PINDA - Nitatoa Maamuzi yote Jumatatu

Jairo alimpa fundisho, hawezi kurudia kosa hilo tena kwa hawa wanaolazimishwa kujiuzulu.
 
hili Pinda mi nishasema kuwa ni linafiki na liongo.....mi sitegemei chochote toka kwa hili jamaa hiyo jtatu.....mbona watu hawajamsoma Pinda????.....watu walitakiwa wamjue tangu sakata la Jairo na pia lile la madaktari.....Pinda hana nguvu kama PM....hata madaktari walimyumbisha ije iwe mawaziri???.....huyu ameonyesha failure ya hali ya juu....hatujawa kuwa na PM bogus kama huyu TZ......
 
Zitto alisema neno nzuri sana na la maana "ACCOUNTABILITY"

Serikali ya Kikwete ina miss accontability

Let them go to hell this way, M4C inachanja mbuga kama haina breki
 
changa la macho,ngoja nifungashe virago niwaachie li inchi lenu bwana loh!
Bora nikawe paka mwizi kwenye nchi za wenzetu kuliko kua binadamu bongo.
 
Akihojiwa na waandishi wa habari amedai kwamba hajapokea barua toka kwa waziri yeyote
anaweza kuwa sahihi. inategemea maamuzi gani magumu ccm walifikia. kama waliambiwa waandike barua za kujiuzulu sidhani kama wangeziandika ucku na kumpelekea hotelini/nyumbani kwake ucku huohuo..
 
Kwanini Pinda mwenyewe asing'oke maana alishindwa kuwawajibisha wa Richmond na waliomsafisha Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini sasa anasubiri nini mimi namshauri kwa vile wabunge baadhi wameonyesha kutokuwa na imani naye kwa heshima yake angeamua kujitoa hata kama Raisi akatae maana watu kutokuwa na imani na wewe ni kazi ngumu kuelezea umma wakuelewe na uzuri hana cha kukosa maana atapewa ulinzi maisha yake yote kwani amefanya kazi kama waziri mkuu.

Na pia aseme kwanini ameamua kuchukua uamuzi kama ataamua kujiuzulu na pia maamuzi mengi yameonesha hana uwezo wa kumshawishi Raisi afuate anachokiamini na muda mwingi Raisi anafanya tofauti mfano sakata la Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini isingekuwa bunge leo hii Katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini angekuwa kazini na pia Katibu mkuu kiongozi aliachwa mpaka akastaafu je yeye anatekeleza kipi kinachoagizwa na bunge kama mtendaji mkuu wa serikali.

Ushauri

Ni bora aachie madaraka na wajaribu wengine na amezunguka nchi nzima hakuna aliyeagiza achukuliwe hatua ambapo mpaka sasa amefanyiwa hivyo kwa hiyo hana uwezo wa kuwajibisha waliochini yake na mara nyingi kwa maswali ya papo kwa hapo hakuna agizo ambalo analoweza sema limetekelezwa mfano sakata la korosho malipo/sakata la korosho wanunuzi/sakata la wauzaji wa mafuta/sakata la madaktari katika mgomo/sakata la pembejeo za kilimo, kwa hiyo na aamue maana hana uwezo wa kuwawajibisha wanaotuhumiwa kuanzia wakurugenzi/wakuu wa wilaya/wakuu wa mikoa/ viongozi wengi wanaoonekana wanawanyanyasa wananchi
 
Wa TZ kazi tunayo, mi nafikiri anamsubiri bwana mkubwa aje aongee na wazee wa CCM Dar kuhusu hilo kwani maamuzi magumu ya serikali hutolewa kwa Wazee wale
 
Mtu mmoja aliwahi kuuliza huko nyuma, "hivi watanzania ni nani aliyeturoga"? Hivi kweli kutegemea Ccm "wawajibishane" badala ya "kulindana" ni nini Kama siyo kurogwa??
 
Sinema inaendelea sijui itakuwa episode ya ngapi
Na picha lenyewe limefikia patamu maana sterling hataki kuuwawa japo waandaji wa picha wanahitaji afe

Tujiulize ni nani na lini huo utamaduni wa kujiuzulu umeanza Tanzania
Kwa culture ipi wameanza lini kuwa na uwajibikaji wa kihivyo
hao wote waliotajwa na wizara zao na kashfa zao ukiwauliza mawaziri wote watakana na miungu yao kuwa hawajui lolote as if hizo wizara au maamuzi yanatolewa na watu wengine ambao sio wao na wao wako pale kama sanamu tuu]
Hawajaona kosa mpaka sasa hivi la kuwafanya wachukue maamuzi hayo
Hiyo wanasema ni report ya akina Zito na wenzake haziwahusu
Wao ni watendaji tuu kwa hiyo madudu yakifanyika kwenye wizara zao hawahusiki na hawawezi kuwajibika kwa makosa ya wengine japo yamefanyika kwenye wizara zao
Utamaduni wa kuachia ngazi bado sana
Na unapofanya kosa ukategemea busara za aliyekuteua kukuambia aaaahhh bana jiuzulu bila wewe kuwa na utashi huo au kuona kosa lako na kujikubali tusitegemee la ajabu hapo
Kungekuwa na dhana ya kuwajibika hata kw amakosa ambayo yamefanywa na watendaji wa wizara yake wala isingechukua muda tuhuma zipo na zimethibitishwa andioka barua ya kujiuzulu aliyekuteua aikuute mezani kwake na wakati huo wewe haupo wizarani
 
changa la macho,ngoja nifungashe virago niwaachie li inchi lenu bwana loh!
Bora nikawe paka mwizi kwenye nchi za wenzetu kuliko kua binadamu bongo.

materialz za kutengenezea paspot zimeisha,cjui una habari?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom