Pingamizi la Dr Slaa dhidi ya Rose Kamili lakataliwa mahakamani

Mkuu kamfungulia Rose Kamili anadai fidia ya milioni 50 ya kutelekeza watoto.

Dr. Slaa amewatelekeza watoto kwa muda gani? Kama ni muda mrefu kwa nini muda wote hakuleta madai hayo mpaka siku anataka kufunga ndoa na Mshumbuzi? Kama jambo hilo ni la kwali alitakiwa muda mrefu tu kumdai Dr. Slaa Child support, kwa sasa kuna kitu nyuma ya pazia, na huenda wataishia mitini kama ilivyotokea kwa yule waliyemleta kama mume wa Mshumbuzi na hatujui kesi imeishia wapo na yule jamaa na barakashia yake ameishia wapi.
 
Hata hii post umeweka kama kejeli wakati ni habari ya kawaida sana, na umekuja na ki-comment ati tunamuombea mamayetu Rose Kamali ashinde. Kwanini usiseme tunamuombea Dr Slaa na Josephine washinde? Acha porojo za std one wewe mtu.

Kejeli vipi kwa hiyo wewe utaki Rose Kamili apate haki yake?
 
Binafsi sioni kama kuna ukweli kwamba Dr. Slaa hakuwatunza watoto wake. Kama ingetokea hivyo kwa vyo vyote huyu mama Rose angemfungulia madai Dr. Slaa kudai child suppoort, hakufanya hivyo. Laeo amekuja kuchomekea hicho kitu baada ya kuona Josephine going to be expected first lady.

Imeandikwa: "wivu wa nyumba yako utanila!"

Slaa hajapinga shutuma za kutokuwalea watoto wake...
 
Ritz jambo muhimu la ushauri kwako.
Mada hii umeianzisha wewe, tumejitokeza kuijadili, unatakiwa ubadilike kutoka kwenye ule mtindo wa kishabiki wa kuleta mipasho na kugeukia upande wa watu wenye fikra pevu kujadili hoja au mada uliyoleta, wewe ukiwa ndiye mwongoza mjadala kwa vile umeleta mada hii.

Ninachoshangaa unaendelea na mtindo wako wa kawaida wa kimipasho bila kujadili hoja uliyoileta kutokana na michango ya waJF. please, jitahidi kuwa flexable katika hili ili kuiongoza mada yako vizuri. Najua fika uwezo unao hivyo unaweza badili mwelekeo wa mipasho na kujikita kwenye hoja za msingi katika kuiongoza vizuri mada yako uliyotuletea.

Candid Scope,
Naona upendi michango yangu mpaka umeamua kuipa majina tofauti basi ngoja mie nijitoe kwenye huu uzi nakutakia mjadala mwema.
 
Last edited by a moderator:
Here we go again, tuko busy na fujo za ndugu zako wanazoendelea kuzifanya katika taifa letu hili la amani na hasa waloyafanya leo Dar na Zanzibar we uko busy na ndoa za watu? "Harusi siyo yako we waishonea suti?". Well miafrica ndivyo tulivyo Ritz

Hata kama ungeambiwa ni samaki ungeendelea kuchekelea tu kwa kuwa ni mwenyekiti wako sio?
 
Ni kweli una upendo na Mama Rose Kamili au unazungumza kiitikadi?
Yaani wewe thread zako nyingi nikizisoma uwa ni zile za kumhusu Dr.Slaa tu. Sijawahi kukuona ukizungumzia ishu nyingine za kijamii. Uwa unanifurahisha sana!!
 
Here we go again, tuko busy na fujo za ndugu zako wanazoendelea kuzifanya katika taifa letu hili la amani na hasa waloyafanya leo Dar na Zanzibar we uko busy na ndoa za watu? "Harusi siyo yako we waishonea suti?". Well miafrica ndivyo tulivyo Ritz

Huu ni unyanyasaji wa wanawake, Mnaacha kuongelea mada iliyopo ilimradi tu kumkingia kifua SLAA?
 
Dr slaa kwa vimwana ni balaa, ile picha aliyopiga wakati anampa Esther Wassira kadi inaelezea yote, jamaa ni balaa

Hukumu ya mahakama imenifurahisha sana, haiwezekani kule wezi wa wake za watu kwenye jamii yetu.
Halafu ndo anataka apwe urais?

hivi maisha ya mtu kama huyu anaweza kutufaa kweli wa tz?

Ameshindwa upadri, akao, mke akamshinda kaenda kupora mwingine na kazaa nae na sasa anataka kufunga ndoa.

Kama padri msaafu kashindwa kuheshimu amri za bibilia inayokataza kuzini na inayokataza kumtamani mke wa mtu, atawezaje kuiheshimu katiba?

Unapotaka ushauri kwa mtu, angalia kwanza maisha yake kabla ya kusikiliza mawazo yake.

Mtu ambae kashindwa kujiongoza kwenye maisha yake hawezi kuwa kiongozi mzuri.
 
wenzio wanaandamana we unahangaika na dr slaa,nenda kaungane na magamba wenzio kwenye maandamano ya kumkomboa ponda
 
Wanabodi,

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na ‘mkewe' Rose Kamili Slaa nee Sukum, akiomba mahakama hiyo imzuie ‘mumewe' Dkt. Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Laurnce Kaduri ambaye alisema amepitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dkt. Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo na amefikia uamuzi wa kuona hoja zilizowasilishwa mbele yake na Dkt. Slaa zikiomba mahakama hiyo iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose, ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.

Jaji Kaduri alisema Dkt. Slaa alikosea kudai kuwa Rose hakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake Josephine kwa taratibu za kisheria kwa sababu Slaa na Rose hawakuwai kufunga ndoa ila kulikuwa na dhana ya ndoa.

"Mahakama hii inaitupilia mbali, tena kwa gharama, pingamizi hilo la Dkt. Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa na haki ya kupinga ndoa yake kwa sababu hakuwa mke wake na wala hawajawai kufunga ndoa, kwa sababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili, sheria inawahesabu kama ni wanandoa, hivyo Mahakama hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa, yaani Slaa na Josephine na mahakama inatupilia mbali pingamizi la Slaa," alisema Jaji Kaduri.

Kesi ya msingi itatajwa mahakamani hapo Novemba 6 mwaka huu.

  1. Kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dkt. Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwa ajili ya kupatanishwa.
  2. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dkt. Slaa bado ni wanandoa.
  3. Dai la tatu, anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dkt. Slaa bado ni halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.
  4. Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) anadai mdaiwa wa pili (Josephine) alimshawishi mumewe (Dkt. Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.

"Pia, nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili"

Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dkt. Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.

Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili (Josephine) amlipe fidia ya Shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake.

Akaongeza kuiomba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.

Source: wavuti.com - wavuti
NINGEFURAHI SANA KUSIKIA KUTOKA LHCR NA TAMWA wanasemaje kuhusu hili. Hawajalipata au wanaendelea kumlinda Dr.
 
Ndoa kati ya Dr Slaa na Rose Kamili ilifungwa wapi, na lini?
halafu cheti cha ndoa huonyesha kama ni ndoa ya mke mmoja au wengi. sasa kama hilo halipo kwa nini Dr Slaa akataliwe kuoa wakati hakuna uthibisho kuwa alimuoa Rose kwa ndoa ya mke mmoja. Hata mimi nisiye mwanasheria nashangaa
 
Slaa Padri wakikatoliki ilkuwaje Akamuoa Rose Kamili ?
Pia wakatoliki Hawaruhusiwi Kuacha..ilikuwaje Akumuacha Rose Kamili ?
Huyu JOSEPHINE ni mke wa Mtu...si tumeambiwa tusitamani MKe wa Jirani ?
Slaa Anaishi na JOSEPHINE Bila ndoa...Si tumeambiwa tusizini ?

Slaa Kama anashindwa kutekeleza sheria za dini yake.....nchi ataiweza ?
 
Hukumu ya mahakama imenifurahisha sana, haiwezekani kule wezi wa wake za watu kwenye jamii yetu.
Halafu ndo anataka apwe urais?

hivi maisha ya mtu kama huyu anaweza kutufaa kweli wa tz?

Ameshindwa upadri, akao, mke akamshinda kaenda kupora mwingine na kazaa nae na sasa anataka kufunga ndoa.

Kama padri msaafu kashindwa kuheshimu amri za bibilia inayokataza kuzini na inayokataza kumtamani mke wa mtu, atawezaje kuiheshimu katiba?

Unapotaka ushauri kwa mtu, angalia kwanza maisha yake kabla ya kusikiliza mawazo yake.

Mtu ambae kashindwa kujiongoza kwenye maisha yake hawezi kuwa kiongozi mzuri.

Sahihisho, mahakama haijatoa bado hukumu ya kesi ya Rose Kamili kwa sababu hata hatua za awali za uskilizaji wa kesi hoyo bado, na sasa imepangwa tu kutajwa November 6. Sasa hoja ya hukumu ya kesi hiyo imetoka wapi?
 
Jamaa wametandikwa leo, mpaka wanajuta kwanini wameandamana, na wenzetu wengine leo hawapo uraiani wanalala custody, ngoja tuone kama wataendelea tena
 
Rose Kamili anatumiwa. Hana shida kwa sasa; ni mbunge na ameshajijenga. Angemwacha kibabu atengeneze first lady wake bila matatizo. Ina maana Rose....kama Willy akikuomba nanhii utampa? unaona! achana nae bhana

Kwani ndoa ni cheo? Acha wehu wewe... Ndoa ni mti wa katikati tunaopenda kula matunda yake. Nakubaliana na dai na 2 kwa nguvu zote. Slaa lazima amuoe Rose. Rose Kamili alikwisha mfumaniwa Josephine kule Dodoma akiwa na mumewe halali Dr Mkware. Dr akakasirika na akaamua kumtenga. Wehu na wazinzi watamtetea Dr Mkware. Bwana Yesu asifiwe, Ataonyesha ukuu wake na kubadilisha na kuitweza dhambi ya uzinzi ambayo kwa muda huu Dr anaifanya.
 
Rose Kamili anatumiwa. Hana shida kwa sasa; ni mbunge na ameshajijenga. Angemwacha kibabu atengeneze first lady wake bila matatizo. Ina maana Rose....kama Willy akikuomba nanhii utampa? unaona! achana nae bhana
Hakuna cha kutumiwa hapo anadai haki zake za msingi kabisa mume mchungu sana haiwezekani na slaa anatakiwa aoneshe ujasiri wake kwa hili as mambo madogo madogo hivi sio ya kuyadharau kama kweli unataka jamii ikuheshimu sasa kama alitelekeza watoto wake wa kuzaa kisa mwanamke akipewa taifa ndo itakuaje?tujiulize mara mbili mbili aisee..
 
Wanabodi,

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali kwa gharama pingamizi lilowasilishwa mbele yake na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willbrod Slaa lililokuwa likiomba mahakama hiyo ifute kesi ya madai iliyofunguliwa na ‘mkewe’ Rose Kamili Slaa nee Sukum, akiomba mahakama hiyo imzuie ‘mumewe’ Dkt. Slaa asifunge ndoa na mchumba wake Josephine Mushumbusi.

Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Laurnce Kaduri ambaye alisema amepitia kwa kina pingamizi lilowasilishwa na Dkt. Slaa na majibu yaliyojibiwa na mlalamikaji Rose anayetetewa na wakili wa kujitegemea Joseph Thadayo na amefikia uamuzi wa kuona hoja zilizowasilishwa mbele yake na Dkt. Slaa zikiomba mahakama hiyo iifute kesi ya msingi iliyofunguliwa na Rose, ni dhahifu na hivyo amezitupilia mbali.

