Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Tuna mambo mengi ya msingi yanayolisumbua Taifa hili. Mavazi na Kiongozi au Mtendaji kavaaje si mojawapo! Picha za kwenye luninga wakati wa taarifa ya habari saa 1 na saa 2 jioni uko sebuleni na mke/kimada wako lazima ipendeze ati.
 
You are not serious on this!
 
Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.

Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.

Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!

Umesema, wana jf wanaomtwanga pinda nawashangaa .. emancipate yourself from mental slavery, Suti sio vazi la kiafrika, hili vazi ni la wazungu kwenye baridi, inashangaz hata wasomi wetu hawajui hili.

Ujinga wa mwafrika?
 
JK amefanikiwa lengo lake, alijua jamaa hakua=wa na mpango hata wa kuwaza kuwa waziri sembuse PM.

Hii ni kuwa Pinda bado anaweweseka na cheo hicho!

usije ukakuta mpak atakavyoondoka madarakani akaendelea kufikiri yee ni PM

Viatu vikubwa hivi!!

safari zote za nchi za Asia mkulima ndio anaachiwa? Jamaa angeenda Marekani angesema tujenge Havard bongo, tuanzishe kampuni ya microsoft bongo, tuwe na white house yetu bongo, tumwite raisi wetu Obama kama wanavyofanya Marekani. Labda jamaa ameamua kuwatafutia topics ze comedy. Just curious!
 
Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.

Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.

Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!

Anasema tuuuuu, atatenda lini. Ni bora anachoona kinafaa kwa Tz na akisimamie kitendeke maana power hiyo anayo. Akija sema nilisema hamkufuata ni weakness maana amepewa hiyo power na anashindwa itumia.

Halafu kama hajui chochote kuhusu kubana matumizi na CCM yake haina dira na basi apunguze safari, maana kila akisafiri atakuja na mengi mpaka atanshindwa aanzie wapi kuyatekeleza atabaki kusema sema tuu,
 
Umesema, wana jf wanaomtwanga pinda nawashangaa .. emancipate yourself from mental slavery, Suti sio vazi la kiafrika, hili vazi ni la wazungu kwenye baridi, inashangaz hata wasomi wetu hawajui hili.

Ujinga wa mwafrika?

Suti ni vazi la kiafrika, vile vile ni vazi la Kijapani, Korea, China, nk, yaani la Kimataifa. Ni vazi linakubalika na wengi na lina soko, naamini PM ana uwezo wa kupromote uzalishaji wa suti nyingi zaidi nchini ili bei ishuke kuliko kuwahisi watu wasivae ili kubana matumizi.
MP Pinda angesimamia kubana matumizi ya serikali kwanza, ama kuleta hiyo agenda kwenye NEC yao ili wajumbe wao waachane na suti kwanza.
 
Anasema tuuuuu, atatenda lini. Ni bora anachoona kinafaa kwa Tz na akisimamie kitendeke maana power hiyo anayo. Akija sema nilisema hamkufuata ni weakness maana amepewa hiyo power na anashindwa itumia.

Halafu kama hajui chochote kuhusu kubana matumizi na CCM yake haina dira na basi apunguze safari, maana kila akisafiri atakuja na mengi mpaka atanshindwa aanzie wapi kuyatekeleza atabaki kusema sema tuu,

Huyu nae! kama kweli anataka kubana matumizi si angekataa ile bajeti Bungeni ya chai maofisini inayomeza mamilioni ya fedha za wakulima? uwezo anao... angepiga stoooop magari serikalini ya Kifahari?

......Asije kesho akatuambia watanzania tuache kutongoza wanawake wazuri kwani ni expensive sana kwa maisha yetu tuliyonayo
icon10.gif
 
...jamani hawa ndio viongozi wetu wanaotuingiza karne ya 21,mbona kazi tunayo!

Hawa ni viongozi waliojitoa muhanga kuijenga nchi hii kwa misingi thabiti ya maadili mema, viongozi walioiletea Tanzania sifa ndani ya Afrika na kwingineko.

Viongozi wanaowaingiza kwenye karne ya 21 mnawajua ni hao wenye mawazo kama yenu nyie mnaoshindwa kuona na kuelewa hata jambo jepesi la kutumia rasilimali za nchi yenu e.g. viwanda vyenu wenyewe ili kuiletea nchi yenu maendeleo badala ya kununua misuti ya bei mbaya kutoka nje! Indonesia aliyoitolea mfano Pinda imepiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kutengeneza na kutumia vinavyozalishwa na viwanda vyao kuliko kupoteza forex kununua vitu kama suti kutoka nchi za nje?

Pinda alikuwa anatoa ushauri na si mwongozo kwamba watu waache kuvaa suti. Kwa hiyo ni juu yetu kuamua kuuponda ushauri huo na kuamua kuendelea kupoteza forex ambazo zingeliweza kutumika kwa mambo mengine muhimu. Mind you, suti inayoingizwa Tanzania hanunuliwi kwa hela za madafu.
 
Acheni domo, tunataka utekelezaji. Tumechoka na usanii wenu. Pinda angejiangalia kwanza yeye kabla ya kurukia wananchi. Baadhi ya wananchi fedha wanazotumia kununua nguo ni zao wenyewe, wamezipata kwa kuuza ng'ombe na korosho. Lakini yeye na Kikwete wanatumia fedha za umma. Kabla ya suti angeangalia safari za nje,msululu wa magari na wapambe wasiokuwa na kazi katika ziara zao za mikoani na nje ya nchi.
 
kuna haja ya kuangalia hivi vitu kwa umakini mkubwa. kitu kinachonishangaza hili la suti ndio amejifunza indonesia au kwa kuwa ni kiongozi anatumia uongozi wake kuongea chochote akiamini kuwa atasikilizwa tu.

sasa tumeanzia kwenye magari ya kifahari wakati tunasubili utekelezaji kwa hamu kubwa, tunazugwa na suti hili likishika moto tutaenda kwenye viatu? hapo bado soksi na pete za gharama za mkononi, Simu za mkononi je? hilo tutaliona tukienda China.

asipoangalia ataamsha hali ya watu kuanza kuvaa suti. Hapa ninamkumbuka Pengo Kuwa anaamsha hasira za watanzania. ni bora akae kimya tu.
 
kuna haja ya kuangalia hivi vitu kwa umakini mkubwa. kitu kinachonishangaza hili la suti ndio amejifunza indonesia au kwa kuwa ni kiongozi anatumia uongozi wake kuongea chochote akiamini kuwa atasikilizwa tu.
sasa tumeanzia kwenye magari ya kifahari wakati tunasubili utekelezaji kwa hamu kubwa, tunazugwa na suti hili likishika moto tutaenda kwenye viatu? hapo bado soksi na pete za gharama za mkononi, Simu za mkononi je? hilo tutaliona tukienda china. Hapa ninamkumbuka Pengo Kuwa anaamsha hasira za watanzania. ni bora akae kimya tu.
 
Nakumbuka Max webber(nafikiri sijakosea jina) katika chambuzi zake, alikuja na idea ya spirity of capitalism , akizungumzia jinsi calvanist walivyoweza kuendelea kwa kuwa walikuwa wabahili- frugal, vitu kama pombe na starehe vilikuwa hawavifanyi na ndio chimbuko la capitalism na maendeleo ya ulimwengu.

Nikiongelea pinda hajakosea kuongelea mavazi na kubana matumizi, mobilization ya resources lazima ianze ndani na kwenye vitu ambavyo tunaweza kuviona vidogo lakini accumulation yake ni kubwa. Leo tukiamua kusupport mavazi yanayozalishwa nchini tutafika mbali,tunachohitaji ni uzalendo wa kweli na siyo ulimbukeni wa mavazi toka nje.

Lingine ni swala la ubora wa mavazi yetu ya ndani, inawezekana watu hawapendi kuvaa mavazi ya ndini kisa tu yanafubaa na kuchujuka upesi.

Nia ya dhati ianze na viongozi wetu, ku-ssuport viwanda na kuvaa mavazi ya ndani.
 
Hapa kuna utani.

Sioni hata chembe ya utani hapa.

These are serious matters! Unavaa suti za hariri wakati unawakilisha masikini wa kutupwa!...rejea wimbo wa MJOMBA usemao..."Sasa tumetenganishwa na ukuta mkubwa mno kati yetu...akimaanisha kwamba JK si mwenzetu kwa sasa!

Lakini pia, hata kwa dhana ya kawaida ya kuenzi vya kwetu iko wapi?

Mbona Nigeria hawahangaiki na masuti ya bei mbaya namna hiyo, wanashona yale maguo yao kwa bazee, ambapo hata rais anavaa?

Anyway...labda ukishakuwa Rais, kila siku kwako ni SHEREHE!
 
I see the circus is creating the intended effect.I can see through it like it is transparent.

mizengomzungu.jpg

Action speaks louder than words Mr. PM. Wewe sio tu unavaa suti, bali unavaa suti kwa style, complete with the last button open and all.

Then unataka watu waache kuvaa suti, for real?
 
Huyu Pinda asitake kuwapangia watu maisha yao. Haya matamshi yake yameanika utupu wa busara zake. Nashangaa hata huo uwaziri mkuu aliupataje.
 
Basi awashonee sare kama za wachina enzi za ukomunist,.. wakiamua njano wote wavae njano, kama nyekundu iwe hivyo hivyo. Duh

Nguo ni utashi wa mtu lakini kama unaenda field shambani au kwenye michezo na suti basi huo ni ulimbukeni na kutowajibika.

Mwenyewe anashangaza, kwani ni mara yake ya kwanza kwenda nje ya nchi? Mbona anashangaa kila kitu!! Kwani inahitaji kwenda kujifunza mpangilio wa mavazi Indonesia au Korea wenye utamaduni tofauti na sisis, kwa nini asiwashangae wamasai wanaovalia shuka mjini mchana kweupe? Hii ni kutokua serious, angeweza kujifunza ya muhimu zaid kwa maendeleo ya nchi.
 
Leo katuni ya KP kwenye Mananchi imenifurahisha sana,mzee anaingia ofisini kwa lubega ya kimasai na baiskeli!Lakini mzee Pind mbona hata hizo land cruiser ni ghari sana,mi nadhani kuanzia sasa mzee awe anatembelea bajaji,alafu kule mkoani Kagera kuna vazi linatengenezwa kutoka magome ya miti linaitwa OLUBUGU,wamshonee Mzee(JK) pensi na mashati ya kuvaa awapo safarini ULAYA!Akiwa bongo huku awe anavaa vest tu inatosha,tupunguze bajeti!

Mzee Pinda acha siasa,anza wewe,'SEMA NO,KWA SUTI pamoja NA BENZI"
Bungeni mwezi wa kumi uingie na pensi tukuone unavyotoa mfano!
 
Back
Top Bottom