Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

Ngida,
sasa anaechekesha zaidi nani? Mimi au wewe?
Soma mwenyewe hapa chini uliyoyaandika!
>Maanake katika yote haya yanayozungumzwa kuhusu mzee wetu Punda<
Sio Punda ni Pinda!
How dare can you call our Prime Minister a donkey???????????
Watch out Ngida!!!

Hi Lampart,
Duh!!!!!!!!!
This is a serious typo. I am really sorry.
I know how hurt you and other patriots are. Please, I apologise for this stupid and silly mistake! Sometimes I am also out of mind - just like Mr Pinda.
I cannot stoop this low and call our own Prime Minister a donkey! This was unitentional and I hope I am forgiven by Mr Pinda himself and by you all.
Next time I will read my posting thoroughly well before submitting it.
Again, sorry guys for the typo.
I do promise that it will NEVER happen again.
I hope Nd. Lampart you have no more excuses to lambast my personality!
 
Wanasema haba na haba. Nadhani hamjatathmini kuwa kuna wizara ngapi na watendaji wangapi wa ngazi ya juu na kati na wa sekta binafsi. Pia mjue sera ya manunuzi inaathiri hapo pia. Hawa mabwana suti zao zinatoka nje na zina gharama na wana zaidi ya 5. Ukiziunganisha hizo suti bongo nzima unapata mini budget ya wizara. Yuko sahihi. Kumbukeni hawa mabwana wanahangaikia micro economya (uchumi wa kaya) so msitegemee atazungumza misamiati adimu.
 
Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.

Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.

Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!

People like these are the main reason we have a PM like Pinda and a president like Kikwete.

Yaani mtu anakuja hapa kujiexpose wazi kabisa kwamba "Pinda wakati wote anazungumza...." that is the problem, not something to be lauded.

Pinda wakati wote anazungumza, hatendi anayozungumza. Hii ni characteristic namba moja ya msanii na mtu asiye makini.

Sasa inaonekana usanii wake huyu Pinda umeshawanasa watu kama huyu Boramaisha, what am I thinking, the names says it all.

That one is Pinda.

This one is Boramaisha.

What do you expect?
 
Niliwahi kusema hapo awali kuwa huyu jamaa hiyo post inampwaya hasa, hajui alitendalo kila siku anaibuka na vigongo vipya halafu vya kishamba vya kujitafutia umaarufu,aende zake huko!!!!
 
Hi Lampart,
Duh!!!!!!!!!
This is a serious typo. I am really sorry.
I know how hurt you and other patriots are. Please, I apologise for this stupid and silly mistake! Sometimes I am also out of mind - just like Mr Pinda.
I cannot stoop this low and call our own Prime Minister a donkey! This was unitentional and I hope I am forgiven by Mr Pinda himself and by you all.
Next time I will read my posting thoroughly well before submitting it.
Again, sorry guys for the typo.
I do promise that it will NEVER happen again.
I hope Nd. Lampart you have no more excuses to lambast my personality!


I feel sure you are forgiven, you seem to be a honest person, unless if you just talk and talk and talk..... without action like Pinda.
 
Inasikitisha sana kuona mtu akienda nje ya nchi tu basi anafikiri kila akionacho huko ni lazima alete bongo hata bila kutumia akili akakaa na kutulia. Ndio matatizo ya watu tuliosoma hapa bongo. Tukitoka nje kidogo basi tunaona kama vile kila kitu tunachokiona ni lazima tukilete home. Hivi huyu jamaa anafikiri hizo nchi za Asia ndio kioo kikubwa kwetu kuliko nchi zingine zote duniani? Hivi kila aendae nje akileta anayoyaona kuimpliment hapa bongo tutakuaje jamani? Kila alikoenda lazima alete maneno ya ajabu tu...kenya,india,indonesia ...arghhhhh!!!!

You are damn right man. Maana hapo Kenya tu kashangaa na kuongea vitu vya ajabu as if hajui kwamba hapa bongo tuna chuo kikuu cha kilimo na agricultural institute za kumwaga tu. Hivi kwanini wanaJF wasiwe wanaprint hii michango ya wadau na kupaste kwenye gazeti moja la weekly watu wakasoma? Nina wasiwasi kwa jinsi internet ya bongo ilivyo na kwikwi viongozi pia hawasomi news ktk net wanasoma printed papers. Tungeprint na hizi comments pia wazione ingekua mwake kabisa.
 
Sasa huu ni kuingilia uhuru wa mtu. Kama ninaweza ku-afford kununua suti, kwa nini nisiivae? PM anatakiwa ku-focus jinsi ya kupunguza matumizi huko serikalini ili kutoa huduma za msingi kwa wananchi.
 
Serikali nayo inatakiwa kuonyesha mfano katika kulitangaza Taifa lake. Kwa misingi hiyo nafikiri Mh. Pinda anatakiwa amshauri bosi wake Rais JK apunguze suti na kuzidisha kuvaa Bhatiki. Haitaji warsha kule Ngurdoto kuhusu mavazi ya Bhatiki. Anaweza ku-google picha za marais wa Nigeria na kujionea mwenyewe kama kweli wako serious about that.
 
Hivi muheshimiwa Rais kwanini usimpe u PM bwana Magufuli ili akusafishie njia kuelekea uchaguzi 2010?Hivi Magufuli anakuwaje mwiba mpaka mmeamua kutokumtumia vizuri na kumficha vichochoroni?
Mkapa alipomaliza ngwe yake alimshukuru sana Magufuli kwa kuifanya serikali yake ing'are na kuahidi kama angeendelea kuwa Rais basi Magufuli angekuwa wapi sijui,labda PM,sasa why not u Mr.President kuitumia hii nafasi kutuletea mabadiliko ya kweli watanzania?
Au unaogopa utendaji wake utakufunika?
 
Nd. Lamaprt,
Wewe ndio wakuzionea huruma mbavu zetu!
Maanake katika yote haya yanayozungumzwa kuhusu mzee wetu Punda wewe umeona huko kuliwa nchi yetu mbele na nyuma ndio kichekesho kikubwa sana!
Ama Watanzania tumekwisha jamani!!!!
Huwezi kumpangia mtu ni kwanini na wakati gani acheke,JK mwenyewe hatuwezi kumpangia. Sasa back to the point wewe hushangazwi na taarifa kwamba kuna fungu maalum la shopping za nguo kwa viongozi?Huoni kuwa maisha yao yamerahisishwa utadhani ni masultani?Rasilimali na pesa vinapoliwa si mbele na nyuma ni nini? Mbele kukiwa dau dogo la vitu kama nguo na nyuma kukifuatiwa na issue kama Kagoda,Kiwira,MEREMETA nk.
Sasa kama huoni hayo we ndo umekwisha.
 
JK amefanikiwa lengo lake, alijua jamaa hakua=wa na mpango hata wa kuwaza kuwa waziri sembuse PM.

Hii ni kuwa Pinda bado anaweweseka na cheo hicho!

usije ukakuta mpak atakavyoondoka madarakani akaendelea kufikiri yee ni PM

Viatu vikubwa hivi!!
 
Wajameni!!???, mi nna swali moja...what's up with hawa viongozi wetu??!!!, this's what I call "BIZZARE"
Just the other day, tumewekewa hapa speeches za our dear presidaa kuhusu watoto wa shule waliojifungua kuingia madarasani na matiti kuchuruzika, mara he wants to make Mwanza be like California, haya na sasa his Prime Minister says this...TUTAFIKA KWELI??!!!, GOD HELP US!
Mr. Prime Minister If you don't have to say anything, I have one word for you...."shut up"
 
Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.

hizi pumba zingine zinatisha, hivi kuishi na wazungu ni bahati nzuri?

 
Utakuta kuna viongozi shopping ya suit anaenda kununua US hawa ndo wakunyoshewa vidole mtu anavaa suit ya mil.2 piga hesabu anazo kama 30 hivi na wananchi tunataabika hakuna madawa mashule ndo kama hivyo watoto wanakaa chini huu ufahari wa nn?
 
Utakuta kuna viongozi shopping ya suit anaenda kununua US hawa ndo wakunyoshewa vidole mtu anavaa suit ya mil.2 piga hesabu anazo kama 30 hivi na wananchi tunataabika hakuna madawa mashule ndo kama hivyo watoto wanakaa chini huu ufahari wa nn?

Milioni mbili Usdola au Tz shilingiz ? Maana kama ni Shiling basi ni kawaida tu hata mabrazamen na masister du wa kibongo huko maulaya ni kawaida kuvaa mavazi yanafikia au kupita mbali ya matumizi mingine ya showing nami ninazo.

Ila Pinda bado anaonekana ana siasa za ujamaa na kujitegemea.
 
Pinda ashauriwa aanze kumshauri Kikwete kuhusu suti za gharama

Na Waandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwahamasisha viongozi ndani ya serikali akianzia na bosi wake Rais Jakaya Kikwete, aache kuvaa suti za gharama kubwa kutoka Ulaya na Marekani, badala yake wavae nguo za viwanda vya ndani, iwapo ana nia ya dhati ya kuikomboa jamii kiuchumi.

Juzi Waziri Mkuu ,Pinda alitoa kauli kuwataka Watanzania kuepuka kuvaa mavazi ya gharama kubwa ikiwemo suti, akieleza kuwa halizifai kwa nchi maskini kama Tanzania. Aidha alirejea kauli yake ya kupinga matumizi ya magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine wa serikali.

“Mtu ambaye anaongoza kwa kuwakoga watanzania kwa kuvaa suti za bei mbaya, ni Rais Jakaya Kikwete ambaye anavaa suti za hariri kutoka nchi za Ulaya na Marekani,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:

“Kiongozi ni kioo cha jamii, sasa kama Pinda ana nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania, kwanza aanze na bosi wake Rais Kikwete ili aonyeshe mfano kwa kuvaa nguo zinazotengenezwa na viwanda vyetu vya Urafiki na KTM”.

Mbali na Lipumba, Naye Mbunge wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa (Chadema), aliungana na kiongozi huyo wa CUF kupinga kauli hiyo akisema inashangaza na kuonyesha wazi udhaifu wa serikali ya awamu ya nne katika kufanya maamuzi.

Dk. Slaa aliyasema hayo jana akiwa mjni Arusha anakohudhuria mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA).

Alihoji ,' Kama Pinda ambaye ni kiongozi mkuu serikalini analalamika kuhusu hali hiyo, Mtanzanzania wa kawaida atafanya nini?

“Kama yeye Waziri Mkuu ambaye ni mtendaji analalamika, mimi Dk Slaa nifanye nini,” alihoji mbunge huyo machachari wa kambi ya upinzani ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema.

Alimtaka Waziri Mkuu kuwa mkali katika kusimamia maadili mema kwa walio chini yake badala ya kulalamika kwenye majukwaa.

Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu, alisema tamko la Waziri Mkuu ni zuri na linaonyesha wazi mkakati wa serikali ya awamu ya nne katika kupunguza gharama ambazo zinaweza kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii.

“Jambo la msingi hapa ni kwa watendaji wote kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu na kuyaingiza katika utekelezaji matamko ya Waziri Mkuu bila kusukumwa,” alisema Zungu.

Mbunge wa viti maalumu, Anna Abdallah licha ya kuunga mkono kauli ya Pinda, alishauri uwepo utaratibu maalumu wa mavazi ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi na hata watendaji serikalini.

Kwa upande wake, Balozi mstaafu ,Job Lusinde naye aliunga mkono kauli ya Pinda na kusema kuwa kiongozi huyo yuko sahihi.

Pinda alitolea mfano wa nchi ya Indonesia ambako wameamua kubana matumizi kulingana na uchumi wa nchi hiyo na kwamba hivi sasa hata rais wao ameamua kutumia vazi la kitambaa aina ya batiki kinachotengenezwa nchini humo.

Akizungumzia kauli hiyo ya Pinda jana, Lusinde alisema kuwa hata yeye amekuwa akiwashangaa viongozi wengi wanapofanya ziara zao kwenda mashambani wakiwa wamevalia vazi hilo la nchi za Magharibi, jambo alilolielezea kuwa ni kichekesho.

Alisema hata yeye wakati akiwa kiiongozi, hakupenda kuvaa suti mara zote na alikuwa haoni umuhimu wa kuvaa suti wakati kiongozi wake Hayati Baba wa Taifa akiwa na mavazi ya kawaida.

Lusinde alisema "katika kipindi cha utawala wa Nyerere hata wakati nakwenda kujitambulisha katika nchi nilizowahi kuwa balozi, nilikuwa katika vazi la ’Chu Eng-Lai’ ambalo kwa wakati huo lilikuwa kama vazi rasmi lililotoholewa kutoka China na hata picha zangu zote ukiziona utakuta niko katika vazi hilo kwa kulinda na kuenzi utamaduni wa Mtanzania” Imeandikwa na Salim Said, Leon Bahati, Arusha na Habel Chidawali, Dodoma
 
Bora Maisha umeona comments za wanazuoni hizo kuhusu kauli ya waziri mkuu wako Pinda
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom