Pinda: Uzinduzi Katiba mpya kuwa Aprili 2014

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amesema uzinduzi wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utafanyika ifikapo Aprili 26, 2014 katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar baada ya kukamilika.

Alisema hayo alipofungua semina elekezi kwa wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu mchakato wa kuelekea kuundwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyofanyika katika Kituo cha Mtakatifu Gasper, mjini hapa jana.
“Ni matarajio ya serikali kuwa Katiba mpya itakuwa imekamilika na kuzinduliwa ifikapo tarehe 26 Aprili 2014, katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema Pinda.
Source: http://www.ippmedia.


Nawasilisha.
 
habari nzuri sana,kimsingi inatakiwakatiba mpya kuwepo kabla ya uchaguzi mkuu 2015
 
Rasimu hii isiwe kama ile iliyorudishwa kufanyiwa marekebisho, lakini hii ni habari nzuri lakini serikali ikimiss up popote ina maana 2015 tutafany uchaguzi bila katiba mpya.
 
Inafurahisha! Ingawa bado naona ni mbali sana. Mchakato hadi kukamilika unachukua miaka mi3? Sidhani kama ni sawa. Kuna kitu kimefichika. Ila wajue kwamba usanii wowote, maandamano yatawatoa madarakani!
 
Back
Top Bottom