Pinda na umiliki wa Sumry Express

Status
Not open for further replies.
CCM kwa sasa kila mtu anakwiba cha msingi uwe na mtu wa kukukingia kifua
 
Sikusema SUMRY EXP imeanza baada Handsome Pinda kupewa u-PM, wala sikusema amejenga Uwanja wa Ndege Mpanda kwa pesa yake lakini swala linakuja hivi vyote vimekuja fasta mara baada ya yeye kuingia kuwa PM, hapo sijazungumzia kuhusu kuanzisha mkoa wa KATAVI maana hata bibi kiroboto alipewa wake wa NJOMBE so ni suala la kupeana hata Sumaye alijimegea MANYARA huenda NDESAMBURO akiwa PM nae akajipatia mkoa mpya wa KIBOROLONI. Mimi binafsi naamini kwenye usawa maana kwa nini iwe RUKWA?MPANDA tena baada ya yeye kuwa PM? na sio mikoa mingine? kwenye hayo mabasi ya SUMRY nakubaliana na nyie ushahidi nitatoa kesho saa 5 asubuhi pale Maelezo Dar es Salaam, samora Avenue. nimeshafanya Booking ya kupata nafasi muda huo. karibuni nyote. Watanzania tuzinduke tusianze kumlaumu mtoa mada kesho nikitoa ushahidi ninyi makada sijui mtaficha siri hiyo wapi. KWA STYLE HII YA MAJADILIANO HUMU NIMEGUNDUA ni kazi rahisi sana kuwaibia watanzania na wasishtuke.

Wewe naona una kawivu fulani. Mbona useseme hata Cleopa Msuya aliibadilisha Mwanga hata kule milimani kabisa nguzo za umeme zimepita? Bora viongozi hao wanaleta maendeleo ya jamii kuliko akina Lowasa waliokutuma kumchafua Pinda wanakula na familia zao na mafidadi wenzao. Halafu usithubutu hata kidogo kumlinganisha Mzee Ndesamburo na mafisadi maana hadi sasa anatumia hela zake kulifanya jimbo la Moshi Mjini kuwa ulaya ndogo kwa usafi. Huna habari kuna wajuembe toka nchi za kusini walienda moshi kujifunza jinsi ambavyo ameweza kuufanya mji ule kuwa msafi? At the same time posho yake ya ubunge alitumia kukarabati Motuary ya Mawenzi na vitanda vya wagonjwa. He had done so many progressive issues for the benefit of the community. Sasa Basi hicho kiwanja na ndege na barabara Rukwa ni kwa matumizi ya Pinda pekee au jamii nzima hata na wewe? Nilienda Rukwa miaka ya 90 na 2000s hakuna barabara!!! na maendeleo duni!!! Sasa unataka iendelee kubaki hivyo maskini hadi lini? Tunachotaka Tanzania kwa sasa ni even development Mkuu na siyo kuendelea kubaki na mikoa ya pembezoni. Sasa na kule kusini ambako kuna wamegundua madini, gas na mafuta na uelekezo wa miundombinu unaanza sasa nako utasemaje? Au unataka bado wamakonde waendelee kuwa walinzi wa majumba yenu Dar halafu mwishowe wanawafukuza wamiliki na wanaendelea kukaa kwenye pagala milele na wewe kwishey!!! Amka mkuu!! Do not be myopic!!!
 
Samahani, hivi Yule bibi kiroboto kule mjengoni anadaiwa kumiliki mabasi gani vile? Naomba kukumbushwa

Huyu bibi kiroboto ndio fisadi babu kubwa sio anamiliki mabasi tu ya SUPA VEO bali hata hotel kubwa pale Njombe na maflat mengi tu hapa Dar!! Ndio maana hatagombea ubunge 2015 ameiba vya kutosha!!!
 
Ni vyema tukiangalia na vyanzo vya taarifa kabla ya kupost, kama huna ushahidi wowote ule (plain as it is). Ni "Majungu" in "umbeya" out"
 
Mhhh fitina,chuki,majungu havileti maendeleo,kama wewe una uhakika na unachikisema lete ushahidi kamilifu tofauti na hapo utakuwa mmbeya tuu.
 
Kale Kazee hakawezi kuwa na mali ya kifisadi Ni mwanafunzi mzuri sana wa late Jk, labda awe amejifunza kwa Gvment hii.

