Pinda: Uvumilivu ukimshinda Kikwete msimlaumu - Onyo Chadema

Mhe Pinda leo amelonga hapa Bukoba mida ya saa 12 na kusema

Pamoja na serkali kuleta maendeleo makubwa Kagera. Pamoja na shule, barabara na mkonga wa mawasiliano.

Bei ya sukari ataishughulikia katika ziara yake. Bukoba ni km 70 toka kiwandani. Hadi tar 8 itatelemka bei.

Kuh amani ya nchi anasema Kikwete amewavumilia sana watanzania. Anasema maandamano haya yanapima uvumilivu wa Kikwete. Ila anasema anavyojua yeye uvumilivu wake unakaribia mwisho. Watu wenyewe hata mabomu mnaogopa, likipigwa moja watu wanakimbia wala hakuna hata mmoja anayesimama. Karibu sasa atasema basi na hapo ndipo mtakapo ona cha moto.

My take baby face anatishia amani ya tz na kujenga hofu katika mioyo ya watu kuwa wakati wowote watashambuliwa na vyombo vya dola.

naomba huyo mkubwa wake achoke hata sasa-then aanzishe vita-tuone nani atakimbia hii nchi-anajaribu kututisha-sisi si watoto wadogo wa kutishwa-
 
Mhe Pinda leo amelonga hapa Bukoba mida ya saa 12 na kusema

Pamoja na serkali kuleta maendeleo makubwa Kagera. Pamoja na shule, barabara na mkonga wa mawasiliano.

Bei ya sukari ataishughulikia katika ziara yake. Bukoba ni km 70 toka kiwandani. Hadi tar 8 itatelemka bei.

Kuh amani ya nchi anasema Kikwete amewavumilia sana watanzania. Anasema maandamano haya yanapima uvumilivu wa Kikwete. Ila anasema anavyojua yeye uvumilivu wake unakaribia mwisho. Watu wenyewe hata mabomu mnaogopa, likipigwa moja watu wanakimbia wala hakuna hata mmoja anayesimama. Karibu sasa atasema basi na hapo ndipo mtakapo ona cha moto.

My take baby face anatishia amani ya tz na kujenga hofu katika mioyo ya watu kuwa wakati wowote watashambuliwa na vyombo vya dola.


Wengine ni low kuliko alivyokuwa akionekana malaria sugu! Huu ni upishi wa habari na kwa vile tuko Jamii Forum na mada inahusu Kikwete basi sense zinapotea hata kushindwa kuona uongo wa mtowa mada! Hebu na atupe ushahidi wa anayoyaandika!
 
Wanatapatapa tu hao nani kasema Tanzania ina amani? Watu wametulia tu, wananchi wana njaa, maisha magumu, shida kibao halafu utasema huyo mtu ana amani kweli? Huyu Mr Kulia vipi mbona anaongea kama akili yake imepinda?!
 
huyu naye alikosa cha kusema jamani???
Wakati mwingine ni bora kukaa kimya, unaweza ukaonekana wa maana!

Mtoto wa mkulima na wewe.......pole

unayejiita mtoto wa mkulima jk anakupiga changa la macho ashindwe kuwavumilia cdm,hali amewavumili wezi wa rasilimali za taifa letu (anawachekea kila kukicha) itashangaza sana akishindwa kuwavumilia wakombozi wa umma hawa wanatujuza madhambi yote [zinaliwa mali za watz bila mafisadi kunawa eti] aumilienì tuamshwe mafisadi na wapambe wao waone vumbi, kila fisadi atawajibishwa na nguvu ya umma unaonaje wazo hilo?
 
sijawahi kuona serikali inayojisifia kwa mafanikio mengi ina tapa tapa kama hii.....
wanacho fanya CCM ni kama kinachoendlea Libya, Gaddafi na watoto wake kila siku wanatoa matamko kutishia watu watulie....kule marekani alipochukua Obama, Republicans (wakina Sarah Palin etc) wakaanza kuchochea mambo mengi sana kuhusu Obama na chama chake, lakini hatukuskia vitisho kutoka serikalini. Serikali ilielezea wasiwasi na Republicans na ika wahakikishia wananchi kwamba yapi ni ya msingi na watashugulikia vipi na yapi ni uuupuuzi...sasa hapa na kwa kujigamba kote kwamba demokrasia imekua, naona bado kuna vitisho vya kitoto..

Namhurumia sana Waziri Mkuu, amekubali kushushwa sana na hii serikali, ataondoka hapo ana dharaulika kupita Lowassa, na bora Lowassa yeye alijiwajibisha na alikua kiongozi "decisive", hakuogopa kufanya maamuzi magumu. lakini Kayanda Peter, yeye anapelekwa tu. Matrekta yake ya kilimo kwanza sasa hivi yanatumika kubebeba mizigo baadala ya kulima mashamba.....

hii nchi itabidi tukubali kurudi nyuma ili tuweze kusonga mbele..kwa hali hii hatutafika popote...
 
Wakati Chiligati na Wasira wanawaza kutumia nguvu ya dola kunyamaziasha nguvu za CDM za Pipooooossss Pawaaaaa-hekima ya pekee kwao ni kuwaelewa kiundani wa kero wanazotumia kuibomoa CCM kwa namna ambayo hawakuzoea tangu upinzani uingie nchini!!!!!!! Kazi ya msing ya chama cha kweli cha upinzani ko kote duniani ni kukiondoa madarakani chama tawala kwa kutumia udhaifu wa chama tawala; mfano ni Uingereza na Ujapani, na nchi nyingi duniani zinazotekeleza demokrasia ya kweli!

Hebu serikali ya CCM iguse CDM kama haitakuwa ndiyo kaburi la CCM? Baada tu ya katiba mpya itakayoandikwa kujumuisha matakwa ya wafadhili wa Tz kwa miaka zaidi ya 50 ndiyo itakuwa kifo cha CCM! Sababu za wazi ni hizi hapa:-

(1) Umma unaoshabikia siasa ya Tz ya leo ni vijana ambao hawana damu ya CCM na ukiritimba wa chama kimoja (CCM-zidumu fikra!!!!); hawa vijana wao wanataka kuona Tz ya kesho siyo ya miaka ya 1977 CCM ilipozaliwa;

(2) Masharti ya yule Mzungu David Martin na EU na wafadhili wote ni kwamba katiba mpya ipatikane haraka-wakati ukweli ni kwamba katiba mpya maana yake ni CCM out outright!!!!!!!!! Kama wanataka kujaribu waiguse CDM kwa nguvu ya dola waone moto na majuto kuwa mjukuu kwao!

(3) Maandamano yaliyofanyika kanda ya ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga, na Kagera, na yale ya mazishi Arusha) CDM wamethibishia waTz na ulimwengu kuwa ni ya amani kweli kweli !!!; sasa kama maandamano yatakayokuja kukamilisha ingwe yatakuwa na fujo basi kila mTz na ulimwengu atasema kuwa fujo hizo ni kutokana na mapandikizi ya CCM ndani ya maandamano hayo!

(4) Serikali ya CCM bila hela za wafadhili haiwezi kudumu hata mwezi mmoja-kuigusa CDM ni kuzidi kusimamisha na kufukuza hela za wafadhili- je mkwere atathubutu kufanya hilo?

(5) Ndani ya CCM kwenyewe tayari kumechafuka-kila mmoja anataka urais wa 2015 kwa kila mmoja kumuangusha mwenziwe; chini ya katiba mpya hakuna ambaye kizazi kipya kinamwelewa zaidi ya Dr wa Kweli!

(6) Katiba na sheria za nchi hii zinaruhusu nguvu ya umma kuondoa serikali ILIYO madarakani kwa maandamano ya amani, kama ilivyokuwa Tunisia na Misri-THIS IS THE ABSOLUTE TRUTH; yaani sauti ya umma, ama katika ballot box au barabarani pale njia za ballot zinaposhindina kama ilivykuwa Tz 31.10.2010!

IN BRIEF-serikali ya CCM ikisikiliza na kutekeleza propaganda za akina Chiligati na Wasira ndiyo itakuwa inaaga kutawala nchi hii kabla ya 2015!!!!!!!!!!!!!!
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewaonya wakazi wa Manispaa ya Bukoba na Watanzania wote kwa ujumla kuacha kuchezea hali ya amani ambayo imekuwepo kwa muda mrefu hapa nchini.

Yaap tusichezee PPRA Act 2004 na katiba yetu kwa malipo ya kifisadi, tusichakachue uchaguzi wa viongozi kwa kuleta ugadafi or sorry udikteta mfano ni uchaguzi 2010 kwa ujumla wake, TRA iache kusababisha hasara kwa kutokukusanya kodi kwa sababu ya rushwa, TAKUKURU waache kuonea wanyonge na waache woga na unafiki, usalama wa Taifa waache kuwa usalama wa mafisadi n.k

Ametoa onyo hilo jana jioni (Ijumaa, Machi 4, 2011), wakati akijibu risala ya Wazee wa Manispaa hiyo ambao waliwaomba Watanzania wote waitunze amani na wasikubali kudanganywa na kauli za uchochezi zenye lengo la kuwatia hofu na kuwakatisha tamaa.

