Pius Msekwa kushtakiwa? Au ndiyo mnene?

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
Katika Hali isiyo ya kawaida Makamu Mwenyekiti na CCM na Spika mstaafu Mh.Pius Msekwa amechafuka ndani ya Bunge kama mwenyekiti wa Bodi ya Ngorongoro kujitwalia mamlaka ya kutoa maeneo ya kujenga mahotel ndani ya hifadhi ikiwa ni kinyume na sheria na mamlaka iliyotolewa kutokuruhusu tena uwekezaji ndani ya Hifadhi..Kambi ya Upinzani na CCM wote wamelisema na sijui nini kitakachotokea baada ya Hilo..Atakayesikia lolote basi tuambizane jamvini.
 
hii hoja itakufa haraka sana, subiri bahasha zikianza kutembezwa,
wabunge wanatufanya sisi wananchi kama ATM yao kila wanapoishiwa
wanawatishia watawala nyau wakitulizwa wanatulia kwani ni bajeti ngapi zilipashwa
zisipte lakini zimepita !!!!!!!!
 
Lazima achukuliwe hatua kali, serikali ya Kikwete hailei rushwa hata kidogo.
 
Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza ni kwa nini huyu mzee mzima anajihusisha na siasa uchwara mpaka sasa? Wazee wenzie wamekaa pembeni kama wakina Dr Salim Ahmed Salim, Warioba, Joseph Butiku n.k. inawezekana ni huu ufisadi ndio unamuweka! Such a shame!
 
Yaani mashirika ya Umma kama ngorongoro yanapata pesa nyingi lakini yameshindwa kuchangia maendeleo ya nchi hii kutokana na mfumo wa baadhi ya wana siasa na watumishi kufanya kama haya mashika ni yao binafsi.

Yaani hata ukimwangalia muhifadhi amewekwa mtu ambaye sio muhifadhi ili aweze kuendeleza ufisadi kwa wajuu bila maswali
 
Lazima achukuliwe hatua kali, serikali ya Kikwete hailei rushwa hata kidogo.
<br />
<br />
ukistaajabu ya Musa utayaona ya firani,na kila shetani na mbuyu wake,serikali hata iliyooza haikosi wafuasi,lakini hii ndio maana ya maisha wote tukiwaza kitu kimoja hatutafika ni vizuri kila m2 akiwaza kivyake kama hapa wakati mimi siiamini tena serikali ndugu yangu ana imani,haya mie macho 2,
 
Huyu Mzee nafikiri anamatatizo, na anafikiri bado Watanzania tunadai Uhuru. Wakati wa kipindi chake cha mwisho kama Spika wa Bunge, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom. Nadhani hapo utaelewa jinsi alivyo kwani vodacom inaeleweka ni ya akina nani.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hakuna kitu, wabunge wa ccm wapo wapo tu, kama kawaida yao, wabunge wa ccm watalalamaa weeeeeeeeeeee na kujifanya wazalendo na wengine kutoa viapo na kauli za kupendezesha watizamaji wa bunge lakini mwisho kama kawaida yao wanaunga mkono hoja na hoja inapita,
mimi sioni kama kuna haja ya bunge tena, ccm wamekuwa wanatumia wingi wao vibaya.
Yaani wabunge wa ccm ni hopeless, hawana uzalendo ni ipo ipo tu na mitumbo yako mikubwa
 
Hivi kwa nini wenyeviti na bodi za taasisi za Tanzania zina nguvu kubwa uliko watendaji.

Nijuavyomm kitu kinachoitwa bodi hakijishughulishi na utendaji.

Bodi kazi yake ni kupitisha au kukataa maamuzi ya UWEKEZAJI na tena yale strategic sasa kama bodi inahusika na kujua fulani apewe kitalu fulani mhhhh
 
Nakuambia bila kufukuza mafisadi kwa maandamano kama ilivyofanyika ufaransa enzi hizo, HATUTAPIGA HATUA YA MAENDELEO KAMWE!,
 
Back
Top Bottom