Please Gov abolish public drinking.

Bra-joe

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,562
986
Kama serikali haitapiga marufuku unjwaji wa pombe hadharani, Tanzania itakuwa ktk hatari ya kuwa na raia walevi kupindukia kama Urusi au Australia. Sasa hivi vijana wengi wakishika fedha kidogo tu, wanajiingiza ktk ulevi, wengi kwa kufuata mkumbo tu, hii ni kwa sababu wakati wanakua wanawaona kaka, wajomba na hata baba zao wakinywa pombe hadharani, pia pombe kwa sasa imekuwa chanzo kikubwa cha familia kutelekezwa au ndoa kuvunjika na matokeo yake kuongezeka kwa watoto wa mitaani na umaskini. Tafadhali sana serikali pombe inywewe sehemu za ndani tu kama bar, night club, pub au hotel. Viongozi zingatieni sana hili jambo b4 it's 2 late.
 
Mwenzangu unakumbuka shuka kushakucha! hawawezekani tena hawa,wawate kama walivyo.
 
We badala ya kusema pombe iongezewe kodi then unataka ifutwe? Leo hela za walevi na wavuta sigara ndio mnazifaidi maana TBL, SBL na TCC ndo walipa kodi wakubwa wa kwanza, acha dhahabu na almasi mnazojisifia ni utajiri.

Kama unadhani urusi ni walevi mbona nyie msio walevi bado wanawaletea misaada hadi vyandarua na ko.nd.omu? Pesa inatafutwa popote bro, kama vipi mfungie mwanao asinywe bia sisi tunahitaji kodi zao tena ziongezeke maradufu tupate huduma za kijamii, wao walevi watajijua.
 
sijasema pombe ifutwe, nimesema inywewe ktk sehemu maalumu za ndani kama Pub au N'club, wala sijasema Urusi hawazalishi au ni maskini kwa sababu ya pombe, na wala sijasema pombe ni kikwazo cha uzalishaji Tanzania. Nimetahadhrisha tusipokuwa makini tutakuwa na jamii ya walevi. Hili ni tatizo la kijamii siyo siasa. Tatizo la wabongo wengi wanapoharibikiwa hutaka wote waharibikiwe.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom