Pinda sasa ageukia mavazi awataka Watanzania kuachana na suti

..nadhani Pinda alimaanisha kwamba,kwa kiongozi anaetumia muda wake mwingi kuwaza na kupanga namna ya kuwaondoa watz kwenye umaskini walio nao, hana muda wa kuwaza habari za suti! utakuaje wewe kiongozi uko smart ilhali wale unaowaongoza wana midabwada??wakati wao kodi yao ndo inakupa huo ufahari??

Ni suala la kutumia common sense tu, namna ya kuco-ope na watu wa chini, ambao hawana uhakika na mustakabali wao kwa ujumla.
 
..nadhani Pinda alimaanisha kwamba,kwa kiongozi anaetumia muda wake mwingi kuwaza na kupanga namna ya kuwaondoa watz kwenye umaskini walio nao, hana muda wa kuwaza habari za suti! utakuaje wewe kiongozi uko smart ilhali wale unaowaongoza wana midabwada??wakati wao kodi yao ndo inakupa huo ufahari??

Ni suala la kutumia common sense tu, namna ya kuco-ope na watu wa chini, ambao hawana uhakika na mustakabali wao kwa ujumla.

Nimeuliza hapo juu, yeye kafanya nini to this end? Maneno matupu hayavunji mfupa waswahili walisema.
 
Kama nakumbuka vizuri wakati wa Budget ya 2009, State house wamepewa fungu la mavazi & viburudisho, mapesa mengi tuu

Mkuu tell me youre not serious, kwanini wasinunue hayo mavazi kwa mishahara yao? Hii ni kali ya mwaka,yani kuna fungu la mavazi na viburudisho specially kwa viongozi?

Kweli nchi inaliwa mbele na nyuma, no wonder Rev. Kishoka kasema huu ni "Ukahaba"
 
Baada ya kutamani wananchi wavae vizuri unazidi kuwadidimiza wavae rubega ili ukija upepo upige chabo ,ndio maana yake !!! Hapa namshangaa sana Waziri wetu huyu tena Mkuu ,jamani hivi huyu mkuu hii ndio safari yake ya kwanza ughaibuni ? Tena kwenye mashamba ya mpunga ? Yaani anatuletea habari za vijijini ,Mheshimiwa pigana na rushwa hapa nchini hayo ya mavazi naona hatujafikia.Au ndio unawapiga dongo msafara wa Kikwete ,wambie waondoke hapa wamevaa mashati ya vitenge na viatu vya matairi.
 
Inasikitisha sana kuona mtu akienda nje ya nchi tu basi anafikiri kila akionacho huko ni lazima alete bongo hata bila kutumia akili akakaa na kutulia. Ndio matatizo ya watu tuliosoma hapa bongo. Tukitoka nje kidogo basi tunaona kama vile kila kitu tunachokiona ni lazima tukilete home. Hivi huyu jamaa anafikiri hizo nchi za Asia ndio kioo kikubwa kwetu kuliko nchi zingine zote duniani? Hivi kila aendae nje akileta anayoyaona kuimpliment hapa bongo tutakuaje jamani? Kila alikoenda lazima alete maneno ya ajabu tu...kenya,india,indonesia ...arghhhhh!!!!
ni kweli mkuu huyu jamaa anaboa sasa,maana juzi katoa ya vx leo suti ,kesho,keshokutwa itakuaje mpaka atasema tule vyura na nyoka na minyoo badala ya kununua nyama,na hiyo nadhani ni safari yake ya pili kutoka.akisafiri tena kama mara kumi nadhani atarudi na story kama hizi mpaka tutakoma,na sasa nimeelewa kwanini vasco da gama anaenda yeye tu viwanja maana naona kaona huyu mtoto wa mkulima atamuaibisha maana ukulima wake mwisho,kawababaikia wachina mpaka kawagawia ardhi kwa mkopo sasa anakuja na story zisizoeleweka,hawa ndio viongozi wetu hawa
 
Hapa pm amechemka sana- suti zipo hata za mchikichini -Ilala kwa beo poa kuliko hata hili shati la Indonesia.
Hata umasikini wetu usipimwe kwenye mavazi.
Nitakuja na vigezo vy kipimo cha umasikini
natoa hoja.
 
Tunahitaji PM urbanite ambaye anajua maisha ya watu wa vijijini na wakati huo huo kashazunguka viwanja kabla ya kuwa PM.

Huyu Pinda anakuwa kama hajawahi kutoka bongo ndiyo kwanza anaanza kusafiri baada ya kuwa PM bwana.
 
Bwana Pinda aachae upumba huo.If so amwambie Kikwete avae Kanzu au Batiki,tuone itakuwaje!Mambo ya Kaunda Suti na Chuo En Lai suti ni ya kikoministi!Hata wa China wameacha mavazi hayo!
Azungumzie mambo ya muhimu ,sio uchwara huu
 
Mimi huwashangaa sana watu wanaopenda kuniga tai kwenye nchi yenye joto kama hii yetu. Kwanza ni ushamba wa hali ya juu. Wazungu walibuni vazi hilo kutokana na hali ya hewa ya nchi zao ambako karibu mwaka mzima hali ya hewa ni baridi kali mno isiyoweza kueleweka kwa mtu anayeishi kwenye joto kama hapa kwetu. Sie Waafrika kwa kupenda kuiga mambo ya Ulaya na kudhani kwamba ndio maendeleo tunajikuta tunajitesa na suti. Si hilo tu, mtu akiniga hiyo suti ili kukimbia joto atahakikisha anakuwa na gari airconditioned na ofisi airconditioned etc. Matokeo yake anatumia fedha nyingi mno kugharimia manunuzi ya suti, gari airconditioned ambalo hutumia mafuta mengi kuliko kawaida, na huko ofisini atataka airconditioner inayotumia umeme mwingi. Mwisho wa yote ili kuweza kuzimudu gharama zote hizo itabidi mtu/afisa huyo ajiingize kwenye hujuma za rushwa na ufisadi ili aweze kulipia gharama hizo.

Kwa bahati nzuri nimewahi kuishi na Wazungu wanatucheka na kutudharau sana kwa tabia yetu ya kuiga mambo yao ambayo wala hayana mantiki kwetu sisi katika hali yetu ya umaskini.

Asante Pinda! Usife moyo, endelea, kazana kuwaelimisha wananchi na tunakuomba utumie rungu lako la Uwaziri Mkuu kusitisha mianya yote ya ubadhilifu ndani ya Serikali. Mungu atakuwa pamoja nawe!
hapana mkuu hapa nakataa sidhani kama watu huko bongo huvaa suti kila siku?mara nyingi nimeona watu kuvaa suti maranyingi kunapokua na matukio muhimu yanayohitaji unadhifu,au mtu anaelekea ofisini na ana semina au mkutano na hata siku mojamoja unavaa tu kazini au hata kutoka sio mbaya,watu watavaa mabatiki kila siku?

Hata yeye mwenyewe alipoenda kushonesha hilo batiki lake huko indonesia kaiga tu na wogawoga wake wa kufagilia viongozi wenzake, angeenda na suti, shati linen, klimplin au hata khaki poa tu kimpango wake,badala aje na mambo ya maendeleo aliyoyaona huko ndo kwanza anatuletea story ya vibajaj na suti huyu jamaa mwehu kama kigogo alivyosema inabidi wamcheki mukichwa
 
Kuna kitu kimoja waziri mkuu ningependa unijulishe, hivi wabunge wa Malaysia, India wanalipwa kiasi gani? Na kipato chao kinaendaje na kipato cha mtu wa kawaida?
 
10/1/2009
Pinda ashauriwa aanze kumshauri Kikwete kuhusu suti za gharama
Na Waandishi wetu
Mwananchi


MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, amemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwahamasisha viongozi ndani ya serikali akianzia na bosi wake Rais Jakaya Kikwete, aache kuvaa suti za gharama kubwa kutoka Ulaya na Marekani, badala yake wavae nguo za viwanda vya ndani, iwapo ana nia ya dhati ya kuikomboa jamii kiuchumi.

Juzi Waziri Mkuu ,Pinda alitoa kauli kuwataka Watanzania kuepuka kuvaa mavazi ya gharama kubwa ikiwemo suti, akieleza kuwa halizifai kwa nchi maskini kama Tanzania. Aidha alirejea kauli yake ya kupinga matumizi ya magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine wa serikali.

“Mtu ambaye anaongoza kwa kuwakoga watanzania kwa kuvaa suti za bei mbaya, ni Rais Jakaya Kikwete ambaye anavaa suti za hariri kutoka nchi za Ulaya na Marekani,” alisema Profesa Lipumba na kuongeza:

“Kiongozi ni kioo cha jamii, sasa kama Pinda ana nia ya dhati ya kuwakomboa watanzania, kwanza aanze na bosi wake Rais Kikwete ili aonyeshe mfano kwa kuvaa nguo zinazotengenezwa na viwanda vyetu vya Urafiki na KTM”.

Mbali na Lipumba, Naye Mbunge wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa (Chadema), aliungana na kiongozi huyo wa CUF kupinga kauli hiyo akisema inashangaza na kuonyesha wazi udhaifu wa serikali ya awamu ya nne katika kufanya maamuzi.

Dk. Slaa aliyasema hayo jana akiwa mjni Arusha anakohudhuria mkutano wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA).

Alihoji ,' Kama Pinda ambaye ni kiongozi mkuu serikalini analalamika kuhusu hali hiyo, Mtanzanzania wa kawaida atafanya nini?

“Kama yeye Waziri Mkuu ambaye ni mtendaji analalamika, mimi Dk Slaa nifanye nini,” alihoji mbunge huyo machachari wa kambi ya upinzani ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema.

Alimtaka Waziri Mkuu kuwa mkali katika kusimamia maadili mema kwa walio chini yake badala ya kulalamika kwenye majukwaa.

Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu, alisema tamko la Waziri Mkuu ni zuri na linaonyesha wazi mkakati wa serikali ya awamu ya nne katika kupunguza gharama ambazo zinaweza kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii.

“Jambo la msingi hapa ni kwa watendaji wote kila mmoja kwa nafasi yake kutimiza wajibu na kuyaingiza katika utekelezaji matamko ya Waziri Mkuu bila kusukumwa,” alisema Zungu.

Mbunge wa viti maalumu, Anna Abdallah licha ya kuunga mkono kauli ya Pinda, alishauri uwepo utaratibu maalumu wa mavazi ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi na hata watendaji serikalini.

Kwa upande wake, Balozi mstaafu ,Job Lusinde naye aliunga mkono kauli ya Pinda na kusema kuwa kiongozi huyo yuko sahihi.

Pinda alitolea mfano wa nchi ya Indonesia ambako wameamua kubana matumizi kulingana na uchumi wa nchi hiyo na kwamba hivi sasa hata rais wao ameamua kutumia vazi la kitambaa aina ya batiki kinachotengenezwa nchini humo.

Akizungumzia kauli hiyo ya Pinda jana, Lusinde alisema kuwa hata yeye amekuwa akiwashangaa viongozi wengi wanapofanya ziara zao kwenda mashambani wakiwa wamevalia vazi hilo la nchi za Magharibi, jambo alilolielezea kuwa ni kichekesho.

Alisema hata yeye wakati akiwa kiiongozi, hakupenda kuvaa suti mara zote na alikuwa haoni umuhimu wa kuvaa suti wakati kiongozi wake Hayati Baba wa Taifa akiwa na mavazi ya kawaida.

Lusinde alisema "katika kipindi cha utawala wa Nyerere hata wakati nakwenda kujitambulisha katika nchi nilizowahi kuwa balozi, nilikuwa katika vazi la ’Chu Eng-Lai’ ambalo kwa wakati huo lilikuwa kama vazi rasmi lililotoholewa kutoka China na hata picha zangu zote ukiziona utakuta niko katika vazi hilo kwa kulinda na kuenzi utamaduni wa Mtanzania” Imeandikwa na Salim Said, Leon Bahati, Arusha na Habel Chidawali, Dodoma
 
Nilikuwa nalifikiria hili pia.

Huyu Pinda anajisemea ovyo kiasi kwamba watu wengine wanaweza kutafsiri kwamba anafanya insubordination hata kwa bosi wake Kikwete anayependa kuvaa misuti ya bei mbaya.

Loose lips sink ships.
 
Lusinde alisema "katika kipindi cha utawala wa Nyerere hata wakati nakwenda kujitambulisha katika nchi nilizowahi kuwa balozi, nilikuwa katika vazi la 'Chu Eng-Lai' ambalo kwa wakati huo lilikuwa kama vazi rasmi lililotoholewa kutoka China na hata picha zangu zote ukiziona utakuta niko katika vazi hilo kwa kulinda na kuenzi utamaduni wa Mtanzania" Imeandikwa na Salim Said, Leon Bahati, Arusha na Habel Chidawali, Dodoma
vazi la chu Eng_lai linauenzi vipi utamaduni wa mwafrika wakati limebuniwa china?mi naona ni yaleyale ya kupinda
 
Mbunge wa viti maalumu, Anna Abdallah licha ya kuunga mkono kauli ya Pinda, alishauri uwepo utaratibu maalumu wa mavazi ili kuepusha mkanganyiko kwa wananchi na hata watendaji serikalini.

Kwa upande wake, Balozi mstaafu ,Job Lusinde naye aliunga mkono kauli ya Pinda na kusema kuwa kiongozi huyo yuko sahihi.

...jamani hawa ndio viongozi wetu wanaotuingiza karne ya 21,mbona kazi tunayo!
 
...jamani hawa ndio viongozi wetu wanaotuingiza karne ya 21,mbona kazi tunayo!

I say, tuacheni utani mwengine wowote ule. Haya ya Pinda yanakatisha tamaa.
Doooooooooooooooooooooooo!!!!
Hivyo tutafika kweli jamani????????
Is this guy in his proper senses??????????
JK alimpata wapi huyu jamaa???????????
 
<utakuaje wewe kiongozi uko smart ilhali wale unaowaongoza wana midabwada??>

You can also put it this way: utakuaje wewe kiongozi umeshiba ilhali wale unaowaongoza wananjaa??
 
Mkuu tell me youre not serious,kwanini wasinunue hayo mawvazi kwa mishahara yao?Hii ni kali ya mwaka,yani kuna fungu la mavazi na viburudisho specially kwa viongozi?Kweli nchi inaliwa mbele na nyuma,no wonder Rev.Kishoka kasema huu ni "Ukahaba"


JMushi1,
>Kweli nchi inaliwa mbele na nyuma<

Please, zionee huruma mbavu zetu!!!
 
JMushi1,
>Kweli nchi inaliwa mbele na nyuma<

Please, zionee huruma mbavu zetu!!!

Nd. Lamaprt,
Wewe ndio wakuzionea huruma mbavu zetu!
Maanake katika yote haya yanayozungumzwa kuhusu mzee wetu Punda wewe umeona huko kuliwa nchi yetu mbele na nyuma ndio kichekesho kikubwa sana!
Ama Watanzania tumekwisha jamani!!!!
 
Nd. Lamaprt,
Wewe ndio wakuzionea huruma mbavu zetu!
Maanake katika yote haya yanayozungumzwa kuhusu mzee wetu Punda wewe umeona huko kuliwa nchi yetu mbele na nyuma ndio kichekesho kikubwa sana!
Ama Watanzania tumekwisha jamani!!!!

Ngida,
sasa anaechekesha zaidi nani? Mimi au wewe?
Soma mwenyewe hapa chini uliyoyaandika!
>Maanake katika yote haya yanayozungumzwa kuhusu mzee wetu Punda<
Sio Punda ni Pinda!
How dare can you call our Prime Minister a donkey???????????
Watch out Ngida!!!
 
Back
Top Bottom