Hayo mabasi sina uhakika kama pm anayamiliki nachojua ana hisa kwenye kampuni moja ya kutengeneza mbegu za mazao jijini Mbeya
 
yale ni tajiri mmoja anaitwa supar feo wa songea japo inasemekana na mama Makinda ana mkono wake.!
Kama kwa Pinda mmekataa kwamba haiwezekani na wewe toa uthibitisho wa mama Makinda kuwa na mkono kwenye hilo,Make
 
. kama wamehama ndio vizuri kuwataja sasa, lakini kwasababu ni watu wakubuni huta wataja.. Uanzishe biashara ya ku export majungu na uzushi, Labda hicho kitakusaidia lakini sio kazi unayoifanya sasa. la sivyo hizo ni POROJO, na tutazidharau na kuziacha hapa hapa[/QUOTE
Alfred Ngowi sijui kama ni real name au ni ID 20 nimesoma ubishi wako humu naona kama vile una maslahi binafsi,na pia aina fulani ya ubishi amba hauwezi kumtofautisha na mtu ambaye hakwenda shule,mjinga fulani yaani ubishi wako hauna point yenye mashiko unabisha tu ilimradi unajua kufungua jf na kuanza kuongea
Unachokikataa hapo ni nini? Wewe ni mke wa Pinda unajua kila kitu alichonachp? Au unabisha tu uonekane upo? Ifikie sehemu heshimu anachosema mtu na chanzo chake cha habari,unataka awataje ili uwafanye nini we kapuku? Walioficha tu pesa Uswiss hawajatajwa sembuse hao waliosema Pinda anamiliki Sumry acha ubishi wa kipumbavu kuna watu na akili zao wanaosoma jf
 
Last edited by a moderator:
Bibi Kiroboto anasadikiwa kuw ana mkinga mwenzie kwenye kampuni ya SUPER FEO
 
acheni majungu wakubwa,mnataka pinda afe masikini?

huu ni wakati wa mavuno,akitoka hapo kushinei,kiinua mgongo hakitoshi japo atalishwa na govment mpaka mwisho wa uhai wake lakini lazima naye awe ameshajiandalia kamradi kake.

ingekuwa enzi ya mwalimu hapo sawa lakini sasa hivi ni Chukua Chako Mapemaaaaaaaaa,(CCM).kaeni mkilalama wenzenu wanaingiza fyeza.
 
Wanajmvi huyu jamaa kwa nje anaonekana msafi kiundani ni mchafu kupitiliza toka aukwae u-PM amekomaa kuchota pesa zetu na kuzipeleka kwenye SUMRY EXPRESS na sasa wameona kama wanashtukiwa wamenunua kampuni ya MBEYA EXPRESS kupotezea. Hebu cheki ule Uwanja wa ndege MPANDA ulivyotengenezwa fasta. Pia, alitaka Yambesi awe Katibu mkuu kiongozi kwa sababu wanatoka wote RUKWA mzee Luhanjo akamzidi kete kwa kumpendekeza best yake mzee OMBENI. Kuweni makini na huyu mtu nje anajifanya anamwaga chozi kumbe fisadi kiaina. Zaidi anajidai anapigia debe kilimo kwanza kumbe ndo anapofisadi kuanzia Matreka,Mbolea etc.......MKUU TUMEKUSHTUKIA


Sio kweli kabisa. Hii habari ya uzushi. Sumry express ni kampuni iliyoanzishwa na mmoja wa watoto wa Mzee sumry anayeitwa Humudi. huyu humudi alikopshwa mtaji wa mabasi 2 na mjomba wake anayeishi Mombasa ambaye ni tajiri mkubwa jijini humo na ana kampuni ya mabasi. mkataba ulikuwa akilipa deni hilo anamwongeza mabasi mengine mawili kitu ambacho jamaa alifanikiwa kufanya. kampuni imekuwa ikikua kwa mtindo huo mpaka mabasi yalipofika kumi jamaa biashara ikamzidi na akaifanya ya familia ndugu wote wakishirikiana kuendesha biashara. Baadae wakahamia sumbawanga mjini (wakitokea Laela, kama kilometre 80 hivi kutoka s'wanga). Na kabla ya mabasi familia hii ilikuwa inaendesha biashara ya hoteli mji mdogo wa tunduma, biashara ambayo ilikuwa imeshamiri sana. Mizengo pinda anapoukwaa uwaziri mkuu tayari sumri ni kampuni kubwa kabisa kiasi kwamba haikuhitaji hata hela za mizengo pinda. Tena kipindi hiki ambacho wewe unadai kampuni ni ya mizengo pinda ndicho kipindi ambacho kampuni imeyumba sana kwa ajili ya madeni ya mikopo waliyochukua bank baada ya kukwaruzana na mjomba wao wa mombasa. Kama mizengo pinda ni mwizi, pesa zake haweki sumry, mimi nimekuwa na hawa jamaa na najua biashara zao vizuri sana. Wakati sumaye akiwa waziri mkuu, ushatokea uvumi kama huu wa kwako wa Sumry ni Sumaye na waziri gani mwingine sijui. Tuache uzushi, tusiwapotoshe watanzania. Ukitaka details zaidi kuhusu sumry, kama unazihitaji sana, nitafute. Ila la msingi uzushi acha kabisaaaaa!!! Ni kansa hiyo!!
 
"alitaka Yambesi awe Katibu mkuu kiongozi kwa sababu wanatoka wote RUKWA mzee Luhanjo akamzidi kete kwa kumpendekeza best yake mzee OMBENI"

Alas! Kumbe vyeo watu wanapeana kwa kujuana? Kwa hiyo mimi nikiacha udereva wa boda boda nampa kazi rafiki yangu bila kujali kama anajua kuendesha au la! Tumesubutu! Tumeweza!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom