Elections 2010 Pingamizi la CHADEMA latupwa

Aliahidi statement within siku tano au baada ya siku tano? Kuna tofauti kubwa hapo.

Kiranga,
unajua watawala wanafikiria Watanzania ni mabwege. Si kweli. FYI, kama ulimwengu ungekuwa unafanya longolongo kama Tz, ungekuta hadi leo motokaa haujavumbuliwa!!
 
Ngoma Nzito. Hata Kama Pingamizi limetupwa, Muhimu na Cha Kutia Moyo ni Kuwa Ujumbe Umefika.
 
acheni double standard kule nyamagana, yule alipambana na masha kakata rufaa na kashinda na kampeni zimeanza ooh wako makini na uamuzi uko sawa, ila wakiamua hukumu dhidi yenu hawako fair wamechaguliwa na rais.

hivi wanapotoa haki kwa upande wenu wanakuwa wamechaguliwa na mbowe ?

Hiyo ndo ilikuwa strategy yao kutaka kuttoka na hii hukumu ili watu wapate kupona. Ilipangwa strategically, hao ndo CCM. Ukweli ni kuwa mkulu amekiuka sheria that is all. Ila kwa sababu ya ufisadi hakuna haki.

Ngoja tusubiri kuona mbeleni, Chadema wakishinda wakwanza kumfunga nii huyo Tendwa kwa kutoa maamuzi ya kiupendeleo.
 
makamba anasema kuwa yametupiliwa mbali kwa sababu hayana mmsingi na pili yameleta 'bugudha'.....sasa sijui kwa muktadha upi....
 
hahaha huyu anayedai kuwa mume wa Josephine anamdai Dk Slaa na Josephine bilioni moja kutokana na usumbufu.,,,,kama fidia ya kuvunjwa kwa ndoa...

Naona mchezo umefika patamu manake amecontract mawakili kabisa......

wana vielelezo:picha za ndoa, vyeti vya kuzaliwa vya watoto, na vyeti vya ndoa.

hii ni kwa mujibu wa Channel tena habari zinazoendelea,,
 
hili suala wala halihitaji kutuchukulia muda mwingine. Watu wameingia kucheza kwa mujibu wa sheria zao, marefa wao, uwanja wao, jabulani yao na washangiliaji wao. Well.. go and play. Imeshatoka hii na haijalishi kama watatoa maelezo au hoja kuelezea mantiki ya uamuzi wao kwani hawaruhusiwi kisheria kutangazahadharani isipokuwa kuwataarifu wahusika tu.
 
hahaha huyu anayedai kuwa mume wa Josephine anamdai Dk Slaa na Josephine bilioni moja kutokana na usumbufu.,,,,kama fidia ya kuvunjwa kwa ndoa...

Naona mchezo umefika patamu manake amecontract mawakili kabisa......

wana vielelezo:picha za ndoa, vyeti vya kuzaliwa vya watoto, na vyeti vya ndoa.

hii ni kwa mujibu wa Channel tena habari zinazoendelea,,

huh! come again!

uchaguzi wa mwaka huu kweli moto.........
 
Tendwa hakumbuki yaliyotokea kenya mwaka juzi wakati wasimamizi walivyokuwa wanachakachua matokeo ili kibaki ashinde. Tendwa kasahau kabisa kuwa kufanya kivyo analimbikiza hasiraa za watu na umma utamhukumu huyu mzee, atamaliza maisha vibaya. It was fair and would be more respectable kama angetokea mbele ya vyombo vya habari kufafanua hiyo kauli siyo kwa style ya kibabe.

Hata kama yuko busy na mikutano mingine sioni kama kuna inshu muhimu kama hii, anajipunguzia mwenyewe heshima na imani kwa watanzania. Ukweli ni kuwa sababu za kutokuwa na imani naye zinazidi kuongezeka hata kama pingamizi kalitupaa, but kaahidi toka wiki jana kuwa anatoa majibu ndani ya siku hizo alizotaja, iweje leo anatutukana kwa kutoa majibu kwa style ya jeuri? hata kama ndo taratibu lakini yafaa watoe ufafanuzi basi wa kutueleza wananchi kuwa kutokana na taratibu zetu za kiofisi, majibu yetu yametolewa siyo kama hivi alivyofanya. TENDWA, WHY ARE YOU DOING THIS? UNAFANYA KAZI KWA AJILI YA WATANZANIA SIYO KWA MANUFAA YA WACHACHE, Usiharibu uchaguzi watu wakauana bure kwa sababu za busara kidogo hazijatumika. Unakula kodi zetu kwa kuendesha hizo seminar, nk. hukumbuki kabisaaaa. Anyway, kuna mwisho wake.
 
Sielewi kwa nini wati mlikuwa mnasubiri uamuzi wa Tendwa kwa hamu hivyo....sijui mlikuwa mnategemea nini..
 
Makamba akinukuu barua ya msajili alisema:
- Pingamizi la CHADEMA halina msingi wowote
- Msajili ametupilia mbali pingamizi hilo
- Pingamizi limeleta usumbufu kwa Wananchi.

Katika hatua nyingine, Bw. Mahimbo, amewaagiza wanasheria wake, wawafungulie kesi ya Madai Dr. Wilbrod Slaa na Josephine kwa kuishi na mke wake wa ndoa. Amedai fidia ya TZS 1 Billion na pia kuna mambo mengine yanayohusiana na watoto:

Sorece: News Bulletin - Channel 10
 
Tunajadili tetesi?Kama habari hiyo ni kwa mujibu wa Clouds FM kuna haja ya kuiangalia suspiciously kwani hao wahuni wanajikomba kwa ccm.Kama aliyetoa tamko ni Makamba then mnategemea angesema nini?Of course we certainly knew Tendwa angeanua nini but reliable sources haziwrzi kuwa Clouds au Makamba.
 
hahaha huyu anayedai kuwa mume wa Josephine anamdai Dk Slaa na Josephine bilioni moja kutokana na usumbufu.,,,,kama fidia ya kuvunjwa kwa ndoa...

Naona mchezo umefika patamu manake amecontract mawakili kabisa......

wana vielelezo:picha za ndoa, vyeti vya kuzaliwa vya watoto, na vyeti vya ndoa.

hii ni kwa mujibu wa Channel tena habari zinazoendelea,,

Hivi ww Kaiser unajua kuwa Channel 10 inamilikiwa na nani? Kumbuka hata wakati wa Mrema kuna mwanamke aliletwa eti amezaa na Mrema. au ulikuwa hujaruhusiwa kupiga kura? ni wale wale tu badala ya kutoa hoja za kuwaondolea umaskini wananchi wanaanza upupu.

Nalisema hili kwa kuwa lilisemwa na Makamba ambaye ni Katibu mkuu wa CCM.
Makamba akumbuke kuwa atakuwa sawa na Man'gula. CCM haina Adabu.

Je umewahi hata siku moja tangu Kampeni viongozi wa Chadema wanazungumzia kuanguka kwa Kikwete hadharani na ana Kifafa, na kutumia hicho kama kigezo cha kupatia kura? Kama unabisha tuteremshe DATA.
 
- Msajili ametupilia mbali pingamizi hilo
- Pingamizi limeleta usumbufu kwa Wananchi.

Hivi ni kivipi hasa hilo pingamizi limeleta usumbufu kwa wananchi? Kuna mwananchi hata mmoja aliyesumbuliwa na pingamizi hilo?
 
Hivi ni kivipi hasa hilo pingamizi limeleta usumbufu kwa wananchi? Kuna mwananchi hata mmoja aliyesumbuliwa na pingamizi hilo?

Labda kwa wananchi kuacha kufanya mambo yao ya msingi na badala yake kujadili juu ya pingamizi. Mjadaala haukuwa hapa JF tu bali hata mitaani kwetu madongo kuinama na huku kijijini kwetu.
 
Hivi ww Kaiser unajua kuwa Channel 10 inamilikiwa na nani? Kumbuka hata wakati wa Mrema kuna mwanamke aliletwa eti amezaa na Mrema. au ulikuwa hujaruhusiwa kupiga kura? ni wale wale tu badala ya kutoa hoja za kuwaondolea umaskini wananchi wanaanza upupu.

Nalisema hili kwa kuwa lilisemwa na Makamba ambaye ni Katibu mkuu wa CCM.
Makamba akumbuke kuwa atakuwa sawa na Man'gula. CCM haina Adabu.

Je umewahi hata siku moja tangu Kampeni viongozi wa Chadema wanazungumzia kuanguka kwa Kikwete hadharani na ana Kifafa, na kutumia hicho kama kigezo cha kupatia kura? Kama unabisha tuteremshe DATA.

Mkuu mchonga,mi hapa nimefanya kusaidia kuripoti kinachoendelea kwenye media zetu kuhusiana na hilo......nothing more! na nadhani ni muhimu tujue ili kweza kujua tunaijadili hii sredi katika muktadha upi
 
Na kwa nini Tendwa alionekana Cahnnel 10 kama vile anashake wakati akiongea na waandishi wa habari?
 
Kesi ya Pundamilia:

Hakimu Simba
Mwendesha Mashtaka: Fisi
Advocate wa Mlalamikaji: Chui
Wasikilizaji waliohudhuria: Tai
Askari Police na Magereza: Mbwa Mwitu

Kama Pundamilia ataokoka ni kwa maajabu tu ya Mungu Mwenyewe
 
Back
Top Bottom