Poleni TISS tena... R.I.P "Dr"

Status
Not open for further replies.
MM mi natamani sana kujiunga na TISS ili niweze kulitumikia Taifa langu hasa kwa wakati huu uliojaa changamoto za kifisadi, nifanyeje?
 
RIP, Dk
Hivi inawezekana kuwa TISS imeyumba sana kimaadili? anyway
 
MM mi natamani sana kujiunga na TISS ili niweze kulitumikia Taifa langu hasa kwa wakati huu uliojaa changamoto za kifisadi, nifanyeje?
Unachekesha sana, ndg yangu ingekuwa ni miaka ya 80 hilo lingewewezekana, lakini kwa sasa ni mitoto ya mifisadi ndiyo ina fursa ndani ya idara hiyo.
 
Kibunago, nimekupata vizuri lakini lengo langu kwa bahati mbaya ni kugusa hasa nafasi yake katika utumishi wa Taifa letu. Nafasi ambayo huwa hawatunzwi. Nataka familia na watu wa karibu wanaomjua wajue kuwa some of us tunaappreciate his service to the nation.

Oh, well, very sad indeed; mashujaa kufa kifo cha kimya kimya inatia huzuni sana. Angekuwa mwanasiasa, au hata mwanamichezo, au mwanamuziki, hata asiye na CV ya kumkaribia angetangazwa na wananchi wangepata nafasi ya kumuombolezea at least familia yake wangejua kuwa mpendwa wao hakuwa nobody.
kazi nyingine kaazi kweli kweli... R.I.P Dr
 
Kwa mara nyingine, ninakuja na kutoa rambirambi kwa Idara ya Usalama wa Taifa kwa kumpoteza mmoja wa viongozi wa waandamizi ambao kwa kweli walikulia ndani ya Idara hiyo. Ni pigo kubwa kwa idara hasa kuondokewa na watu wenye weledi na waliojitahidi kufanya kazi yao licha tofauti ambazo zimekolezwa miaka hii michache iliyopita.

Bahati mbaya kutokana na kazi zao watu kama Dr. ni vigumu kuwaona viongozi wa kitaifa wakijitokeza kwenye misiba yao kwani wanalindwa na sheria ya TISS ya 1996. Ni hawa ambao majina yao na sifa za utumishi wao haziandikwi magazetini au hawawezi kuja na kulalamika hadharani jinsi mambo yalivyo magumu kitaifa. Ni hawa ambao huwa wanajikuta wananyong'onyea katika kuta za nyumba zao wasijue wafanye nini. Hawa wasio na watetezi wa wazi.

Na hii ndio sababu siwataji hawa wazee wetu ambao wametumikia taifa katika nafasi mbalimbali na hawakukubali kuwa corrupted kama kundi la baadhi ya vijana ambao wameingia kwenye idara siku za karibuni na sasa wamegeuka kuwa mabepari uchwara.

Natumaini siku moja idara hii itakuja kufanyiwa maboresho yanayohitajika haraka ili watu kama marehemu wazidi kuvutiwa kulitumikia taifa.

RIP - Amezikwa makaburi ya Kinondoni katikati ya mwezi wa kwanza baada ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu na kwa uadilifu.

RIP Dr..
Uko kitengo gani TISS?
RIP Lupembe
 
Du hii sheria labda tuisome vyema sote na kuomba msaada wa tafsiri Mahakamani:

Ningekuwa mimi ningeminya tu kutamka kuwa alikuwa ktk TISS na badala yake ningetaja jina lake wazi hapa na watu wangeendelea kutoa pole zao na faraja kwa wafiwa kama kawa. Maana jina lake linabeba Utu wake unaostahili kutambuliwa pasipo kujali alikuwa wapi kikazi au mwajiri wake alikuwa nani.

Aidha kama mpaka anafariki kweli kwa ujumla hakujulikana katika jamii kuwa alikuwa Intelligence Officer or Agent wa TISS basi jina lake lingetajwa tu hadharani hapa na kazi yake (Cover Design) ambayo kwayo jamii ilimfahamu na kumwona alivyokuwa akiwajibika ipaswavyo katika hiyo huduma nyingine aliyokuwa akiitoa katika jamii kama Mwanasheria au Daktari au Mkufunzi au mfanya biashara n.k

RIP M.
ok ok
 
Mkuu Mie kuna mmoja nimekuwa nikisali nae msikitini alikuwa ni mzee mmoja mwadilifu sana na mzalendo mwenye uchungu wa kweli na nchi. Kwa kweli nilikuwa namuadmire sana kama ndio huyo basi tumeondokewa na kifaa na wengi walikuwa hawamjui kweli.
Nadhani MM anayemzungumzia ni Mkristo
 
Ni siku nyingi kidogo simsikii Dr Hassy Kitine akizungumzia lolote nchi.

Hivi yupo Tanzania hii hii na wala asiseme neno kuhusu upepo wa mabadiliko nchi ninavyomjua msimamo aliyonayo juu ya mambo mengi yanayogusa jamii kitaifa????????

Hupo dunia ya ngapi ndugu yangu, soma soma magazeti. Mwadilifu yeyote hawezi kukaa kimya kama kuna uozo ndani ya CCM na serikali yake. Juzi juzi tu kabla ya uchaguzi Dr. Kitine alikwaruzana na CCM, This day likatuabalisha. Kwa maelezo zaidi gonga chini hapo...
chahali.blogspot.com/.../as-expectedccm-yamjibu-dkt-kitine.html
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom