Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Leo tukiamua kusupport mavazi yanayozalishwa nchini tutafika mbali,tunachohitaji ni uzalendo wa kweli na siyo ulimbukeni wa mavazi toka nje.Lingine ni swala la ubora wa mavazi yetu ya ndani, inawezekana watu hawapendi kuvaa mavazi ya ndini kisa tu yanafubaa na kuchujuka upesi.Nia ya dhati ianze na viongozi wetu, ku-ssuport viwanda na kuvaa mavazi ya ndani.

Viwanda vya ndani vipi Mkuu, vyote vimetafunwa na BWM kamalizia kupiga bei. Kiltex, Mutex, Sunguratex, Urafiki angalau wachina wanatengeneza khanga na vingine vyote kama sio marehemu basi ni mahutihuti.

Na laana iwapate watanzania waliokua wamepewa dhamana ya kuendesha lakini wakaviuwa kwa maslahi yao.
 
Huyu Pinda asitake kuwapangia watu maisha yao. Haya matamshi yake yameanika utupu wa busara zake. Nashangaa hata huo uwaziri mkuu aliupataje.

Mazee kesho usishangae akianza kuwanusa midomo mawaziri kama wamepiga mswaki, keshokutwa atawaangalia chupi zao kama safi.

Waziri Mkuu ningetegemea aongelee mikakati ya kujenga viwanda vya suti Tanzania anayependa kuvaa suti apate kwa bei rahisi, nyingine tu export. Anayependa kuvaa lubega na mgolole haya, wa Kaunda suit na Safari suit haya, hata ma nudist kwenye nudist colonies zao poa.Si ndiyo mambo ya kujinafasi na uhuru hayo?

Mwanafalsafa mmoja wa Uchina ya zamani alisema, mitindo inayokubalika dunia nzima ni migumu sana kui resist, na unaweza kuamua kuikataa ukapitwa na dunia, au unaweza kuamua kuikubali ukawa mshindi.

Hao wachina wenyewe wanaowatolea mifano wote wanapiga mi pinstripes na mi western suits siku hizi, ila wenzetu wanatengeneza wenyewe.This is what the PM should be focused on, not some small minded big government nannysm.

0010dc53fa040b2be7d101.jpg

Chinese Premier Wen Jiabao (R) and his counterpart of the Democratic People's Republic of Korea (DPRK) Kim Yong Il wave during a ceremony marking the 60th anniversary of the establishment of the China-DPRK diplomatic relations and the launch of the China-DPRK Friendship Year in Beijing, capital of China, March 18, 2009. (Xinhua/Ma Zhancheng)
 
Bluray,

..Wachina walikuwa wanavaa uniform kwa miaka mingi sana. baada ya mambo yao kuwa mazuri ndiyo wameanza kuvaa suti.

..nadhani anachokizungumzia Waziri Mkuu Pinda ni tabia ya watumishi wa umma na viongozi kupenda kujirusha wakati hali yetu ya kiuchumi siyo nzuri.

..inawezekana tatizo la Pinda ni mapungufu yake ktk kuwasilisha ujumbe huo. lakini ukweli unabaki palepale kwa serikali yetu ina matumizi makubwa yasiyo ya lazima and something needs to be done.
 
Sidhani kama kuna mtu atayeleta ubishi kuhusu matumizi mabaya ya fedha za umma. Lakini mtumishi yeyote wa umma kama akitumia hela au kipato chake halali kwa nini asiweze kukitumia kwa kadri apendavyo iwe kuvaa suti za Brooks Brothers au Jos. A Bank?

Kama mtu kipato chako kidogo na unachagua kwenda kilabuni kila jioni kunywa mikangala yako..heck...knock yourself out. Kama unatumia hela za umma kujirusha then hapo kutakuwa na tatizo.
 
Bluray,

..Wachina walikuwa wanavaa uniform kwa miaka mingi sana. baada ya mambo yao kuwa mazuri ndiyo wameanza kuvaa suti.

Sasa kama hakuna kuvaa suti mpaka mambo yawe mazuri kwa nini yeye anavaa? Si unamuona hapo juu au siye Pinda huyo?
 
Bluray,

..hata mimi nasubiri kuona kama Pinda ataachana na suti baada ya hili tangazo lake.

..kama hiyo picha imepigwa baada ya Pinda kudai atapunguza uvaaji suti na mambo mengine ya anasa-anasa na ufujaji basi atakuwa amejimaliza mwenyewe kisiasa.

..binafsi nadhani tunakosea kwa kuwa-fixated ktk suala la kuvaa suti. mjadala huu ni mkubwa na mpana na unahusisha UADILIFU na UMAKINI wetu ktk MATUMIZI YA SERIKALI na VIPAUMBELE VYA TAIFA LETU.
 
Hatukosei, PM ndiye kakosea badala ya kuongea vitu substantive kama nilivyosema hapo juu - viwanda, uzalishaji wa nguo nchini, suti zinazokuwa locally produced with high quality and affordable prices, some even for export since we have all the natural and economic advantages- yeye anaenda kwenye superficialities.

Hii inakuonyesha how weak his thought process is.
 
Bluray said:

..kauli ya Pinda imetoa nafasi ya mjadala huu kuwa trivialized.

..ni kweli kwamba Pinda amekosea.

..lakini kosa kubwa ni kunaswa na mtego wa mapungufu ya kauli ya Waziri Mkuu Pinda. nadhani hilo ndilo tatizo la mjadala huu hapa jamii forums.
 
I believe some of the discussion going on here, quite apart from trivializing Pinda, transcends the Pinda mediocrity by analyzing the bigger picture.

Mambo mengine ni communication skills na press.Kimsingi the theme- minus the smallmindedness of bashing western suits as if we cannot be multifacteted- is right, but the level of intellect potrayed gives the impression that we have the wrong man as PM.

This is something I pointed out from day one.

Tatizo la Mkapa na Lowassa ni mafisadi arrogant (big issue1) otherwise I would rather have a Mkapa administration with Lowassa as PM than the incumbent jokers.
 
ITatizo la Mkapa na Lowassa ni mafisadi arrogant (big issue1) otherwise I would rather have a Mkapa administration with Lowassa as PM than the incumbent jokers.
Mkuu wangu sema unatania!..Laa sivyo, nitashindwa kuelewa ikiwa kweli Mtanzania mwenye upeo mkubwa kama wako utapendelea kuongozwa na watu kama Mkapa na Lowassa kwa sababu ya hoja ndogo kama hii ya Suit!..

Duh! ama kweli Ndivyo Tulivyo mkuu wangu samahani sana lakini hili la Suit wala sioni uzito wake kwa sababu Pinda hakutaka ku beat the Bush kazungumza alichozungumza..kasema anachokiona yeye na hakika uzito kabisa kulinganisha na madudu ya Mkapa na Lowassa..

Je, kuna ukweli wowote ktk maelezo ya Pinda achana kabisa namtazamo wake!....Ni kweli sisi weusi tuna tatizo sana la matumizi yetu ktk mavazi na maswala ya anasa iwe Hollywood, NY, Paris, London hadi Ukerewe!.. sisi tuna thamini sana vitu vya anasa badala ya ku invest fedha zetu ktk uzalishaji, tunategemea zaidi vipaji vyetu (tulichobarikiwa) kuwa ndio njia kuu za uchumi wetu..Na tunatumia kama vile hakuna kesho!

Maendeleo kwetu ni kwetu ni kuwa na vitu vya anasa na sii investment gani tumewekesha zikizalisha!

Sasa pengine kama kweli siku itafikia tukaweza kupunguza matumizi ya kijinga kama haya pengine itasaidia kitu lakini Ukweli bado unasimama kwamba sisi tuna tatizo la ULIMBUKENI..

Sababu zinaweza kuwa tofauti, Pinda kwa upeo na mshangao wake kuiona hoja tofauti na wewe pamoja na wengine wote but still ULIMBUKENI wa mtu mweusi ni tatizo kubwa..
 
Hivi jamani kuvaa ama kutokuvaa suti, do we really want to discuss that as a nation? Kuvaa ama kutokuva suti? I think this is individual issues? Does it deserve the attention we are giving it? Yani our neighbours say Watanzania wanajadili kuvaa ama kutokuva suti?

Kweli dunia itatuchukulia serious kwenye mambo mengine? Kwa nini tusiache pumba zingine ziende na upepo? Nasikia aibu kusoma headline inahusu suti? Wakati watoto wetu wanakaa chini, wagonjwa wanakufa kwa magonjwa yanayozuilika and here we are including JF discussing about suits.

Please naomba guys let us go back to issues otherwise we will be like Pinda .. PM asiyejua priorities ? Kuvaa ama kutokuvaa suti , does it really matter?

Ciao
 
Please naomba guys let us go back to issues otherwise we will be like Pinda .. PM asiyejua priorities ? Kuvaa ama kutokuvaa suti , does it really matter?
Mkuu it matters ikiwa PM kazungumzia na nadhani JF wanafanya kile kinachotakiwa kufanya.. Kusema wazi UBOVU wa viongozi wetu, ila tu tujaribu kujifunza na kuongezea vitu muhimu kama ulivyozujngumza hapo juu.

Kiutendaji hizi suti na magari ya fahari ndio sababu watoto wetu hawana nguo wanakaa chini madarsani na wagonjwa wanakufa bila kupatiwa dawa...Serikali yetu ni sawa na mzazi MLEVI hivyo ukizungumzia Pombe kuwa sababu sidhani kama kuna kosa ila jinsi PM Pinda alivyo wakilisha the all issue ndio kichekesho..

Somo bado linabakia palepale huwezi kunambia mlevi wa anasa (pombe) ukasahau familia yake ni swala ya individuals!

If it is a problem ni muhimu tulizungumzie...
 
Mkuu heshima mbele! Mi ninahisi ya kuwa kuna-frustration kubwa sana hivi sasa kuhusu uongozi uliopo, na frustration ndizo zinazomfanya hata mkuu Bluray kusema hata kheri akae na viongozi jeuri lakini wenye akili (intelligent).

Lakini mi naamini ya kuwa Tanzania na sisi wananchi wake tunapenda ku-blame exterior things lakini hatuangalii internally. Hapa kuna issue nyingi sana ikiwa ni pamoja na kuwa hatukuwa tayari (respect to the few who were more open minded) kukubali kuwa our leaders like JK and Pinda are people with a narrow view of life and who do not reflect the kind of leaders that we aspire for. We projected our desires and aspirations na tukaamini kuwa Pinda is really broad minded and intelligent and all that, ditto for JK.

Sasa ukimkuta prime minister yuko preoocupied na mavazi katika nchi maskini kama Tanzania basi ujue huyu mtu kakosa kitu cha kusema, hana la kuchangia, maana haelewi kinachoendelea.
 
Hivi jamani kuvaa ama kutokuvaa suti, do we really want to discuss that as a nation? Kuvaa ama kutokuva suti? I think this is individual issues? Does it deserve the attention we are giving it? Yani our neighbours say Watanzania wanajadili kuvaa ama kutokuva suti?

Kweli dunia itatuchukulia serious kwenye mambo mengine? Kwa nini tusiache pumba zingine ziende na upepo? Nasikia aibu kusoma headline inahusu suti? Wakati watoto wetu wanakaa chini, wagonjwa wanakufa kwa magonjwa yanayozuilika and here we are including JF discussing about suits.

Please naomba guys let us go back to issues otherwise we will be like Pinda .. PM asiyejua priorities ? Kuvaa ama kutokuvaa suti , does it really matter?

Ciao

Pinda yuko sahihi kuvaa suti ni gharama mno kwa uchumi wa nchi na ni kumaliza pesa za kigeni.Kwa nini na sisi tusivae nguo za batiki na vitenge zinazotengenezwa na viwanda vyetu na pamba yetu humu humu nchini.

Kuvaa nguo zetu wenyewe kungesaidia kupanua viwanda vya ndani,vya ushonaji n.k na mafundi cherehani wetu waliozagaa mitaani wangekuwa na soko la uhakika la kazi zao ambalo linachukuliwa na ready made suits za ulaya.Viwanda vyetu vikipanuka na wakulima watalima zaidi na hivyo kupata faida zaidi.Yako manufaa mengi tu ndio maana kiongozi wa Indonesia anapenda kuvaa bidhaa zake zizalishwazo nchini mwake hata kama si nzuri kama suti za ulaya.

Watu wa afrika magharibi na kati huvaa sana nguo za viwanda vyao si kuanzia akina baba,akina mama ndio usiseme hupenda zaidi hizo kuliko za ulaya hivi watanzania kuna nini kwenye vichwa? Afrika magharibi na kati watu wameamshwa sana kuvaa vyao Tanzania wasomi wazima hawaelewi wanamkalia kidedea prime minister wengine hadi kuthubutu kusema apimwe akili.Tanzania ruhusuni uraia wa nchi zaidi ya moja haraka kuna hawara yangu anataka kukimbia nchi kachoka ujinga wa Tanzania.

Kama kweli raisi a mawaziri ni wazalendo na wakareketwa wa nchi na bidhaa zake waanze kuvaa nguo za urafiki,karibu textile na kadhalika na viatu aina ya yeboyebo zinazozalishwa na viwanda vya Tanzania. Nasubiri kwa hamu siku nitakayoona Kikwete katinga mashati na suruali za kitenge cha urafiki halafu chini akamalizia miguuni kwa kuvaa yeboyebo za sh.elfu moja akienda kukutana na Obama halafu tuone kama Obama atamtambua kuwa ni Raisi wa Tanzania au la kwa kuangalia kitenge na yeboyebo.
.
 
Maneno matupu hayavunji mfupa.Pinda kafanya nini concrete to this end so far?

Mimi sasa hivi naanzisha "Pinda watch" tuone kama atavaa suti tena au vipi.
 
Hivi ina maana Pinda hakujua kabisa kwamba kiongozi kuwa simple hata kimavazi ni sihara njema ? Yaani alihitaji kwenda Indonesia ndiyo arudi na kelele hizi ? CCM bwana leo Pinda kaja na hili . Sumaye aliwahi kusema kwamba ahakujua Nchi ilikuwa masikini hadi bada ya kuachana na uwaziri mkuu na JK nadhani anajiuliza kwa nini Nchi ni masikini wakati tuna kila kitu ila hajiulizi kwa nini anadhani kuomba omba na ujenzi wa Taifa na anakutetea . Ninashangaa bado kasi hizi .
 
Kwani hizi suti si wananunua kwa pesa yao wenyewe? Halafu ningemuelewa angevaa shati lililotengenezwa na kitambaa cha Tanzania badala ya kuvaa batik ya Indonesia kwenda kumuona Rais wa Indonesia.
 
Huwa namfananisha Mheshimiwa Pinda kama godoro la sufi ambalo liki kojolewa mara moja huoza...

Nadhani yupo tu kwenye system kama kofia iliyotundikwa kwenye msumali chumbani...Hajui kinachoendelea Serikalini..! MSIMLAUMU SANA..!!

Na nadhani huwa anaandaliwa vitu vya kufanya na secretary wake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom