Pole Sheikh Yahya....!

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,398
319
Pole shekh Yahya,
Uso kuwa na haya,
Na utabiri mbaya,
Ulojaa mabaya.

Umejiweka mtukufu,
Na huna utakatifu,
Una mawazo mafu,
Tena toka kwa wafu.

Unatuletea ya kuzimu,
Tuso abudu mizimu,
Umetufanya wazimu,
Na wenye fikra adimu.

Elimu yako ya kijini,
Waitangaza nchini,
Kuturudisha chini,
Na mambo ya kifirauni.

Ole tena ole,
Mungu atoa ole,
Usipoiogopa ole,
Hutaipata pole.

Na dini hayafanani,
Uletayo hadharani,
Maamuma wafundisheni,
Usituletee wanazuoni.
 
Alama za wanafiki, ni tatu bora uzijue
Katu nae haaminiki, japo ahadi azitoe
Pia na hasadikiki, hatumizi maaganoe

Yahaya Ni mnafiki aliye ja uzandiki

Alama yake ya pili, mnafiki ni mrongo
Maisha hana ukweli, wala mizuri mipango
Yake usiyakubali, atakukoroga bongo

Yahaya Ni mnafiki aliye ja uzandiki


Akiaminiwa hukhini, mnafiki ni sifaze
Hachi na hana dini, hudhulume nduguze
Usimtie nyumbani, na sirizo simjuze

Yahaya Ni mnafiki aliye ja uzandiki

Nne linipalo wasi, hasa linahusu kesho,
Hayupo mwenye tetesi, kipi atapata kesho,
Uchumaji wa nafsi, na hakuna mwenye fusho,

Mjuzi wa haya ALLAAH, hakuna atambuaye.
 
utabiri tu bana hana lolote. hard disk yake ilikwisha kufa siku nyingi, na atashije mjini pasi kuwadanganya na kuwatia hofu wasomi ili apate chakula yake na familia?
 
Kasema Maulana,
Tena kwa bayana,
Mzushi hiyana hana,
Muogopeni sana.

Hekima katujaaria,
Mabaya hakutuchuria,
Mema kuhudhuria,
Tena si kwa sheria.

Ni mfuasi wa she'twani,
Shekh yahya si utani,
Hayatufikisha peponi,
Tusiyafuate asilani.

Vita tumpigeni,
Tena tusimwachieni,
Ni kumruhusu shetani,
Atukaribie rohoni.
 
nasikia Mashabiki wa Simba Nusura wampige baada ya kudai kuwa Simba haitakuwa Bingwa ila Yanga ingekuwa Bingwa, sasa baada ya Simba kuwalaza Azam , Simba Tawi la Magomeni wakaandamana mpaka Home kwake kwenda kumshikisha adabu kwa utabiri wake kimeo, wao Simba wanadai alikua anawatilia Nuksi.
 
Ni mfuasi wa she'twani,
Shekh yahya si utani,
Hayatufikishi peponi,
Tusiyafuate asilani.
 
Ana IT expert ambaye anaweza kuwa ni member wa JF hivyo atamfikishia tu ujumbe huu
 
Tusimuharibie mwenzetu ka-utaratibu kake ka kuishi mjini. Ana wateja wake humu, wakifika hawatasema ujumbe huu, wataeleza shida zao tuu waibiwe hela.
 
Back
Top Bottom