POAC Report iliyosomwa Bungeni leo

nimeona LAC/PAC kwa kweli ccm hawana akili kabisa; wazee wale kwisha kabisa yaani wanaimba wimbo full wa ccm. ngoja hii ya zitto niione
 
Wakuu, kwakuwa doc hii ni ndefu, nashauri watu wai-download as an attachment hapa chini

Nashukuru sana kwa kuiweka hapa, maana nimeisikiliza mwanzo mwisho wakati Zitto akiiwasilisha bungeni, hakika inaumiza, na aliniboa serukamba alipochangia.

Mkuu ile ya mrema nayo inasikitisha na ni nzuri sana ila msomaji wake hakupaswa awe mrema. kama unayo naomba utuwekee nayo, pia kama una video ya Tundu lissu nimependa alivyofloo.

Thanks again
 
Nimeisoma.Ni nzuri ila mapendekezo kuhusu sera ya uwekezaji wangeongeza pendekezo la umiliki wa makampuni kwa kuangalia uzawa ingekuwa vyema zaidi.ila mpaka hapa naona Kamati imefanya kazi vizuri,taaluma imezingatiwa
 
Wakuu tuisome kwanza kwa kina ndio tuchangie kusaidia Taifa letu maana Wabunge wetu wengine hata hawachangii
 
Watanzania tufikie mahala tuzipe recruitment agencies kazi ya kuteua wakurugenzi na mameneja wanaoongoza Mashirika ya Umma

Hata tukiingia ubia na wenzetu ambao tunafanya nao Biashara unakuta kuna tatizo la management kwa upande wetu.Ishuya Tazara ni good example kwa hili
 
Ni ripoti nzuri. Hata hivyo kuna vitu havijaeleweka, nitakuwa navitoa kimoja kimoja kila ninapokipata:

1. Ripoti inasema kati ya mashirika 156 yaliyowasilisha taarifa, 51 taarifa zake zilikaguliwa na kukamilika, na 105 zinaendelea kukaguliwa. Baadae ripoti inasema kamati imejadili kwa kina taarifa za mashirika 78 kati ya 105 yaliyokaguliwa! Confusion...
 
You are missing the point

This is not a report...this is an edited version of what politicians are given for public consumption

Ukitaka uhondo tafuta CAG report kamili nadhani ni pages zaidi ya 250
 
Na pia tusisahau kuna watu wanaochambua ripoti kwa kuangalia nani ka-present,let us be objective.Tuangalie contents za ripoti
 
Nashukuru sana kwa kuiweka hapa, maana nimeisikiliza mwanzo mwisho wakati Zitto akiiwasilisha bungeni, hakika inaumiza, na aliniboa serukamba alipochangia.

Mkuu ile ya mrema nayo inasikitisha na ni nzuri sana ila msomaji wake hakupaswa awe mrema. kama unayo naomba utuwekee nayo, pia kama una video ya Tundu lissu nimependa alivyofloo.

Thanks again
i cant believe ni wewe
 
Na pia tusisahau kuna watu wanaochambua ripoti kwa kuangalia nani ka-present,let us be objective.Tuangalie contents za ripoti

the difference hapa hakuna ripoti ila kuna hotuba

omba ripoti toka kwa wahusika utapewa
 
Naomba nieleze jambo moja. Hii ni taarifa ya Mwaka ya Kamati ya POAC. Ukiona hapo utaona ni mwaka wa fedha unaoishia June 30,2009! Taarifa ya CAG inayoishia june 2010 inawasilishwa Bungeni siku ya jumanne na baada ya hapo ndio Kamati zitapewa na Spika ili kushughulikia.

Kwa hiyo katika Taarifa hii hutakuta taarifa ya CAG maana imeshatoka na unaweza kuipata katika tovuti ya national audit office. POAC inatoa taarifa ya kazi kufuatia taarifa ya mwaka 2009.

Kazi ya kamati ni kuhoji na kutoa maelekezo, maagizo na mapendekezo kufuatia taarifa ya CAG. Kwa wale wanaotaka CAG report inayoendana na taarifa ya POAC waende kwenye tovuti ya CAG.

Kila la kheri
 
Ni kwa nini kamati imekagua ripoti ya CAG inayoishia June 2009 na sio 2010? Haioni kuwa inakagua vitu ambavyo ni too outdated?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom