Pole kwa Wajapan, lakini tujiangalie kama wote tumeenea!

meddie

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
434
125
Jamani wanaJF ni masikitiko makubwa kwa yaliyowapata rafiki na ndugu zetu wajapan! Lakini kwa haraka naomba kuuliza kama wote tumeenea! Isijekuwa kati yetu wamesafiri kwenda japan kwa mapumziko na kukutana na dhoruba hii. Hivi JK yupo hapa nchini? asijekuwa yupo japan!!
 
Kenya wametoa tahadhari kwa wananchi wake wa mwambao. Tz kimya, jamani mlioko kwenye mamlaka husika tusaidieni
 
Mhh inatisha kwa kweli hapa tu miili ya watu 300katia miji wa Sedai imepatikana,naona wanatoa tahadhari kwa watu wa mwambao wa bahari ya Pacific.
 
Kwa kweli inatisha sana. Kila mtu kwa imani yake (huwa sipendi neno "dini") tuwaombee ndugu zetu Wajapan; Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema awasaidie waweze tena kujenga upya nchi yao na waliopoteza maisha - RIP.

Kwa upande wetu, tumwombe Mola atuepushe na mabalaa hayo ya asili na kwa hakika tukimwomba kwa imani atasikia kilio chetu.

Nakulilia Tanzania, nakulilia Tanganyika, nakulilia Zanzibar nchi yangu; sijui hayo yakitokea hapa kwetu ewe Zanzibar sijui utafananaje? Hakika utafutika juu ya uso wa ardhi. Ee Mola tunusuru.
 
Back
Top Bottom