Police Arusha

Toka nikiwa Mdogo nilikuwa nashuhudia Dingi alivyokuwa akimnyanyasa mama kwa Vipigo
mchana na usiku. mimi na ndugu zangu "sijui wao walikuwa wakifikiria nini kuhusu vitendo
hivyo" tuliishia kulia na kuwaamua, yanaisha.

Maisha yaliendelea mpaka nilipokuja fikisha miaka 23 nikiwa chuo tayari, wakati huo manyanyaso
yalikuwa yameongezeka, na sasa alikuwa amehamishia unyanysaji mpaka kwa madogo,

By then, ukizingatia alikuwa amekwisha anzisha na kamchezo kakutokuijali familia kwa vitendo
vya wazi kabisa, school fees halipi, mtu akiugua yeye ndo kwanza anahama home ka wiki
hivi arudi infact hali ilikuwa imekuwa tete, mtaani walikuwa wakiona imepita wiki bila fujo home
wanajiuliza kuna tatizo gani.

Siku ya ukombozi ilikuwa namna hii.
Dingi kapotea nyumbani ka wiki hivi, siku hiyo asubuhi anarudi, mama yuko anaosha vyombo,
baada ya kuwa tumemaliza kunywa uji, Baba akafika na kumkanyaga mama mgongoni mpaka
akaangukia vyombo.

niliiona picha kwa macho yangu mwenyewe, hakukuwa na kubadilishana kwa maneno wala nini,
hata mother alikuwa hajamuona dingi wakati anafika.

Kijana nikapata akili, nikaamuka na kumuangushia kichapo cha kutosha mzee, nikampa za usoni
za kumsotosha , kumbe madogo nao walikuwa ni kama wanasubiri mtu wa kuanzisha, wakaamuka
vijana kwa mabinti, tukamzibiti mpaka akakimbia kuomba msaada kwa majirani.

hakurudi nyumbani mchana huo, akatokea usiku na jaziba za kutosha na kampani ya baba zetu
wadogo. tukawafungia kazi kama kawa, kichapo wote.

Toka siku huyo, sijawahi kumuona mama analia.Hii ni true story ya Maisha Yangu,
sioni hatari kuiweka hapa wala sisuntwi na nafsi yangu kwa nini namwaga mchele
hadhari sababu it happed, na majirani zangu wote wanajua, na ninajuwa huwa
wanaizungumzia hii issue sana tu.

Naomba ili liwe kama somo kwa serikali.
 
Hata polisi ni waTanzania wenzetu hasa waliopo Arusha wanaishi uraiani na raia wanaowapiga mabomu kila siku watoto wao wanasoma na watoto waathiriwa wa mabomu waandamanaji wengi ni ndugu,jamaa na watu wanaokutana nao kila siku kwa mtu anayetumia akili hawezi kutekeleza amri za kijinga kama hizo labda kwa maafisa wenye ulinzi

heko polisi wadogo zindukeni.
 
habari za kutunga utazijua tuuuuuuuuuu mikwaruzo kibao

.
Hivi kweli inaingia akilini kwamba uwanja wa NMC ulikuwa umejaa watu halafu police wafanikiwe kukamata hapo 27 tu? Tia akili wewe!
.
 
hawa polisi wamechoka kabisaa na hii kazi ya kutukamata kamata kama mchezo ule wa kitoto wa hide and seek yani KOMBOLELA . Wamechoka kutumikishwa na ccm kwa maslahi ya hichi chama kuliko maslahi ya wananchi waliowaajiri
 
Back
Top Bottom