Good! kauli za vitisho zinazotolewa na bosi wake Dr. Reveland.Sheikh.Advocate.Mwl.Prof.Gen.Mch.Eng Jakaya MK.

Akizungumza na maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform), Waziri Mkuu alisema: “Wana-Kagera mnajua maana ya vita kwa sababu mmepata rasharasha mwaka 1972 wakati Idd Amin aliposema anataka aje kunywa chai Mwanza lakini ninyi pia ni mashahidi wa vita halisi ya mwaka 1978,” alisema.

Kauli za vitisho....au vipi?

“Hivi majuzi tumepata matatizo kule Gongo la Mboto, wakati watu wanakimbia kuokoa maisha yao, wako wengine waaliokuwa wakikimbilia kwenye nyumba za wenzao ili kuiba mali zilizoachwa. Ni ajabu iliyoje kumsikia mtu akitamka: Bora vurugu bwana!” alishangaa.

Duh! Kumbe ilipigwa makusudi ili kutishia wananchi.....enh hata mfe njaa, mkae gizani, mkose ajira, mkose elimu..msipige kelele..kisa Gongo la..moto..oh mboto...eeh hii kweli ni zaidi ya kauli za vitisho...hii ni action movie oh...sorry movement.

Alisema kama kamwe wananchi wasikubali uchochezi huo kwani maandamano na vurugu siyo suluhisho na amani ikishapotea kuirudisha ni gharama kubwa mno.

Usijali tumekuelewa...si unamaanisha ugadafi au unamaanisha nini? Poa tu vifaru mnavyo...ndege mnazo...ni zenu na watoto wenu na si za watanzania...very good.


CCM CCM CCM......IF YOU DON'T LEARN FROM HISTORY...BE READY TO WRITE A NEW CHAPTER ON IT.
 
Tunisia na Misri sio chama cha upinzani kama hapa Tz ndicho kilishawishi raia wanaöndamana ni wanaCDM na wala sio wapenzi wa vyama vingine,Cdm kikitaka kupata aibu kikaandamane Zenji,Cdm peke yenu msijidanganye kuwa mtaweza,ili yatokee hayo ni cc kuviweka kando vyama na kuliweka Taifa mbele
 
Nilikuwa namheshimu sana Pinda na kusema ukweli, mimi nilikuwa mmoja wao wa wale waliokua wanapinga usambazwaji wa meseji kwamba mheshimiwa alikuwa akifanana na Mnyama fulani aishie majini jamii ya Mjusi wakubwa, but to this far, nimeamua kujiunga na kambi ileeee kwamba huyu jama/mzee/kijana mwenzetu hajiheshimu hata kidogo, wala hafai na hastahili kuitwa mtoto wa mkulima labda turefushe hilo jina na kuita hivi Mtoto wa Mkulima Bepari. Eeeh si hata mabepari nao ni wakulima labda mwenzetu ndio alichokuwa akimaanisha nyie mkakimbilia kummwagia sifa kemkem..

Huyu huyu ndio Musa huyu, Ndio Masihi huyu, anachafuliwa na Mkuu wake tu lakini yuko smart.....maneno meengi wapi bana, huyu ni wale wale tu, nasema Pinda umepoteza heshima yako mbele ya jamii iliyokupenda na kukuheshimu.....
 
waziri mkuu mizengo pinda amewaonya wakazi wa manispaa ya bukoba na watanzania wote kwa ujumla kuacha kuchezea hali ya amani ambayo imekuwepo kwa muda mrefu hapa nchini.

Ametoa onyo hilo jana jioni (ijumaa, machi 4, 2011), wakati akijibu risala ya wazee wa manispaa hiyo ambao waliwaomba watanzania wote waitunze amani na wasikubali kudanganywa na kauli za uchochezi zenye lengo la kuwatia hofu na kuwakatisha tamaa.

Akizungumza na maelfu ya wakazi wa manispaa ya bukoba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mayunga (uhuru platform), waziri mkuu alisema: “wana-kagera mnajua maana ya vita kwa sababu mmepata rasharasha mwaka 1972 wakati idd amin aliposema anataka aje kunywa chai mwanza lakini ninyi pia ni mashahidi wa vita halisi ya mwaka 1978,” alisema.

“hivi majuzi tumepata matatizo kule gongo la mboto, wakati watu wanakimbia kuokoa maisha yao, wako wengine waaliokuwa wakikimbilia kwenye nyumba za wenzao ili kuiba mali zilizoachwa. Ni ajabu iliyoje kumsikia mtu akitamka: Bora vurugu bwana!” alishangaa.

Alisema kama kamwe wananchi wasikubali uchochezi huo kwani maandamano na vurugu siyo suluhisho na amani ikishapotea kuirudisha ni gharama kubwa mno.

“kila kukicha, kuna watu wanazua madai ya kila aina, mara kura zimeibiwa, mara katiba mpya; walichoamua ni kutembea nchi nzima … pengine hawana kazi za kufanya ndiyo maana wanatembea kuitisha maandamano huku na kule,” alisema.

Alisema: “kama suala ni kuing’oa ccm madarakani ni laima wajiulize maswali ya msingi ni vipi wataweza kuindoa ccm katika matawi, mashina, kwenye kata na tena mjijengee uhalali kwa wananchi hadi wawakubali.”

“msipofanya hivyo, mtatembea weee lakini ccm haingoki ngo!,” alionya na kuongeza kwamba: “uongozi unategemea wananchi wanavyotutazama… wanatupima, je watu hawa wataweza kutusaidia? Je watajali shida zetu?” alitahadharisha.

Mapema, katika risala yao iliyosomwa na mzee haruna almasi, wazee hao waliomba kupatiwa matibabu bila mlolongo mrefu ili wasihangaike. “tunaomba serikali ituwekee utaratibu mwepesi wa kuwasaidia wazee kupata tiba…”, alisema mzee almasi.

Wazee hao ambao walisema wanaiunga mkono hotuba ya rais jakaya kikwete aliyoitoa februari 28, 2011 wakati akilihutubia taifa, pia waliomba kuwe na uwakilishi wa wazee katika ngazi mbalimbali za vikao vya kufanya maamuzi kuanzia kwenye serikali za mitaa hadi bungeni.

Kesho (jumapili, machi 6, 2011), waziri mkuu atakuwa wilayani chato ambako anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la halmashauri ya wilaya hiyo na kufungua saccos ya mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye shule ya msingi ya chato.



Imetolewa na:

Ofisi ya waziri mkuu,
jumamosi, machi 05, 2011



tunaomba picha ya umati tafadhali
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewaonya wakazi wa Manispaa ya Bukoba na Watanzania wote kwa ujumla kuacha kuchezea hali ya amani ambayo imekuwepo kwa muda mrefu hapa nchini.

Ametoa onyo hilo jana jioni (Ijumaa, Machi 4, 2011), wakati akijibu risala ya Wazee wa Manispaa hiyo ambao waliwaomba Watanzania wote waitunze amani na wasikubali kudanganywa na kauli za uchochezi zenye lengo la kuwatia hofu na kuwakatisha tamaa.

Akizungumza na maelfu ya wakazi wa Manispaa ya Bukoba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mayunga (Uhuru Platform), Waziri Mkuu alisema: "Wana-Kagera mnajua maana ya vita kwa sababu mmepata rasharasha mwaka 1972 wakati Idd Amin aliposema anataka aje kunywa chai Mwanza lakini ninyi pia ni mashahidi wa vita halisi ya mwaka 1978," alisema.

"Hivi majuzi tumepata matatizo kule Gongo la Mboto, wakati watu wanakimbia kuokoa maisha yao, wako wengine waaliokuwa wakikimbilia kwenye nyumba za wenzao ili kuiba mali zilizoachwa. Ni ajabu iliyoje kumsikia mtu akitamka: Bora vurugu bwana!" alishangaa.

Alisema kama kamwe wananchi wasikubali uchochezi huo kwani maandamano na vurugu siyo suluhisho na amani ikishapotea kuirudisha ni gharama kubwa mno.

"Kila kukicha, kuna watu wanazua madai ya kila aina, mara kura zimeibiwa, mara Katiba mpya; walichoamua ni kutembea nchi nzima … pengine hawana kazi za kufanya ndiyo maana wanatembea kuitisha maandamano huku na kule," alisema.

Alisema: "Kama suala ni kuing'oa CCM madarakani ni laima wajiulize maswali ya msingi ni vipi wataweza kuindoa CCM katika matawi, mashina, kwenye kata na tena mjijengee uhalali kwa wananchi hadi wawakubali."

"Msipofanya hivyo, mtatembea weee lakini CCM haingoki ngo!," alionya na kuongeza kwamba: "Uongozi unategemea wananchi wanavyotutazama… wanatupima, je watu hawa wataweza kutusaidia? Je watajali shida zetu?" alitahadharisha.

Mapema, katika risala yao iliyosomwa na Mzee Haruna Almasi, wazee hao waliomba kupatiwa matibabu bila mlolongo mrefu ili wasihangaike. "Tunaomba Serikali ituwekee utaratibu mwepesi wa kuwasaidia wazee kupata tiba…", alisema Mzee Almasi.

Wazee hao ambao walisema wanaiunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Februari 28, 2011 wakati akilihutubia Taifa, pia waliomba kuwe na uwakilishi wa wazee katika ngazi mbalimbali za vikao vya kufanya maamuzi kuanzia kwenye Serikali za Mitaa hadi Bungeni.

Kesho (Jumapili, Machi 6, 2011), Waziri Mkuu atakuwa wilayani Chato ambako anatarajiwa kuweka jiwe la msingi katika jengo la Halmashauri ya Wilaya hiyo na kufungua SACCOS ya Mshikamano kabla ya kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye shule ya msingi ya Chato.



IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, MACHI 05, 2011

Umenena mkuu,

Tutailinda amani yetu kwa gharama yoyote ile.
 
Hivi Tanzania ni nchi ya mtindo gani! Mbona hata wale niliokuwa na imani nao angalau kidogo nimeshaanza kuona kama hawana la kuwatetea wanyonge?

Waziri mkuu akumbuke hayo matawi ya CCM anayoyasema yapo wakati watu bado wana imani na serikali yao, imani hiyo ikipotea hakuna cha CCM wala mwananchi gani! Badala ya kukimbilia kulaumu tokeni maofisi msimamie kazi, acheni uswahiba wa kupeana madaraka kindugu au kirafiki, waondoeni mafisadi, kusanyeni fedha na muache kulipana posho na mishahara ya ajabu wakati watu wenu wana taabika.

Acheni safari zisizo na tija kwa wana nchi maana zinatumia fedha nyingi mno. Muwajali vijana. Mkifanya hivyo, panueni midomo mseme!!
 
International Criminal Court nayo ipo haijafutwa, Ocampo anasubiri viongozi kama Ghadaffi,
 
Wameshaanza kutapatapa. Tatizo wanamtumia mtu ambaye hawezi kujibu hoja zaidi ya kulia lia.

Halafu anaongea na watu wa mijini tu kumbe anasahau kuwa huko vijijini ukitamka CCM basi uwe na akili ya kichaa..watu mamepigika na hawataki tena kusikia CCM
 
taahira over mtoto wa mkulima bepari. Hv ww huwa una2mw na nan lkn? Kwel ww ni hafif, mwili, akil, na hyo roho yko km ya mkwere na pnda! Cku 2kiingia barabaran 2naanza na ww then pinda. C ujifunze 2 hata kunyamaza? 2meshajua ww ni b'mdgo wa mkwre kwn mpk uongee sn?
Umenena mkuu,

Tutailinda amani yetu kwa gharama yoyote ile.
 
Tunisia na Misri sio chama cha upinzani kama hapa Tz ndicho kilishawishi raia wanaöndamana ni wanaCDM na wala sio wapenzi wa vyama vingine,Cdm kikitaka kupata aibu kikaandamane Zenji,Cdm peke yenu msijidanganye kuwa mtaweza,ili yatokee hayo ni cc kuviweka kando vyama na kuliweka Taifa mbele

Ndugu ninasikitika sana kwa kauli yako kwamba unataka kuona CDM wakiaibika eti waende Zanzibar,Na pia nasikitika sana unaposema hawataweza wenyewe...ukiwa na maana unataka waombe msaada kwa vyama vingine ambavyo siwezi kamwe kuviiita pinzani kwani vinanguvu ya soda.

Hamad Rashid unadhani ni mpinzani kweli tena wakati kashatengewa sinia la ubwabwa kule Zanzibar....!!!!Unasubutu kusema haupo tayari kama wewe kuunga harakati hizi za CDM kisa wanajifanya wanaweza wenyewe...!!! Kama kweeli unataka kuweka mustakabali wa Taifa mbele usingeangalia ni chama gani ila ungeangalia wanachosema ni kweli au uongo...na kama ni kweli basi ungeungana nao kusukuma mbele gurudumu hilo hadi kufikia lengo la yale utakayo.

MY TAKE:
Weka mbali swala la chama, angalia point zinazotazamishwa kama zinakugusa kuwa ni za kweli basi jiunge katika mbiu ya kweli. Kama chama chako hakipata nafasi ya kuyaona haya basi hicho ni miongoni mwa vile vyama vya msimu wa RUZUKU.

Pole ndugu amka na waamkao, toka usingizini kwa walalao kama unataka kuwahi utakako kwenda. You're a geat thinker...You have to think...!!
 
Mje Goms tafadhali wembe umekata mbuyu
wembe mmoja mbuyu chini ti krikiti!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom