*~Please**Mommy**Please~*

interesting views...
Je hii ni kuua?
Does it having feelings? it doesn't see, it can't survive on its own, etc. When does it become a human?...Hii ni debate itakayoendelea milele. I dont support it...but ndo arguments in favour hizo
Pia....je ni bora kukatisha maisha at this stage, au kuacha aje kuwa omba omba au kama yule kwenye ile video Uganga? [ame="http://www.youtube.com/watch?v=3v7ZQUzr0yo"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
interesting views...
Je hii ni kuua?
Does it having feelings? it doesn't see, it can't survive on its own, etc. When does it become a human?...Hii ni debate itakayoendelea milele. I dont support it...but ndo arguments in favour hizo
Pia....je ni bora kukatisha maisha at this stage, au kuacha aje kuwa omba omba au kama yule kwenye ile video Uganga?
Very sad kwa kweli, lakini ni vipi wewe ukiwa kama mzazi utajuwa kile kitakacho jiri kwenye maisha ya hicho kiumbe unacho taka kukitoa uhai?
 
Baby4.jpg

Baby0.jpg

Baby2.jpg

Baby1.jpg

Baby8.jpg

Baby9.jpg

Baby10.jpg

Baby11.jpg
 
Very sad kwa kweli, lakini ni vipi wewe ukiwa kama mzazi utajuwa kile kitakacho jiri kwenye maisha ya hicho kiumbe unacho taka kukitoa uhai?

Mkuu kama mzazi atajua kwamba hataki hicho kiumbe, na atajua hataweza kukipa upendo, basi bora akiepushe mabaya huko mbeleni. Solution ya hili ni kuweka clinic za kuondoa mimba mapema kabla haijafika mbali. Na zitakazofanya kazi katika mazingiza yaliyo-bora zaidi.
 
Na kwa nini mpaka unasubiri mimba hiingie ili uhichoropowe!?
Wewe wangekuchoropoa ungali kinda ukepata wapi hii nafasi ya kuja hapa na kutoa mawazo yako ya kikatili... mawazo ya kuuwa vichanga ambavyo havikukuomba kuwepo kwenye tumbo lako ambalo unaliona bora zaidi ya hivyo vichanga?
 
Oh no! This is so wrong....how can any human being with a heart and soul choose to do this?

1. Mtu anafanya arbotion kutokana na matatizo either ya kiafya-kashauriwa na Dr. au kuna mshutuko au ajali.
2. Kuna wanaotoa kwa vile it was unplanned/unwanted hao ndio thambi iko juu yao-wauwaji na sio wanawake pekee na waliowapa hizo mimba pia/wanaume. kwasababu mashauri mengi yakutoa mimba yanashirikisha wanaume na hata wengine ndio kwanza wanashauri na kutoa fedha za kutekeleza.
3.Sio kweli fetus/zygot inapata maumivu in arbotion process kwani ubongo wa kichanga tumboni hau function kiasi cha kuweza kuhisi maumivu. The fact remains ni zambi kubwa sana wandamu tunatenda.
 
the world is getting sicker.evil lurks among us, to use any reason whatsoever to try to justify such horrific acts shows us just how rotten our modern westernised society actually is.so how westernised are you, ndugu zangu.
 
Watoto kwanini watembelee JF bwana. Kama wazazi wao wanaona JF hapafai basi wasiwa ruhusu watoto wao kuingia. Sasa wanaona hizi picha ni graphic je watoto wakisign up halafu wakaanza kuchungulia kwenye jukwaa la wakubwa? Hao wazazi ndiyo wanabidi wacontrol watoto wao. Kama wanaona JF kuna pich hazifai wawaambie madogo waende website za cartoon network na Disney channel.

ni afadhali kama hao watoto wakiona huu upuuzi who knows may be it will make think twice kabla ya kukumbatia magazeti ya picha za ngono wanayopeana shuleni au kabla ya kupractice hizo ngono na binti wa jirani... some people are doing it because of ignorance, they grow up hearing things like,” it is not a baby is just a buch of cells” au “ ni manyama nyama tu”
 
Our lives begin to end the day we become silent about things that matter!Martin King Luther Jr.
 
interesting views...
Je hii ni kuua?
Does it having feelings? it doesn't see, it can't survive on its own, etc. When does it become a human?...Hii ni debate itakayoendelea milele. I dont support it...but ndo arguments in favour hizo
Pia....je ni bora kukatisha maisha at this stage, au kuacha aje kuwa omba omba au kama yule kwenye ile video Uganga? YouTube - Broadcast Yourself.

How can someone forecast someone else’s future so precisely to the point of killing him/her?

Watoto wangapi waliozaliwa kwenye maisha ya kawaida lakini wanaishi miserable life? Je na wale waliozaliwa kwenye maisha ya kimaskini lakini wanaishi maisha ya kawaida?

Mwanamke anapojihisi anamimba mtoto huwa tayari ana wiki kama mbili hivi, abortions nyingi ktk nchi zilizoendelea hufanywa kati ya wiki 8 hadi 10, check out by yourself how well the fetus is developed at this stage, kwa kifupi mtoto tayari ana moyo wenye mapigo, mfumo wa fahamu unaofanya kazi, uso, mikono, miguu etc na ana umbo la binadamu ktk nchi zetu hizi inachukia muda mrefu zaidi kwa mama kuwa na uhakika ana mimba, kufanya uamuzi wa kuitoa na kupata njia za kuitoa

besides, someone not being able to see, feel or take care of himself can not justify his murder...Je kwa sababu moja au nyingine mtu akimchukua mtoto wake ambaye haoni, hasikii maumivu wala hawezi kujihudumia akamuua atakuwa ametenda sawa? Watu wana guts za kufanya huu unyama si kwa sababu mtoto tumboni haoni ila kwa sababu wenyewe hawamuoni huyo mtoto, kama huyu mtoto angewekwa hapo mezani mtu akaambiwa “haya huyo hapo ua!” angemuua?
 
Na kwa nini mpaka unasubiri mimba hiingie ili uhichoropowe!?Wewe wangekuchoropoa ungali kinda ukepata wapi hii nafasi ya kuja hapa na kutoa mawazo yako ya kikatili... mawazo ya kuuwa vichanga ambavyo havikukuomba kuwepo kwenye tumbo lako ambalo unaliona bora zaidi ya hivyo vichanga?

Well said…

it is pathetic…

watu wanajiona wame mature kiasi cha kufanya ngono, lakini sio kiasi cha kuwa wazazi,…ukweli ni kwamba if you are not ready/mature enough to have a baby with this man/woman then you are not ready/mature enough to have sex with him/her vinginevyo ndio sababu kubwa ya hii chinja chinja inayoendelea hapa duniani

Na kila mtu anapaswa kujua kwamba hakuna contraceptive ambayo ni 100% effective
 
Na kwa nini mpaka unasubiri mimba hiingie ili uhichoropowe!?
Wewe wangekuchoropoa ungali kinda ukepata wapi hii nafasi ya kuja hapa na kutoa mawazo yako ya kikatili... mawazo ya kuuwa vichanga ambavyo havikukuomba kuwepo kwenye tumbo lako ambalo unaliona bora zaidi ya hivyo vichanga?

How can someone forecast someone else’s future so precisely to the point of killing him/her?

Watoto wangapi waliozaliwa kwenye maisha ya kawaida lakini wanaishi miserable life? Je na wale waliozaliwa kwenye maisha ya kimaskini lakini wanaishi maisha ya kawaida?

Mwanamke anapojihisi anamimba mtoto huwa tayari ana wiki kama mbili hivi, abortions nyingi ktk nchi zilizoendelea hufanywa kati ya wiki 8 hadi 10, check out by yourself how well the fetus is developed at this stage, kwa kifupi mtoto tayari ana moyo wenye mapigo, mfumo wa fahamu unaofanya kazi, uso, mikono, miguu etc na ana umbo la binadamu ktk nchi zetu hizi inachukia muda mrefu zaidi kwa mama kuwa na uhakika ana mimba, kufanya uamuzi wa kuitoa na kupata njia za kuitoa

besides, someone not being able to see, feel or take care of himself can not justify his murder...Je kwa sababu moja au nyingine mtu akimchukua mtoto wake ambaye haoni, hasikii maumivu wala hawezi kujihudumia akamuua atakuwa ametenda sawa? Watu wana guts za kufanya huu unyama si kwa sababu mtoto tumboni haoni ila kwa sababu wenyewe hawamuoni huyo mtoto, kama huyu mtoto angewekwa hapo mezani mtu akaambiwa “haya huyo hapo ua!” angemuua?

Okay, lets not let emotions run high on this! Mmeweka picha zenye kusudi la ku-arouse emotions kwa watu. Lakini hii ni discussion, and it's a highly contreversial issue. Na mimi nimeamua kuchukua upande tofauti na wewe, so don't hate me! Pili, ningependa kubadilisha mwelekeo wa argument yangu ya kwanza, maana ilikuwa weak kidogo.
Kwenye sheria topic hii inaingia katika ishu ya murder. Katika element za ku-prove murder, kwanza kabisa aliye-uawa ni lazima awe mwanadamu. Sasa kama hichi kiumbe ulichoua hakitaweza ku-meet hii requirement ya kwanza, basi abortion si uuaji. Nadhani mmenielewa. Na kama mtasema iwekwe sheria mpya ya kukataza hichi kitendo, je italeta picha gani kwa hivi viumbe? Si itamaanisha kuwa hichi kiumbe si binadamu, na hivyo kuangusha argument yenu yote ya kukipa usawa kama mwanadamu. Sijui mmenielewa?
Kwa sasa ningependa ku-discuss kama hichi kiumbe ni mwanadamu.

Mimi sidhani. Na sababu ninayotoa ni kuwa hakina basic human elements. Hizi ni vitu kama uwezo wa kupumua, kutoa uchafu, kuwa na feelings, nk. Hapa debate ita-move kuwa more scientific, lakini ndo hali halisi nionavyo mimi.
Nadhani kungewekwa sheria ya kukigeuza hichi kiumbe kuwa mwanadamu baada ya stage fulani ya mimba, ambapo kitaweza kuishi 'chenyewe' (kwa support za mashine - NICU).
 
Okay, lets not let emotions run high on this! Mmeweka picha zenye kusudi la ku-arouse emotions kwa watu...
Hizo picha ndio ukweli halisi wa kile kinacho fanyika.
Lakini hii ni discussion, and it's a highly contreversial issue. Na mimi nimeamua kuchukua upande tofauti na wewe, so don't hate me! Pili, ningependa kubadilisha mwelekeo wa argument yangu ya kwanza, maana ilikuwa weak kidogo.
Sitakuchukia mkuu na wewe ukiahidi kufanya hivyo. Vile vile juwa kwamba upo huru kabisa kubadilisha msimamo wako.
Kwenye sheria topic hii inaingia katika ishu ya murder. Katika element za ku-prove murder, kwanza kabisa aliye-uawa ni lazima awe mwanadamu. Sasa kama hichi kiumbe ulichoua hakitaweza ku-meet hii requirement ya kwanza, basi abortion si uuaji. Nadhani mmenielewa. Na kama mtasema iwekwe sheria mpya ya kukataza hichi kitendo, je italeta picha gani kwa hivi viumbe? Si itamaanisha kuwa hichi kiumbe si binadamu, na hivyo kuangusha argument yenu yote ya kukipa usawa kama mwanadamu. Sijui mmenielewa? Kwa sasa ningependa ku-discuss kama hichi kiumbe ni mwanadamu.
Hivyo vitoto vinavyo nyofyolewa matumboni mwa mama zao ni binadamu, kama mimi na wewe. Tatizo ni kuwa havina uwezo wa kujitetea.

Mimi sidhani. Na sababu ninayotoa ni kuwa hakina basic human elements. Hizi ni vitu kama uwezo wa kupumua, kutoa uchafu, kuwa na feelings, nk. Hapa debate ita-move kuwa more scientific, lakini ndo hali halisi nionavyo mimi.
Nadhani kungewekwa sheria ya kukigeuza hichi kiumbe kuwa mwanadamu baada ya stage fulani ya mimba, ambapo kitaweza kuishi 'chenyewe' (kwa support za mashine - NICU).
Ndugu yangu, dah! Yaani nashindwa hata namna ya kukujibu hapa...! Mmmh!
Hayo mamtatizo au hali ya uwezo wa kushindwa kupumua, kutoa uchafu na feelings, bado hazi-halalishi uhuwaji wa vichanga... Hali kama hizo ulizo ziorozesha hapo juu zinaweza kumkuta binadamu wa umri wowote aliye hai na haipelekei madaktari au ndugu wahusika kuamua kuwaangamiza wale wenye matatizo kama hayo.

Vipi ndugu zetu walio pata matatizo ya ugonjwa wa kupooza (kiharusi - paralysed) Tuwauwe wote kwa kuwa wamepoteza uwezo wa kujitegemea?

Prenatal development
Prenatal development is divided into two primary biological stages. The first is the embryonic stage, which lasts for about two months. At this point, the fetal stage begins. At the beginning of the fetal stage, the risk of miscarriage decreases sharply,[27] all major structures including hands, feet, head, brain, and other organs are present, and they continue to grow and develop. When the fetal stage commences, a fetus is typically about 30 mm (1.2 inches) in length, and the heart can be seen beating via sonograph; the fetus bends the head, and also makes general movements and startles that involve the whole body.[28] Some fingerprint formation occurs from the beginning of the fetal stage.[29]

Electrical brain activity is first detected between the 5th and 6th week of gestation, though this is still considered primitive neural activity rather than the beginning of conscious thought, something that develops much later in fetation. Synapses begin forming at 17 weeks, and at about week 28 begin multiply at a rapid pace which continues until 3–4 months after birth. It isn't until week 23 that the fetus can survive, albeit with major medical support, outside of the womb. It is not until then that the fetus possesses a sustainable human brain. [30]
 
Okay, lets not let emotions run high on this! Mmeweka picha zenye kusudi la ku-arouse emotions kwa watu. Lakini hii ni discussion, and it's a highly contreversial issue. Na mimi nimeamua kuchukua upande tofauti na wewe, so don't hate me! Pili, ningependa kubadilisha mwelekeo wa argument yangu ya kwanza, maana ilikuwa weak kidogo.
Kwenye sheria topic hii inaingia katika ishu ya murder. Katika element za ku-prove murder, kwanza kabisa aliye-uawa ni lazima awe mwanadamu. Sasa kama hichi kiumbe ulichoua hakitaweza ku-meet hii requirement ya kwanza, basi abortion si uuaji. Nadhani mmenielewa. Na kama mtasema iwekwe sheria mpya ya kukataza hichi kitendo, je italeta picha gani kwa hivi viumbe? Si itamaanisha kuwa hichi kiumbe si binadamu, na hivyo kuangusha argument yenu yote ya kukipa usawa kama mwanadamu. Sijui mmenielewa?
Kwa sasa ningependa ku-discuss kama hichi kiumbe ni mwanadamu.

Mimi sidhani. Na sababu ninayotoa ni kuwa hakina basic human elements. Hizi ni vitu kama uwezo wa kupumua, kutoa uchafu, kuwa na feelings, nk. Hapa debate ita-move kuwa more scientific, lakini ndo hali halisi nionavyo mimi.
Nadhani kungewekwa sheria ya kukigeuza hichi kiumbe kuwa mwanadamu baada ya stage fulani ya mimba, ambapo kitaweza kuishi 'chenyewe' (kwa support za mashine - NICU).

I don't hate you mtoto, you can stand on whatever you choose and ofcourse you are free to give your ideas humu

Hatuwezi kusema embryo/fetus anageuka kuwa binadamu anapoweza ku survive kwenye incubators, NICU etc, incubators zilivumbuliwa miaka ya 1800 na tangu technology hii iwe invented imekuwa ikiongezwa ubora ili ku support watoto wachanga premature wenye umri mdogo zaidi na zaidi na bado teknologia hii inaendelea kuongezwa ubora wake, sasa karne hii umri wa mtoto premature kuweza kuishi baada ya kuzaliwa unategemea sana na kukua kwa technologia na postnal care

Labda tuongelee kuhusu human biological development ambayo ni process in which human being grow to maturity, biologically, this covers human growth from a human zygote to a human adult,

Human being starts life as prenatal (zygote then embryo then fetus), after he is born he is called a child, then the same human becomes an adolescent etc

For that reason, human becomes human as soon as there is life in him (as soon as fertilization takes place) being small, not able to survive out of uterus, being premature etc does not make him less human,
 
Mkuu umenena... No comments...!
 
...Iwapo mwanamke amebakwa (na majambazi/mwendawazimu/etc) akapata ujauzito, ni halali kuitoa hiyo mimba au?

Mnamfikiriaje mwanamke wa namna hiyo? Fikiria ni mtu unayemjua anakuomba ushauri.
 
interesting views...
Je hii ni kuua?
Does it having feelings? it doesn't see, it can't survive on its own, etc. When does it become a human?...Hii ni debate itakayoendelea milele. I dont support it...but ndo arguments in favour hizo
Pia....je ni bora kukatisha maisha at this stage, au kuacha aje kuwa omba omba au kama yule kwenye ile video Uganga? YouTube - Broadcast Yourself.

hiyo video imenisikitisha kuliko hata hizo picha

watu hawatoi mimba kwa kupenda, na sio tu kwa ajili baba mtoto ameikataa mimba, sababu nyingi za kutoa mimba ni uwezo

ni vigumu kutaka kuwa na familia wakati uko masomoni huna income yoyote
 
Lakini kumbuka pia kwamba watu masikini ki kweli kweli sio wengi wanaotoa mimba, kwa sababu hawawezi kulipia abortion,

akili ni kufikiria hayo yoote ya uwezo, umasikini, masomo nk kabla ya kujamiiana na mtu

Mie naona pia watu hajui nini hasa maana ya kutoa mimba na madhara yake, kwa hiyo wanaichukulia kama easy way out, but it is not..kwa hiyo inabidi waelimishwe
 
...Iwapo mwanamke amebakwa (na majambazi/mwendawazimu/etc) akapata ujauzito, ni halali kuitoa hiyo mimba au?
Si halal hata kidogo...

Hakika ni kuwa siku hizi imekuwa ni biashara kwa madaktari hasa katika nchi zetu za Afrika na nyinginezo kuwatishia wagonjwa ili wapate biashara au kufanya upasuaji ili wapate pato kubwa zaidi.

Uislamu umeweka mikakati yake katika kila jambo. Ikiwa mzazi ataambiwa na daktari mtaalamu na aliyebobea katika suala la magonjwa kwa mzazi na mtoto bila kuwepo ushawishi wa aina yoyote ile itafaa kwa mzazi kukubali kutolewa mimba ili aokolewe mama.

Hata hivyo, wazazi wanatakiwa waende kwa daktari wataalamu katika fani hiyo na ikiwa kutakuwepo na daktari mcha Mungu muadilifu itabidi muende kwake, ili kupata ushauri juu ya afya ya mama mjamzito.

Daktari ndiye atakaye mshauri juu ya afya yake na kama kuna dharura itakayo sababisha utowaji wa mimba. Utowaji wa mimba hiyo itazingatiwa tu kuwa kuna uwezekana wa mama kufariki kwa kuwa na kiumbe hicho, au kuendelea kwake kuwa na mimba hiyo kutamletea mauti.

Na isitoshe kukubalika huko, bali kumetakiwa uthibitisho huo utolewe na daktari mwenye kuaminika kabisa. Na muhimu kwanza atafutwe daktari muadilifu mwenye kuaminika...

Ama kuitoa mimba tu kwa sababu ya kutotaka mtoto, au kukhofia riziki yake, au malezi yake, au kuchelea gharama za maisha kama kumsomesha, kumvisha, au kumlisha n.k. hayo yote hayaruhusiwi kisheria.

Mnamfikiriaje mwanamke wa namna hiyo? Fikiria ni mtu unayemjua anakuomba ushauri.
Inajulikana kuwa hicho kilichopo tumboni hakihusiki kwa njia moja au nyingine na jarima ile ya kubakwa mwanamke huyo, na maadam haikuwa ridhaa ya mwanamke kufanywa hivyo na alijitahidi kupambana na mbakaji/wabakaji akazidiwa, ni wajibu wake kukihifadhi hicho kiumbe na M'Mungu Atakilinda na kukijaalia kuwa ni chema na poza kwa mama yake.

Na ikiwa mwanamke huyo hajaolewa, basi ni jambo jema kwa wanaume wenye imani kumsitiri na kumsaidia kumtoa katika mitihani hiyo iliyomkumba. Ama kama ana mume, basi mume wake ajitahidi japo ni vigumu sana, kusubiri na kukikubali kiumbe hicho ambacho hakina hatia yoyote ile. Na malipo makubwa yanawasubiri watu aina hiyo.
 
Last edited:
hiyo video imenisikitisha kuliko hata hizo picha

watu hawatoi mimba kwa kupenda, na sio tu kwa ajili baba mtoto ameikataa mimba, sababu nyingi za kutoa mimba ni uwezo

ni vigumu kutaka kuwa na familia wakati uko masomoni huna income yoyote

Mara nyingi sisi hufanya makosa yaliyo makubwa mbele ya M'Mungu nasi tukawa ni wenye kusema bahati mbaya au Iblisi ndiye aliyekushawishi. Kudhania hivyo haitusaidii chochote bali linatupatia sisi muhula na nafasi ya kufanya mengine na kisha kutoa hoja hizo hizo.

Haiwezekani ukawa umefanya tendo kama la zinaa kisha useme sikukusudia kwani kitendo hicho kinajumlisha mambo mengi sana. Mwanzo mnaanza kutongozana, mzungumze, mpeane miadi na mfanye kitendo chenyewe ambacho ni kibaya sana. Tunashauriwa na kuimizwa sana kuwa na subira katika mambo yetu yote. Kwanini tuendeleze tamaa zetu za mwili za dakika chache, na majuto yake yawe nawe daima katika maisha yako yote!?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom