Please...sema hata neno tu, waweza kumuokoa huyu mama!

hii ndoa imeingiwa na kidudu mtu kaka angu tena huyo dada ana afadhali mume anatoa matumizi wengine huwa wanakimbiwa kabisa hawapati matumizi wala watoto hawahudumiwi

Maty,

Hiyo haina ubishi kuwa kwani huyu mama ana ushahidi wote kwamba mume ana watu wengine wa nje. Anasema aliwahi kusome sms kwenye simu ya mume akataka kufa kwa vitu alivyokutana navyo. Hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini pamoja na kuamua kuvumilia mwanamume anamfanya kama vile siyo binadamu?
 
Dena Amsi, kuna wanaume wanajua kununa usiombe, kuna jamaa namfahamu kwa kununa ndo mwenyewe mpaka huwa najiuliza hivi huko nyumbani kwake inakuwaje kwa mke wake, kwa hiyo wala usimshangae huyo anaemnunia mkewe.

Mie hapa umeniacha hoi sasa dume zima linanuna ndani halafu inakuwaje sipati picha. Mmmmhh haya bwana lakini mwanaume kununa si poa
 
na chakula cha ucku anakipata?.....hizo ishu za kuondoka home ckubaliani nazo, y aondoke?

Mara moja au 2 kwa mwezi. Tena kwa hisani ya baba mwenye nyumba. Mama akiomba huruma anaambia mume hana nguvu za kugawa dozi mara nyingi kiasi hicho. Yaani hii issue imenimaliza kabisa.
 
ishu za wamama cku hizi kukimbizana na watoto kuhama zimepitwa na wakakti, abanane hapo mpaka kieleweke...

Ndo maana nilikuwa nakusubiri wewe. Actually package yangu ya counselling nilikuwa nataka kuilekeza kwenye kumlazimisha baba akae kwenye meza ya mazungumzo. Yaani mama ameanza kwa kuacha kumpigia pigia simu na kujipendekeza kwa mambo mengine (ikiwemo haki yake ya msingi ya ndoa) na sasa anasubiri kuliwasha la kumtaka baba atoe msimamo kama anataka ndoa iendele au la! Hiyo unaionaje?
 
Ningemshauri huyu mama arudi nyuma kuangalia ni wapi alikoachia nafasi mpaka haya kumkuta,aendelee kuwa mwaminifu katika ndoa na familia yake.Asijaribu naye kutoka nje ya ndoa maana ndio itakayofanya tatizo lisiishe.Kila jambo lina chanzo chake na kila jambo lina wakati wake.Laana isiyo na sababu haimpigi mtu,hivyo kutakuwa na sababu na ajaribu kuifuatilia kwa ukaribu akimwomba Mungu amkumbushe ni wapi alikoruhusu hali hiyo.Kuhama hama makanisa sio suluhisho kama asipotulia na kumsikiliza Mungu hapo alipo kuhusu shida yake.Na haiwezi kuondoka kwa mara moja kama anavyotaka,na ndio maana anahama hama inaonekana hana uvumilivu na anaamini mwanadamu badala ya Mungu.Tulia mama kuwa mvumilivu kwa kitambo wakati ukiomba kwa bidii Mungu atakufungulia mlango.Mume wako atatulia kama si yeye,hutaamini macho yako.
Usipende kushindana na mume wako,huenda unabishana naye mara nyingi hii pia humkimbiza mume nyumbani.Usipende kulinganisha mazingira ya mtu fulani na aliyo nayo mumeo either kwa kumwambia mbona fulani anafanya hivi etc hii ni sumu kwenye ndoa.
Au kuna wakati ulimropokea mume wako kwa kumwambia wakiitwa wanaume nawewe utakwenda kumbe yeye akachukulia serious na ndio maana iko hivyo.

Kuna sababu,haiwezekani mtu uende dukani ununue nguo tena kwa bei ghali halafu usiivae,lazima itakuwa na kasoro au ilimwagikiwa na uchafu.

Uhai wa ndoa yako mama uko mikononi mwako wala hakuna mchawi wala nini.TAFUTA CHANZO NA JIBU UNALO
 
Maty,

Una maana aendelee kukaa home na waendelee kuchangia kitanda kimoja kama maiti walioko kwenye friji ya mochuari?

Yeah babu hayo ndio majaribu shukuru mungu hayo hayajakutokea lakini humu duniani kuna majaribu acha kabisa na kama huyo dada ni kweli anasali ndio kabisa shetani anazidi kumkandamiza ili amuache mungu arejee kwake asithubutu kabisa kuondo ayazoee tu hayo matatizo na yataisha. Mkumbuke ayubu wa kwenye bible alinyang'anywa kila kitu na bado akaachwa na majipu mwili mzima huyo dada mume hataki tu kumpa kitu mahitaji mengine anapata mbona hayo ni majaribu kidogo tu
 
MOD mbona inaonekana niko banned.Kutoka kipindi cha uchaguzi mpaka leo?.Nifungulie Bwana niweze na mimi kutoa maoni yangu kutumia quick reply na sio mpaka nipitie Reply to topic ambayo ni njia ndefu sana,.
 
ishu za wamama cku hizi kukimbizana na watoto kuhama zimepitwa na wakakti, abanane hapo mpaka kieleweke...

si ndio hapo mtu uondoke kwenye nyumba yako uanze kuwazungusha watoto kwenye nyumba za kupanga jamani abaki tu hapo hapo
 
Maty,

Hiyo haina ubishi kuwa kwani huyu mama ana ushahidi wote kwamba mume ana watu wengine wa nje. Anasema aliwahi kusome sms kwenye simu ya mume akataka kufa kwa vitu alivyokutana navyo. Hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini pamoja na kuamua kuvumilia mwanamume anamfanya kama vile siyo binadamu?

babu kama ana wanawake wa nje mbona kazi yake inakuwa rahisi hapo, wanawake wa nje ni balaa wengine wako radhi hata wakaroge mradi amshikilie mumewe cha msingi yeye ni kukazana na maombi tu kwa sababu shetani kasimama katikati ya hiyo ndoa
 
Mimi nilidhani avae bukta na kuwa ngangari kama nyama yao ili kieleweke. Na hata mume akiamua kuendelea kufanya mambo yake nje lakini awe na nidhamu.
 
Hii ni story ya mwanamke mmoja ambaye nimekutana naye katika harakati za kupeana ushauri wa kutatua matatizo yanayotusibu katika mahusiano. Amekubali niiweke hapa ili kupata maoni ya wadau. Matatizo yake ni mengi sana ila kwa ufupi ni kama ifuatavyo:

1. Suala na unyumba katika ndoa yao yenye umri wa karibia miaka 4 wakiwa na watoto 2, limekumbwa na ukame wa ajabu. Wanashiriki tendo la ndoa kama mara 2 tu kwa mwezi na ni lazima mume atake. Mwanamke akiomba anaambiwa kuwa mume hawezi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara. Wakati wa uchumba wao na siku za awali za ndoa yao, walikuwa wakishiriki tendo la ndoa hata zaidi ya mara 2 kwa week na wote waliliridhika na kufurahia tendo hilo. Hali ilianza kubadilika baada ya kama miaka 2 hivi. Mbaya zaidi hata kama mmoja akirudi safari baada ya kukaa kwa muda mrefu kiasi cha week nzima au zaidi, bado hakuna uhakika wa tendo la ndoa!

2. Mawasiliano ndani ya nyumba hasa hasa yale ya kimahaba nalo limekuwa tatizo. Yaani ni kama vile wanaishi maktaba. Muda mwingi mume akiwa nyumbani anacheza na simu yake akituma na kupokea sms kutoka kwa watu tofauti. Pia mume akiwa nje na jamaa wengine anakuwa mchangamfu sana, akiongea na vicheko juu.
3. Vitu vingi vya mume vimefunigiwa katika mkoba (brief case) wenye password ambayo mke hajui. Pia mume anazo account za benki ambazo mke wake hazijui kabisa. Na simu za mume zimewekewa password ingawa vitu vyote vya mke ikiwemo simu, account za bank n.k viko wazi na mume anavivinjari wakati wowote anaopenda.

4. Ni nadra kwa mume kukubali na kusifia (to appreciate) kitu alichokifanya mke. Na mara nyingi anamkatisha tamaa katika mipango yake anayomshirikisha.

Kutokana na haya matatizo na mengine mengi, huyo mama amekosa raha muda mrefu na aliwahi kufikiria kujidhuru (got closer to attempt suicide) ila kwa sasa ameamua kutafuta ushauri ama wa kuokoa ndoa au maisha yake. Amesali sana, amfeunga sana na kubadili makanisa kama nguo za mashidano ya mavazi lakini bado nazunguka pale pale. Kwa hiyo wadau nawaomba ushauri wenu ili niongeze kwenye package ya counseling ninayoendelea nayo kwa sasa.

Wasalaam, ....Babu DC
DC, ukweli kisa hiki kinasikitisha, pia hata kuogopesha kuingia kwenye ndoa. Huyu dada mpe pole zake pia mshauri, akiwa kama mwanamke anatakiwa kua na hekima na maarifa, na awe mtu wa kutunza siri, alichokosea huyo dada ni kuhama makanisa na kila anapoenda anawaeleza watumishi. Anatakiwa kujua hata watushi wa mungu ni binadam kama wengine na wanamadhaifu yao, na baadhi yao hawana siri, na hicho ndo kinamcheleweshea muujiza wake. Mungu wetu ni mwaminifu sana na kwakua ana ndoa na huyo kaka anatakiwa asimame kwa imani yake na mungu hua anasikiliza sana maombi ya mwanamke mwenye haki, kuna mistari kwa bible ya kusimamia. Ki ukweli ajue kuna mtu sehem kamshika huyo baba, chakufanya anatakiwa na yeye abadilike awe strong na yeye vitu vyake aweke pswd si kwa mashindano, akirudi home amkute mwenye furaha yuko busy na mambo yake kama haumoni vile, awe msafi avae vizuri abadilishe mavazi askae kimama mama, sio analia anasali mpaka anapauka, yeye avumilie tu na amwambie mungu wake nitavumilia mpaka mwisho ila mungu mfungue mume wangu. Ajaribu kuongea na mungu wake kama anaongea na mtu hapo karibu, amwambie mungu nataka uirudishe ndoa yangu kama kweli wewe mungu uliiamuru mifupa mikavu kuishi ukaipa pumzi na ikaishi na mimi nataka ndoa yangu iishi. Nashetani urudishe kila ulichokiiba kutoka kwangu na avitaje, ndoa yangu, kuaminiwa na mume wangu, kuheshimiwa na unyumba wangu rudisha shetani, then asimame na zaburi ya 2.8na9 amtenganishe mume na huyo anaemfunga. Amwambie mungu unaekataa kuachana na kufarakana sitaki kumuacha mume wangu, na umenipa kumiliki na kutawala, kuanzia leo mpaka mwisho nitammiliki mume wangu na kutawala kila kilicho chake, kwani hata ufalme wa mungu hupatikana kwanguvu walio dhaifu hawata uona. Amwambie mungu afanye, na amshushe kiburi mumewe kila jambo livurugike na atarudi. Ukweli sijaolewa bado ila nadhani ajaribu njia hii na atunze siri yake, aorodheshe anavohitaji na akomae kwenye nyumba yake, atafute pesa kidogo ampeleke dinner mumewe, akirudi amuombe unyumba yeye mwenyewe na akibubali asifanye makosa tena ampe style tofauti, inaruhusiwa kua malaya kwa mumeo fanya kama machangu poa tu mradi asivuke mipaka, anunue vizawadi vya hapa na pale ampe, hiyo pia ni moja ya maarifa ya kumrudisha. Ni hilo tu ila mungu hashindwi na jambo.
 
Mimi nilidhani avae bukta na kuwa ngangari kama nyama yao ili kieleweke. Na hata mume akiamua kuendelea kufanya mambo yake nje lakini awe na nidhamu.

babu mtu akishashikwa na shetani hata umvalie ovaroli haelewi kwani somtimes pale akili si yake sana sana utakuwa unapoteza muda wako tu na kufanya mambo yawe makubwa zaidi ya hayo. Huyo amkabidhi mungu tu alafu yeye akae pembeni na amlalamikie mungu kama kweli alimpa huyo mume atafanya yote mmama ayaombayo narudia tena awe na imani kama huna imani hata ulale unasali na kufunga kila siku maombi yako hayawezi kufanyiwa kazi aombe halafu aamini kwamba imekua hata kama haijawa na wala asianze kuwaza labda mume wangu atabadilika kesho yeye asubiri tu. Najua kwa akili ya kawaida ni ngumu tena ngumu sana ila akimshirikisha mungu ataweza tu kidogo kidogo then mambo yataenda sawa. Hebu ajaribu kufikiria kama yule mume angekua amekufa angefanyaje?
 
mwambie apime,kama kubaki kny hio ndoa ambayo iko half dead,kama kuna faida kuliko kuondoka...
kama atleast huyo mwanaume bado anawajali wanae i mean anatimiza wajibu wake kama baba then abaki for the sake of her children...
otherwise naona ni lack of communication between them ndio tatizo,hivi inakuwaje mpk mumeo anajifanyia mambo yake unashindwa hata kumuuliza???...mpaka mnaoana si mnakuwa mmezoeana vya kutosha kama best friends???..mwambie huyo dada avunje ukimya amuulize mumewe kwa nini anabehave anavyobehave....!
 
DC, ukweli kisa hiki kinasikitisha, pia hata kuogopesha kuingia kwenye ndoa. Huyu dada mpe pole zake pia mshauri, akiwa kama mwanamke anatakiwa kua na hekima na maarifa, na awe mtu wa kutunza siri, alichokosea huyo dada ni kuhama makanisa na kila anapoenda anawaeleza watumishi. Anatakiwa kujua hata watushi wa mungu ni binadam kama wengine na wanamadhaifu yao, na baadhi yao hawana siri, na hicho ndo kinamcheleweshea muujiza wake. Mungu wetu ni mwaminifu sana na kwakua ana ndoa na huyo kaka anatakiwa asimame kwa imani yake na mungu hua anasikiliza sana maombi ya mwanamke mwenye haki, kuna mistari kwa bible ya kusimamia. Ki ukweli ajue kuna mtu sehem kamshika huyo baba, chakufanya anatakiwa na yeye abadilike awe strong na yeye vitu vyake aweke pswd si kwa mashindano, akirudi home amkute mwenye furaha yuko busy na mambo yake kama haumoni vile, awe msafi avae vizuri abadilishe mavazi askae kimama mama, sio analia anasali mpaka anapauka, yeye avumilie tu na amwambie mungu wake nitavumilia mpaka mwisho ila mungu mfungue mume wangu. Ajaribu kuongea na mungu wake kama anaongea na mtu hapo karibu, amwambie mungu nataka uirudishe ndoa yangu kama kweli wewe mungu uliiamuru mifupa mikavu kuishi ukaipa pumzi na ikaishi na mimi nataka ndoa yangu iishi. Nashetani urudishe kila ulichokiiba kutoka kwangu na avitaje, ndoa yangu, kuaminiwa na mume wangu, kuheshimiwa na unyumba wangu rudisha shetani, then asimame na zaburi ya 2.8na9 amtenganishe mume na huyo anaemfunga. Amwambie mungu unaekataa kuachana na kufarakana sitaki kumuacha mume wangu, na umenipa kumiliki na kutawala, kuanzia leo mpaka mwisho nitammiliki mume wangu na kutawala kila kilicho chake, kwani hata ufalme wa mungu hupatikana kwanguvu walio dhaifu hawata uona. Amwambie mungu afanye, na amshushe kiburi mumewe kila jambo livurugike na atarudi. Ukweli sijaolewa bado ila nadhani ajaribu njia hii na atunze siri yake, aorodheshe anavohitaji na akomae kwenye nyumba yake, atafute pesa kidogo ampeleke dinner mumewe, akirudi amuombe unyumba yeye mwenyewe na akibubali asifanye makosa tena ampe style tofauti, inaruhusiwa kua malaya kwa mumeo fanya kama machangu poa tu mradi asivuke mipaka, anunue vizawadi vya hapa na pale ampe, hiyo pia ni moja ya maarifa ya kumrudisha. Ni hilo tu ila mungu hashindwi na jambo.

mamushka dia umemaliza kila kitu kaka DC mpelekee hii huyo dada na nakuambia ipo siku atakuja kutoa ushuhuda hapa yaani hata sina la kuongeza. MAMUSHKA WEWE NI NOMA
 
mwambie apime,kama kubaki kny hio ndoa ambayo iko half dead,kama kuna faida kuliko kuondoka...
kama atleast huyo mwanaume bado anawajali wanae i mean anatimiza wajibu wake kama baba then abaki for the sake of her children...
otherwise naona ni lack of communication between them ndio tatizo,hivi inakuwaje mpk mumeo anajifanyia mambo yake unashindwa hata kumuuliza???...mpaka mnaoana si mnakuwa mmezoeana vya kutosha kama best friends???..mwambie huyo dada avunje ukimya amuulize mumewe kwa nini anabehave anavyobehave....!

Nakubaliana na wewe na kaka dc ameshasema kashamuuliza anachojibu kula si unakula na mimi sijakufuza we tulia, jamani hz ndoa zioneni hivi hivi huyo kashikwa anapepea tu kwenye vikaratasi maporini anamuona mkewe kama mavi, mtu akishafikia hali hii hata ukimuuliza hawezi kukujibu la maana kwani hata akili inakua sio yake
 
swala la kumsifia mwenzi wako ni swala la mhimu sana katika mahusiano na ninakubaliana naye jinsi anavyoumia kwa kila anachofanya mwinziwe anaona kama ni kazi bure. Ila ni lazima kufikiria jw ni kwanini huyu jamaa abadilike kiasi hiki? lazima kuwe na source jamaa hawezi kubadilika tu bila sababu, anaweza akawaameona, amesikia au naye anaumia sana ila sababu hakuna mawasiliano kati yao basi ndio inakuwa kila mtu kivyake, nainavyojua mwanammw huwa anchukia na kumweleza mke wake hata kwa kumtukana ili tu amalize hasira zake, lakini unapoona jamaa amekasirika na hataki kuongea basi tambua kuwa lazima kuna jambo hapo wala sio dogo, na umegusia kuwa jamaa alimsumbukia sana wakati wa dating...
Ahsante sana Mkuu,

Mama anafanya kazi na yuko busy sana kwa hiyo hapotezi muda mwingi kanisani. Ila anasema anajitahidi mwisho wa week kuhakikisha anafanya kazi za home mwenyewe ikiwemo kupika n.k. Anachoshangaa ni kuwa kama kuna wageni wanaweza kusifia usafi wa nyumba, chakula n.k ila mume hata siku moja hawezi! Inamuuma sana huyo mama!
 
Kama itagundulika kuwa ndivyo,basi ni rahisi kdogo kuandaa approach ya kumkalisha na kumuuliza, tofauti na hivyo ataruka kiunzi na kukataa kbsa.
Huo ni upande mmoja wa baba, lkn labda mama nae ana matatizo yake ambayo hajasema?...

Kweli PJ,
kila hadithi ina pande mbili kabla ya kutoa hitimisho. Inawezekana kuna kitu huyo bi dada katenda ambacho kimemfanya mume kuwa na vita baridi. DC hebu dodosa tupate upande wa pili wa shilingi.
 
Kuna watu wako toxic kweli. Nimeona deletions kibao halafu ni postings za wale wale usual suspects...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom