Pole sana mama angu

mnyikungu

JF-Expert Member
Jul 26, 2009
1,960
2,464
pole sana mama angu: siku zote kila nikikupigia simu huna neno jingine zaidi ya mimi kuoa, kila siku mwanangu mwanangu unaoa lini? mwanangu oa, mwanangu nahitaji mkwe, mwanangu nahitaji mjukuu, agggg...... nimechoshwa na maneno yako kwa kweli, nimechoshwa kwa sababu ni jambo ambalo haliwezekani kwa sasa, mama miaka yetu siyo kama miaka yenu, wanawake wenzenu wa sasa hivi wako tofauti sana na nyinyi, mama uwekezaji wa ndoa ni mgumu kuliko uwekezaji mwingine wowote duniani, nimeona marafiki zangu wameoa ila ni mateso matupu na ndoa zao, mama nipe muda nikifika miaka sitini hivi nafikiri ndo utakuwa umri sahihi wa mimi kuoa MAANA NIMEONA MABINTI WANAPENDA ZAIDI WAZEE, kwa ujana wangu sijaona wa kumuoa, siyo kwamba sina macho hapana mama, ila tu mapenzi ya siku hz ni ya maigizo, ni copy n pasting toka kwenye tamthilia na movie za nje, wanawake siku hawana muda wa kuwahudumia waume zao ila wana muda wa kuihudumia mitandao ya kijamii kama facebook, twitter, na mingine mingi bila kusahau whatsapp, wanawake wanaojali vitu na siyo utu, mapenzi ya kweli mshayazika mama, mmeshidwa kuviambukiza vizazi vya sasa hivi, nisamehe bure mama angu, tutaongea zaidi nikija kukusalimia mwezi wa kumi na mbili. ni mimi mwanao FIKRA HURU ZINAZODUMU,

^^
Safi sana Mkuu,,
Tena andika..
Mabinti wa leo wanapenda pesa hawajali utu,
Tena wanapenda wao waoe sio waolewe,
Tena wanasema ikiwezekana mwanaume nae abebe mimba,
Tena neno utii kwa mume ni msamiati uliofutika ktk mioyo yao,
Kila siku wanatutukana sie maskini tusio na fedha kuwa ni wanaume suruali yaani kwao shida si za wote ni za wanaume tu,
Tena wanasema bila pesa,na elimu ya juu we boza,
Wanasisitiza kuwa Mke pesa,mapenzi ya dhati tukuletee huko kijijini.
Cc. Mrembo by Nature anaewaita wanaume mapu..mb na miss strong
^^
 
Kwa hiyo kazi yako wewe ni papuchi tuuu kwenda mbele? ? Eti kaka yangu?
 
Pole sana mama, maana hata mkweo na wajukuu sijui kama utafanikiwa kuwaona maana mwanao mnyikungu anataka kuoa uzeeni!
 
Last edited by a moderator:
Hii sentensi sijaielewa, lol!
Halafu hii kuoa ukiwa na miaka 60, duuu, utazaa vitukuu au utazaa kabla ya kuoa?
kuzaa ni dhana tofauti na ya kuoa, kuzaa unaweza ukazaa tu ila kuoa ni mbaka miaka hiyo
 
Hii sentensi sijaielewa, lol!
Halafu hii kuoa ukiwa na miaka 60, duuu, utazaa vitukuu au utazaa kabla ya kuoa?
maana yake ni hivi wanawake wa sasa hivi hawana mapenzi ya dhati kama ya mama zetu zamani, hawana uvumilivu, hawajui majukumu yao na nk
 
Sasa hivi ndoa imedumu Sana miaka mitatu! Ikifikisha mitano mnatakiwa mfanye golden jubilee maana hizi smart marriage siku hizi miaka miano ni sawa na 50 yrs enzi za mwalimu!
 
mama nipe muda nikifika miaka sitini hivi nafikiri ndo utakuwa umri sahihi wa mimi kuoa MAANA NIMEONA MABINTI WANAPENDA ZAIDI WAZEE

Ukifikisha miaka hiyo 60, je utaoa mwanamke wa namna gani?

Je, una uhakika gani kuwa utafikisha miaka 60?
 
Back
Top Bottom