Pole Nyonda Pole *

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Pendo ninakupa pole
Kwa yote yalokusibu
Nakupa haya na yale
Ni miye wako habibu

Pole nyonda pole, kutoka kwa pendo pole!

Yamenitoka machozi
Mawazo yajaa tele
Nimeshindwa fanya kazi,
Nikiyawaza ya yule

Pole nyonda pole, kutoka kwa pendo pole!

Jalali tumuachie
Tugange yaliyo mbele
Moyo wako utulie
Upate ya kheri tele

Pole nyonda pole, kutoka kwa pendo pole!

Moyoni mwangu tulia
Ewe nyonda wa milele
Tulia binti tulia
Nakusubiria kule

Pole nyonda Pole, kutoka kwa pendo pole

Na. M. M. Mwanakijiiji (Sauti ya Kijiji) BGM.


* Rafiki yangu mmoja mpenzi amenisimulia simulizi la huzuni na kunifanya niandike hiki kama sehemu ya faraja yangu kwake. Dedicated kwake huyo.
 
Mmh.. aisee nyinyi ni watu wazuri kweli maana hata kama nilikuwa na makosa mia nimejikuta nimesamehewa hivi hivi! LOL
 
Mzee mwanakijiji, nakuja na zangu pole,
natokea pale ujiji, najikongoja polepole,
nivuke vyote vijiji, nazileta zangu pole,

pole Nyonda pole, salaam zangu pokea.
 
Pole mwanakijiji.

Kumpa mtu pole yafaa atoaye pole naye apewe pole.

Ngoja nikakariri mistari.

ha hahaaaaaaaaa huna lolote, wenzio hizo fani zetu, mistari imekaa kichwani kama tebo ya pili!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom