Pius Ngeze: Mfupa uliomshinda fisi waonyesha dalili za kupata mlaji...

Al Dente

New Member
Oct 18, 2012
4
2
Taarifa toka kwenye vyanzo vyetu vya habari zinasema kuwa ule mfupa uliomshinda Fisi waonyesha dalili za kupata mlaji.

Taarifa hizo zinasema kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Uchumi na Mipango,amemwandikia Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania Bw Adolph Kumburu kutaka kupata PERSONAL PRESENTATION ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw Pius Ngeze.

Taarifa hizo pia zinasema aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Kahawa Bw Pius Ngeze ndie aliyeshindwa kuiongoza Bodi ya Kahawa na kusababisha makundi kwenye Bodi hiyo yaliyosababisha msuguano mkali baina ya Bodi ya wakurugenzi,Menejimenti na wafanyakazi kwa ujumla

Mzee huyo Bw Pius Ngeze ambaye ni rafiki wa karibu sana na Mkurugenzi Mkuu huyo wa Bodi ya Kahawa Bw Adolph Kumburu ambae aliweza kumwendesha M/Kiti huyo mpaka kufikia kuivuruga sekta hiyo ya Kahawa nchini na kusababisha Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mzee huyo Bw Pius Ngeze kuvunjwa na serikali kwa ubadirifu,uonevu na unyanyasawaji kwa wafanya kazi wa Bodi hiyo nyeti nchini.
 
we mwenyewe mdaku pia hujaeleza kwa kina nini hasa unawasilisha, jipange ueleze hoja yako kwa ufasaha, lakini kama huna taarifa huyo mama mwenyekiti wa bodi ya sasa ndio balaa zaidi, ana mgongano wa kimaslahi baina ya kampuni yao ya uwakili na kampuni za kahawa, mtaendelea kuliwa tu
 
  • Thanks
Reactions: SpK
Tatizo mnataka siasa kila mahali. Bodi ya kahawa inatakiwa iwe ya kitaalamu na haitakiwi kuendeshwa kisiasa kama ambavyo wengi wanataka. Adolph Kumuburu ni mtaaluma na alikuwa na mikakati sahihi na ya dhati ya kunusuru sekta ya kahawa ila vikwazo vya kisiasa vinamkwamisha.

Ushauri:
Tusipotenganisha siasa na utaalamu, hakika hatutapiga hatua katika sekta yoyote.
 
  • Thanks
Reactions: SpK
mimi nawashangaa ccm. Huyu mzee alikua Mbunge wa jimbo la Ngara hakunachochote cha maana alichofanya. Sasa kwanini mtu ambaye hata hafai kwao atawezaje kwingine?. Kubebana na Upendeleo ndo unarudisha nyuma hii nchi. mia
 
Zimamoto inaelekea wewe hujui chochote kuhusu alicho taka kukifanya huyu Kumburu kwenye bodi hiyo ndio maana unasema ni mtaaluma.Yeye Kumburu kutunga sheria zake toka kwenye kichwa chake bila kufuata kanuni na sheria zilizopo kwenye Kahawa ndio unamwita mtaaluma ? Hajui chochote zaidi ya yeye kutaka kuua bodi hiyo na huyo Ngeze wakati huo ni MAMLUKI WA WAZUNGU TU kutaka kuua bodi hiyo ili wazungu wajibebe kahawa kwa ulaini hana lolote lile wala uongozi hajui
 
Last edited by a moderator:
Kumbe bado mnatafunana kwenye hiyo bodi ,basi inaelekea huyo Mkurugenzi Mkuu ni tatizo. Ila inaelekea wale vilaza waliowekwa bench wakati Kumburu anaingia wanapambana kumwondoa .Kabla Kumburu hajaingia, bodi ilikuwa na vilaza kupita maelezo ,tena wailikuwa wanashiriki kwenye maamuzi makubwa ya sekta ya kahawa .
 
Kilaza aliyewekwa benchi ni yupi, je unajua uwezo wa kumburu na elimu yake ni kiwango gani. Ni vizuri ufuatilie utajua kumbe kilaza ni Kumburu mwenyewe kwani ameshindwa kabisa kuendesha Bodi na kukimbilia kuunda makundi ya kumlinda.
Historia yake inajionyesha kwani alikimbia Alminium Africa kwa kashfa, akaenda Mbinga Coffee Curing akufanya chochote zaidi ya kulumbana na Meneja mkuu bwana Kasongo akijipendekeza kwa mzungu expatriate ili achukue madaraka na hapo alipopshindwa ndipo akakimbilia Technoserve. Huko ili kulinda nafasi yake akawa kibaraka kwa kuwanyanyasa waafrika wenzake wakamzawadia nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa ili akalinde miradi yao.

Wao ndio walihusika na kampuni iliyoendesha interview. Kama wasingemsimamia leo hii hasingekuwa Mkurugenzi mkuu. Yeye kwa kulipa fadhila kwanza akaanzisha njama za kujizungusha wafanyakazi kutoka huko(Technoserve) ili asipate wa kumuhoji. Baada ya hapo anataka kuua vikundi vyote vya wakulima ili vibaki vya Kilicafe pamoja na kuingiza kanuni anazozitekeleza kiubaguzi kulinda vikundi hivyo.
Huyu jamaa ana kiburi ambacho watu wanajiuliza anakitoa wapi, we uliona wapi mfanyakazi anakataa kutii amri ya wakubwa zake na bado anaendelea kuwepo kazini. Hii haipo mahala popote duniani. Je vyombo vya serikali havioni.
 
Si hivyo tu mzee Ngeze ni mwadilifu sana kwani namfahamu vizuri yeye binafsi na utendaji wake wakati akiwa katika bodi za CRDB,POSTA,RAILWAY na mwenyekiti wa ccm Wa mkoapamoja na mbunge.
 
Kilaza aliyewekwa benchi ni yupi, je unajua uwezo wa kumburu na elimu yake ni kiwango gani. Ni vizuri ufuatilie utajua kumbe kilaza ni Kumburu mwenyewe kwani ameshindwa kabisa kuendesha Bodi na kukimbilia kuunda makundi ya kumlinda.
Historia yake inajionyesha kwani alikimbia Alminium Africa kwa kashfa, akaenda Mbinga Coffee Curing akufanya chochote zaidi ya kulumbana na Meneja mkuu bwana Kasongo akijipendekeza kwa mzungu expatriate ili achukue madaraka na hapo alipopshindwa ndipo akakimbilia Technoserve. Huko ili kulinda nafasi yake akawa kibaraka kwa kuwanyanyasa waafrika wenzake wakamzawadia nafasi ya kuwa Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa ili akalinde miradi yao.

Wao ndio walihusika na kampuni iliyoendesha interview. Kama wasingemsimamia leo hii hasingekuwa Mkurugenzi mkuu. Yeye kwa kulipa fadhila kwanza akaanzisha njama za kujizungusha wafanyakazi kutoka huko(Technoserve) ili asipate wa kumuhoji. Baada ya hapo anataka kuua vikundi vyote vya wakulima ili vibaki vya Kilicafe pamoja na kuingiza kanuni anazozitekeleza kiubaguzi kulinda vikundi hivyo.
Huyu jamaa ana kiburi ambacho watu wanajiuliza anakitoa wapi, we uliona wapi mfanyakazi anakataa kutii amri ya wakubwa zake na bado anaendelea kuwepo kazini. Hii haipo mahala popote duniani. Je vyombo vya serikali havioni.

Wewe kweli unaongea /andika nadharia zaidi .Mtaje aliyetoka na Kumburu Technoserve !Usimtaje Primus coz yeye alikuwa bodi akaondoka sababu ya hao vilaza waliokuwepo wakiendesha majungu. Ama una chuki binafsi ,inawezekana wewe unahoja za ajira msingi kuhusu utendaji mbovu wa Kumburu ila huna hoja zenye mashiko .Jipange upya coz hakuna asiyejua uchafu uliokuwa ukifanyika kwenye bodi ya kahawa kabla ya Kumburu .
1.Nani aliyeweka rehani Jengo la kahawa likataka kuuzwa na Exim Bank?
2.Nani alipoingia Mkataba wa kuwapangishia CRDB mlango mkuu wa kuingia makao makuu ya ofisi za bodi ya kahawa?
3.Nani aliyewakaimisha wakurugezi wasaidizi wasio na sifa zaidi ya miaka 7.Taratibu gani za ajira hizo?
4.Nani aliyekuwa akiwalipa mshahara mkubwa masekretari wenye secretarial certificate ungilinganisha na maafisa wenye Shahada ?

Kabla hujachangia hoja tafakari hayo maswali kisha uje na strong argument (critic ) ku support majungu yako dhidi ya Bodi ya kahawa hususani Mgt .

Narudia tena Inawezekana kweli Kumburu ana mapungufu mengi kiutendaji ila wewe umeshindwa kuyaweka wazi coz hujajipanga ,so acha majungu toa fact kama huna unatulia .
 
  • Thanks
Reactions: SpK
Bw Mwakalinga tumeona mchango wako kuhusiana na hii mada ila cha msingi ni kwamba tuongelee mambo ya maana hata wewe mwenyewe inaelekea hutoi mada yenye maana bali ni kupoteza uma kwenye mambo yasio na msingi .

Wote tunajua kuhusiana na jengo kuwekwa rehani kwenye benki ya EXIM pamoja na kuuza mlango mkuu wa jengo hilo kwa crdb ni makosa yaliyofanywa na uongozi uliopita uliokuwa ukiongozwa na Bw L.D.Omar na ni kweli alikuwa dhaifu.

Lakini kinachotakiwa kujulikana hapa ni kwamba yeye Kumburu toka alipoingia kwenye Bodi hiyo zaidi ya ugomvi tu kila mahali amefanya nini cha maana zaidi ya kujenga makundi ya watu ? na kutunga sheria zake kichwani za kufukuza wafanya kazi bila kufuata taratibu,kanuni na sheria za kazi.

Cha kujiuliza hapa ni kwamba ujeuri wa huyu Bw Kumburu anautoa wapi kiasi kwamba hataki kufuata maagizo anayopewa na Bodi ya Wakurugenzi wake mpaka anafikia kuwaambia watumishi flaniflani kuwa yeye kama Mwanaume hawezi kupangiwa kazi na mwanamke,na kauli hii ndio inayoonyesha kuwa Bw Kumburu kitendo cha kumdharau Mwenyekiti wake ambae ni mteule wa rais ni kwamba amemdharau hata Rais wa nchi Mh Dr Jakaya Kikwete kwamba uteuzi alioufanya wa kumteua Dr Sinare ambae ni Mwanamama ni makosa.Hivyo kufanya hata wale wanamama walioteuliwa na Raisi ni makosa

Kingine alichokifanya Bw Kumburu tangu aingie bodi hiyo ni kwamba alitaka kuwauwa wakulima wa mkonge nchini kwa kushirikiana na wazungu kuwa magunia ya kusafirisha kahawa yawe yanaagizwa toka nje ya nchi bila kujali viwanda vya ndani.Kwa kumtumia aliyekuwa mbunge wa Vunjo wakati huo Bw Aloyce Kimaro aliipeleka hoja hiyo bungeni baada ya kurudi nae kutoka China ili akaitete hoja hiyo na kwenye maswali ya hapo kwa hapo kwa Mh Waziri Mkuu swala hilo Pinda alilipiga chini na kugonga mwamba.

Hakuishia hapo Alishawahi kuuza kahawa za wakulima kwa bei poa akidai kuwa hakuna muda wa kuzunguka na kahawa za wakulima huku soko likiwa limeanguka na aliposhindwa na wakulima kukataa zisitoke zilirudishwe mnadani na zikapata bei ya juu zaidi wakati soko lilikuwa bado chini.

Hakuna asiyejua jinsi anavyowamaliza wakulima wa kahawa kwa mchezo wake wa kuwabadilishia dola wazipatazo kwenye minada na kuwalipa kwa sh za kitanzania kitu ambacho amekiita ni GAIN ON EXCHANGE na kwa nini asiwalipe wakulima hao tofauti hiyo badala yake anaziweka fedha hizo mfukoni.Kwa mfano kwa miaka miwili iliyopita aliweza kuwaibia mkulima zaidi ya sh, za kitz 1.2 bilion hatujajua mwaka huu ni kiasi gani kimeliwa.Pia ni kwa nini asiwashauri wakulima wawe na Ac za dola badala yake anawaficha, na je kwani huko mikoa ya kusini kama Mbinga na Mbeya benk zao hazifanyi transaction za dola ?.Na kwa nini asikatae kuuza kahawa za hao wakulima kama hawajafungua Ac za dola kama kweli ana nia nzuri na wakulima wa zao hilo nyeti? Cha kujiuliza hapa ni je Bodi ya Kahawa inafanya biashara juu ya mgongo wa mkulima?

Wote tunaelewa kuwa alipigania na kuhakikisha kuwa sheria ya kutokuhamisha kahawa mkoa mmoja kwenda mwingine hairuhusiwi ila akaweka kipengele kuwa mpaka upate kibali toka kwa kwa DG, na hasa kama mkoa husika una kiwanda cha kukobolea kahawa, lakini cha kushangaza wakulima na vikundi vinavyolima kahawa mkoani Kigoma wanabanwa na sheria hii na wanalazimishwa kukobolea kahawa zao kwenye kiwanda kilichopo Kalinzi na kiwanda hicho hakina ghala lenye kueleweka na hata hakijasajiliwa kwa ajili ya stakabadhi ghalani lakini cha kushangaza anawaachia wakulima na wanunuzi wa kahawa mkoani Arusha na Manyara kusafrisha kahawa zao mpaka Moshi kukobolewa wakati Mkoani Arusha kuna kiwanda cha kukoboa kahawa kiitwacho Arusha Coffee Mill.

List ya wafanyakazi waliotoka Technoserve na Kilicafe waliopo TCB tutaiweka hapa pamoja na huyo Primus ambaye tunasikia alishaacha kazi na kuja kuomba kazi upya akitokea huko huko Kilicafe na Mpishi wake wa chai aliyetoka nae hukohuko Technoserve na sasa kamleta dereva ambaye inasemekana alikuwa hukohuko technoserve .

Kiburi cha huyu bw hakijulikani vizuri anakitoa wapi ila ukiangalia vizuri na ratiba ya vikao vya bodi inaonyesha kuwa terehe 25/10 kuna kikao lakini cha kushangaza hajatoa au kujulisha wajumbe wa bodi pamoja na Mwenyekiti wake kuhusiana na kikao hicho isipokuwa yeye amepanga safari yake ya kwenda italy tarehe 23/10 kwa siku zisizopungua 5 na anaondoka na maafsa wawili kitendo kilichowashangaza wengi kwa kuwa kwenye Mkutano wa terehe 5/7 aliwaeleza wajumbe wa bodi kuwa shirika lina matatizo makubwa ya fedha na hata kufikia bodi kushindwa kuendesha shughuli zake sasa hizi za kwenda kutalii kazitoa wapi ambazo ni zaidi ya sh 20milioni? Na kwamba hata Mwenyekiti wa bodi hiyo inasemakana hana taarifa na safari hiyo.

Amejifungulia ofisi Mjini Dar kwenye jengo la posta mpya pamoja na kuwa Bodi hiyo ina ofisi bandarini.Ofisi hii inasemakana ilishatakiwa ifungwe na bodi ya wakurugenzi na ibaki moja tu ya bandarini lakini Bw Kumburu amekaidi na ameendelea na kuihudumia ofisi hiyo na hata kumwamisha secretary kutoka Moshi kwenda kukaa huko akiwa na kazi ya kuvuta vumbi mpaka bosi atakapokuja.

Hivyo hapa tunasema Personal Presentetion aliyopewa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Bw Kumburu kuhusiana na Mzee Pius Ngeze ni batili kwani bodi yake haikumaliza kazi kwa heshima kwa kuwa bodi hiyo ilivunjwa kutokana na utendaji usioridhisha.
 
Wewe kweli unaongea /andika nadharia zaidi .Mtaje aliyetoka na Kumburu Technoserve !Usimtaje Primus coz yeye alikuwa bodi akaondoka sababu ya hao vilaza waliokuwepo wakiendesha majungu. Ama una chuki binafsi ,inawezekana wewe unahoja za ajira msingi kuhusu utendaji mbovu wa Kumburu ila huna hoja zenye mashiko .Jipange upya coz hakuna asiyejua uchafu uliokuwa ukifanyika kwenye bodi ya kahawa kabla ya Kumburu .
1.Nani aliyeweka rehani Jengo la kahawa likataka kuuzwa na Exim Bank?
2.Nani alipoingia Mkataba wa kuwapangishia CRDB mlango mkuu wa kuingia makao makuu ya ofisi za bodi ya kahawa?
3.Nani aliyewakaimisha wakurugezi wasaidizi wasio na sifa zaidi ya miaka 7.Taratibu gani za ajira hizo?
4.Nani aliyekuwa akiwalipa mshahara mkubwa masekretari wenye secretarial certificate ungilinganisha na maafisa wenye Shahada ?

Kabla hujachangia hoja tafakari hayo maswali kisha uje na strong argument (critic ) ku support majungu yako dhidi ya Bodi ya kahawa hususani Mgt .

Narudia tena Inawezekana kweli Kumburu ana mapungufu mengi kiutendaji ila wewe umeshindwa kuyaweka wazi coz hujajipanga ,so acha majungu toa fact kama huna unatulia .

Nitakutajia majina ya wafanyakazi aliojizungusha kuwa ni:

1. Primus Kimaryo
Huyu ni Mkurugenzi wa Masoko. Alikuwa Bodi ya Kahawa akaacha kazi na kuamuajili Kilicafe. Kilicafe ni association iliyoanzishwa na Kumburu alipokuwa Technoserve, tena yeye mwenyewe aliwahi kuwa Meneja wa Kilicafe. Kumburu ndiye alikuwa na say ya Primus kuajiriwa Kilicafe na ndiye aliyehakikisha alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi anamrudisha Bodi ya kahawa. Kama si hivyo kwa nini basi Primus alikuwa ameacha kazi Bodi ya Kahawa na kwa muda mfupi akawa amerudi tena Bodi ya kahawa. Kama utakumbuka wakati wa Omari alishindwa kabisa kufanya kazi.
2. Kajiru Kisenge
Huyu naye alimtoa Technoserve na alikuwa yuko chini yake directly. Alimwingiza Bodi ya Kahawa akampa mshahara wa upendeleo tofauti na waliojairiwa naye akina Msoka na Mkondya. Hii ilisababisha wafanyakazi hao wakimbie Bodi kwa kuona wanabaguliwa. Tena Kumburu asivyokuwa na aibu akamzushia kesi mkurugenzi wa Maendeleo ya kahawa Bw. Sipira ili amtengenezee nafasi Kajiru aje ashike nafasi ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya Kahawa ili Idara hizi mbili muhimu zishikwe na watu wake toka Technoserve na kilicafe. Kwa vile alishakubaliana na Ngeze wamfukuze Sipira akaajiri mfanyakazi wa kuziba nafasi yake ya RCDO North Bw. Malulu( Cha ajabu Bw. Malulu ana taaluma ya Elimu huku amepewa majukumu ya kusimamia maendeleo ya kilimo, Kumburu huyu sijuhi walimtoa wapi). Nafasi moja ikawa na maofisa wawili.
3. Meneja wa Masoko - Tanga(Wanaofanya kazi Bodi ya kahawa wanajua jina lake)
Huyu naye alimtoa Technoserve ili amtumie kuendesha ofisi ya Tanga. Huyu ni binti wa kwao akina Ngeze hivyo aliua njiwa wawili kwa jiwe moja.
4. Meneja Masoko Dar
Huyu hakutoka Technoserve ila wana ushemeji
5. Muhudumu wake Georgita
Huyu naye alitoka naye Kilicafe alipokuwa akimuhudumia. Kuanatetesi ambazo hazijathibitishwa kuwa wana mahusiano ya ndani zaidi.

Kuhusu makosa yake ni kama ifutavyo:
1. Kuendesha Bodi kwa kutumia mfumo ambao haujaidhinishwa na serikali.
2. Kuvunja sheria ya kazi kwa kubagua wafanyakazi kimaslahi
3. Kupendelea baadhi ya wafanya biashara ambao ana maslahi nao kama vikundi vya Kilicafe.
4. Kukataa kutii maagizo ya wakubwa zake(Gross insurbordination) kama kukataa kumwamisha mgonjwa ili kunusuru maisha yake ambalo pia ni kosa la kukusudia kuua kwa makusudi.
5. Kuendesha shirika la umma kama mali yake bila ya kufuata kanuni na taratibu(mifano iko mingi)
Haya ni baadhi ya taarifa tulizopewa na wafanyakazi wenyewe na kuzihakiki, nadhani wakifuatwa wataeleza zaidi na kwa ufasaha zaidi
5. Sababu zingine na ushahidi zimeishandikwa na aliyechangia hapo juu. Vile vile kuna hata tume iliyokuwa imeundwa na wizara ya Kilimo ilibainisha makosa mengi ambayo ameyatenda.

Mimi naona kwa vile kumburu ni msahaulifu sana anafikiri hayo makosa yaliyoonekana kwenye tume na yote yaliyoandikwa huko nyuma kwa vile muda umepita yatakuwa yamesahaulika. Kumbukumbu za maandishi uwa hazifutiki, bado naamini kuna siku atawajibika.
 
Kama Menejimenti iliyopita ilikuwa na mapungufu ingawa hakukuwa na msuguano kama ilivyo kwenye menejimenti iliyopo hebu tueleze

1. Kuuza mlango mkuu wa kengo la kuingia kahawa house na kula hele za wakulima kupitia kwenye mnachokiita GAIN ON EXCHANGE ni kipi ndio balaa kabisa.?

2.Kulikuwa hakuna makundi ya watu wakati huo je kwa nini sasa kuna makundi ya watu

3.je Bw Kumburu amesomea wapi utawala au ndio wale wanaoitwa watu wa bahati na kwamba sheria zinatoka kichwani kwake na nani alimwambia kuwa uongozi ni sehemu ya kunyanyasa anao wasimamia?

4.Je ni sheria ipi anayotumia Bw Kumburu kukaidi maagizo ya wakubwa wake wa kazi.

5.je Kumburu anatumia kifungu kipi cha sheria za kazi kutangaza kuwa HAPANGIWI KAZI NA MWANAMKE ? Ndio maana anamdharau kiasi kikubwa hivyo.

Mshaurini aache kuwa kibaraka wa wazungu wanatamwacha njiani bila yeye kujua wazungu hawana urafiki wa kudumu ni urafiki wa muda tu. Ni Mzungu yupi ulimkuta akimnyanyasa mzungu mwenzake kama sisi waafrika sio wajinga wa kutupwa
 
Wadau!

Pamoja na ugeni wangu naona hapa kuna kufitiniana au kuna mgongano wa kimaslahi. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

Ilishawahi kuandikwa kwenye mwananchi kwamba Bodi ya kahawa asilimia kubwa ni vihiyo- form 4 kwenda chini.
 
Siyo kweli kwani hao waliotajwa walishajiendeleza katika taaluma zao, mathalani Idara ya Masoko hata kama walikuwa ni form IV si walishapelekwa nje wakapata ujuzi zaidi katika fani ya kuonja k.m Bw. Mboya. Bw. Mboya amekubuhu katika taaluma ya uonjaji na amehudhuria kozi nyingi na amewahi kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa mambo yalienda vizuri sana. Huyu Bwana ukilimganisha na kumburu kiutawala wana tofauti ambapo Mboya anamwacha Kumburu kama mwendo wa umbali kati ya Mbinga na Moshi kwa mguu. kwa kumuogopa Mboya akamnyanganya madaraka aliyopewa na Bodi ya wakurugenzi ya kuwa Chief Liquorer and Auctionear bila ya idhini ya Bodi ya Wakurugenzi iliyompa cheo hicho.

Kwenye Interview alishindana na mfanyakazi aliyemkuta Bw. Kiangi ambaye anao uzoefu wa miaka mingi na ana Masters tangia mwaka 1988 ( Kumburu mwanye Degre ya kwanza tu alimshinda kwa kukingiwa kifua na Technoserve). Kumburu alipoingia tu kwanza akamfanya Bw. Kiangi Estate Manage huku akijua kua Bodi ya kahawa haina estate za ku Manage aibu ilipomfika akamrudishia cheo chake cha Technical Manager lakini akacha kumshirikisha katika kukagua viwanda kama hapo mwanzo, hivyo ni kama amemuweka benchi.

Accounts alikuta kuna wafanyakazi wenye CPA wawili Bw. Kilian Massawe na Bw. Mwakyami. Kwa kuwaogopa akaaza na kumfukuza kazi Mkurugenzi wa fedha Bw. Kilian Masawe. Bw. Mwakyami mzoefu tena chief Internal Auditor akanza kumbagua hata kwenye vikao vya mejimenti anamwita kwa kutegemea ajenda ingawaje kwenye barua aliyoiandikia wizara alimjumuhisha kama mmojawapo wa wajumbe wa menejimenti.

Idara ya Maendeleo ya kahawa wote aliwakuta wa Degree ya kwanza kama yake Kumburu. Aliyekuwa anakaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Maendeleo ya kahawa Bw. Melkiard Massawe kwanza akamdemoralise kwa kumteremsha mshahara china hata ya wajiriwa wapya, kisha akamtupa Mara akakae benchi kwa vile kiwango cha kahawa kinachozalishwa huko ni kidogo sana kumpeleka mfanyakazi mwenye uzoefu kama huyu.

Aliyekuwa Meneja wa Kanda Bw.Rutachweka alimkuta ana Masters mbili. Huyu akampeleka Kigoma katika ofisi isiyokuwa na vitendea kazi na wala hakuna shughuli ya kufanya kwani uzalishaji ni mdogo sana na pia mnunuzi ni wa aina moja yaani ushirika na vikundi. sijuhi kama anapata kazi ya kufanya huko.

Hata hao aliowajiri alipoona ni wasomi zaidi yake na wana msimamo kama Bw. Sipira( ana Masters ya Utawala na degree ya kwanza ya Kilimo) kwa kumuogopa kuwa anasifa za hata kuwa DG kuliko yeye akamsimamisha kazi ili amfukuze. Kama si Bodi ya wakurugenzi kuingilia angemfukuza. Wataalam wengine aliowaajiri akina Mapunda , Msoka, Mkondya( wote wkiwa na Degree za kwanza) aliwajengea mazingira ya kuwabagua au kwaruka katika maamuzi wakakimbia. Kwa vile analazimika kuajiri wasomi ndipo akawa anakazania kuajiri toka Technoserve au maofisa wenye taaluma tofauti kama ya ualimu.

Kama kweli ni mgeni ebu angalia katika muda wa miaka minne Kumburu aliyokaa Bodi alivyoisambaratisha Bodi ya kahawa. Bodi ikawa haifuati tena taratibu zilizowekwa zaidi ya kila siku kubuni mapya. Bodi ya Kahawa sio tena shirika la umma bali mali ya Kumburu inayoendeshwa kwa utashi wake. Wataalam amewatawanya na huku yeye mwenyewe hajui, amebaki kuendesha Bodi kwa kubahatisha.
 
Nakumbuka vita hii iliwahi kupelekwa bungeni na mbunge wa Mbozi ambae sasa ni mwenyekiti wa ccm wa mkoa wa Mbeya ;akilalamika jinsi hii bodi ya kahawa ilivyokuwa imeundwa na aliyekuwa waziri wa kilimo Maghembe!! Inaelekea suluhu bado haijapatikana ya matatizo aliyoanisha mbunge na kama kawaida mkweree anaona ni kama upepo unapita Tu!!
 
:A S 109:Mbunge wa Mbozi alikuwa ameandaliwa na Kumburu ili amsemee. Tulijua na ni yeye pia ndiye aliyemwandikia barua aliyopeleka kwa waziri, kwani hatujui? Mambo ya Bodi ya Kahawa Zambi angejuaje? Alikatiwa jamani.
 
Nakumbuka vita hii iliwahi kupelekwa bungeni na mbunge wa Mbozi ambae sasa ni mwenyekiti wa ccm wa mkoa wa Mbeya ;akilalamika jinsi hii bodi ya kahawa ilivyokuwa imeundwa na aliyekuwa waziri wa kilimo Maghembe!! Inaelekea suluhu bado haijapatikana ya matatizo aliyoanisha mbunge na kama kawaida mkweree anaona ni kama upepo unapita Tu!!

****** haya mambo yake ya kupuuzia kila kitu kwa kudhania ni upepo, utapita kuna wakati kitakuja KIMBUNGA...Sijui nacho atakipuuzia au vipi?
 
Tatizo mnataka siasa kila mahali. Bodi ya kahawa inatakiwa iwe ya kitaalamu na haitakiwi kuendeshwa kisiasa kama ambavyo wengi wanataka. Adolph Kumuburu ni mtaaluma na alikuwa na mikakati sahihi na ya dhati ya kunusuru sekta ya kahawa ila vikwazo vya kisiasa vinamkwamisha.

Ushauri:
Tusipotenganisha siasa na utaalamu, hakika hatutapiga hatua katika sekta yoyote.

Umenena vema,Watanzania tuache Majungu,chuki na fitna badala yake tufanye kazi kuliko kulalamika tu-by Oremus
 
  • Thanks
Reactions: SpK
Back
Top Bottom