisema Kamuhanda.


Akizungumzia sababu ya kuimarisha ulinzi, Kamanda Kamuhanda alisema hatua hiyo inatokana na hali halisi ya kisiasa kwa sasa na kwamba polisi wana wajibu wa kuchukua tahadhari kuhakikisha usalama unakuwepo.


Alipoulizwa kama jeshi hilo linatumiwa na viongozi wa CCM katika kuhakikisha mikutano ya CHADEMA haifanikiwi, Kamuhanda alisema si kweli kwani hata baadhi ya viongozi wa CCM wakiwamo wabunge wa mkoa huo hajawahi kukutana nao.


Tangu kuingia kwa viongozi kadhaa wa CHADEMA mkoani Iringa, jeshi hilo limekuwa katika tahadhari kubwa kwa hofu kuwa wanaweza kufanya mikutano kabla ya sensa ya watu na makazi kumalizika.
 
sep 2 si mbali Subira yavuta heri

watu wote wa Iringa wekeni ratiba zenu vizuri ili muweze kuhudhuria mkutano huu

M4C DAIMA
 
Huyo kamanda ni afadhali amepima upepo mapeema,upepo hauzuiliwi kwa mkono
 
Serikali wafanye tathmini kama zoezi la sensa lilifanikiwa. Of coz mie mpaka sasa sijahesabiwa pamoja na maandalizi kibao ili nihesabiwe!

Kama sensa haikufanikiwa angalau kwa 66.3% il-hali CDM ilisimamisha M4C kwa vile Polisi walituhumu kuwa inavuruga zoezi la sensa basi itabidi Polisi na CCM waiombe CDM radhi. Haitoshi tu kuwaruhusu kuendelea na mkutano kwani hiyo na haki na wajibu wa CDM kikatiba na kimaudhui.

Na je kwani CDM ilikuwa inafanya M4C ktk mikoa yote kwa wakati mmoja?
 
yaani walijua wameikomesha CDM,kumbe ndio wameipa muda wa maandali wa kutosha,na watu ambao wangekosa siku hiyo wamewasaidia kuhudhuria.
 
Vizuri ametumia busara .hataki kufanya ujinga kama ule wa mwenzie wa morogoro!
 
Back
Top Bottom