Pingamizi la CHADEMA LATUPWA ,Siyoi Sumari ang'ara

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
[h=3]NEC Yamsafisha Siyoi: Pingamizi La Chadema Latupwa Nje[/h]
NEC yamsafisha Sioi (Tanzania Daima)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemsafisha mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, kutokana na tuhuma za utata wa uraia wake zilizokuwa zimewasilishwa katika rufaa na mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari.

Uamuzi huo wa NEC uliotangazwa jana mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi wa tume, Julius Mallaba, akisema kuwa kutokana na sababu kadhaa zilizoonyeshwa na jopo la ‘wataalamu’ wa tume waliokaa kupitia vifungu vya sheria za uhamiaji za Kenya na Tanzania, rufaa hiyo imeonekana haina msingi.

“Kwa mujibu wa maelezo na vielelezo vilivyowasilishwa pamoja na rufaa ya mrufani na kwa kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, Katiba ya zamani ya Kenya, Sheria ya Uraia ya Tanzania, Na. 6 ya mwaka 1995, Tume inakubaliana na uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi wa kukataa pingamizi la mrufani kwa sababu zifuatazo.

“Katika maelezo ya mrufani na vielelezo alivyowasilisha tume, hakuna popote ilipothibitishwa kuwa Sioi alipata uraia wa Kenya. Kwa kuwa mrufani ndiye aliyetoa madai kuwa mgombea alipata uraia wa Kenya kwa kuzaliwa kwake Kenya, basi alipaswa kuthibitisha madai yake kwa mujibu wa kanuni,” alisema.
 
Mbona maelezo ya hiyo sheria hajafafanuliwa nchi hii labda tumebakiwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania ndio wanaolinda haki na kubaki na uzalendo vinginevyo wangekuwa na tamaa wangekamata hii nchi na kuindesha Majaji wote wameoza hata yule mwingine aliyepewa tuzo ya Dr Martin Luther King juzi juzi hapa Cj Agustino alisimamia jopo la majaji kufuta sheria ya mgombea binafsi ha ha ha taifa la wagagagigigoko
 
Bila shaka hii ndio kazi aliyokuwa anasema EL aliporudi toka majuu.
 
Back
Top Bottom