Jaji Kaduri alisema Dkt. Slaa alikosea kudai kuwa Rose hakuwa na haki ya kufungua kesi hiyo ya kumzuia asifunge ndoa na mchumba wake Josephine kwa taratibu za kisheria kwa sababu Slaa na Rose hawakuwai kufunga ndoa ila kulikuwa na dhana ya ndoa.

“Mahakama hii inaitupilia mbali, tena kwa gharama, pingamizi hilo la Dkt. Slaa linalosema kuwa Rose hakuwa na haki ya kupinga ndoa yake kwa sababu hakuwa mke wake na wala hawajawai kufunga ndoa, kwa sababu sheria ya ndoa inasema mtu ambaye umeishawahi kuishi kama mke na mume kwa zaidi ya miaka miwili, sheria inawahesabu kama ni wanandoa, hivyo Mahakama hii inasema Rose ana haki ya kufungua kesi ya kuzuia ndoa ya wadaiwa, yaani Slaa na Josephine na mahakama inatupilia mbali pingamizi la Slaa,” alisema Jaji Kaduri.

Kesi ya msingi itatajwa mahakamani hapo Novemba 6 mwaka huu.

  1. Kesi hiyo ya madai ya ndoa Na.4/2012 ilifunguliwa mahakamani hapo na Rose dhidi ya Dkt. Slaa na Josephine kwa mara ya kwanza mapema Julai mwaka huu, akiiomba mahakama isikubali shauri hilo lipelekwe kwenye Bodi ya Maridhiano ya Masuala ya Ndoa ya kwa ajili ya kupatanishwa.
  2. Dai la pili, Rose anaiomba mahakama itanganze yeye na Dkt. Slaa bado ni wanandoa.
  3. Dai la tatu, anaiomba mahakama itamke kuwa ndoa baina yake na Dkt. Slaa bado ni halali kisheria na kwamba ndoa nyingine itakayofungwa kinyume na sasa ndoa hiyo itakuwa ni batili.
  4. Katika dai lake nne, mlalamikaji ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) anadai mdaiwa wa pili (Josephine) alimshawishi mumewe (Dkt. Slaa) kuivuruga ndoa yake na mumewe ambaye ni mdaiwa wa kwanza.

“Pia, nia ya wadaiwa hao wawili ya kutaka kufunga waliyopanga ifungwe Julai 21 mwaka huu katika eneo lolote lile, ndoa hiyo ihesabike kuwa ni batili”

Aidha anaiomba mahakama iwaamuru wadaiwa wamlipe fidia ya shilingi 50,000,000 kama gharama za matunzo ya watoto watoto wawili ambao Emiliana Slaa na Linus Slaa aliyezaliwa mwaka 1987 na kwamba walianza kuishi pamoja na Dkt. Slaa kama mume na mke, ambao amekuwa akiwahudumia kwa tangu mwaka 2009 baada ya mume wake kumkimbia.

Pia anaiomba mahakama imwamuru mdaiwa wa pili (Josephine) amlipe fidia ya Shilingi 500,000,000 kwasababu alimsababishia usumbufu mkubwa na kumharibia ndoa yake.

Akaongeza kuiomba mahakama hiyo impatie nafuu nyingine ambazo itaona inafaa.

Source: wavuti.com - wavuti
Hivi katika kipindi crucial kama hiki, chaos everywhere, mwanamme smart unawezaje kujadili mambo binafsi ya ndoa za watu, huku watu wenu wanatusumbua, hivi kweli uwezo wa kufikiri ndo umeishia hapo! au tuamini like father like son! uswahili bwana! arghhhhhh
 
watu wengine bana watu tunahofu na uhai wetu we unaleta mambo ya watu hapa!
 
Back
Top Bottom