Kama ningekua ndie Rais Jakaya Mrisho Kikwete basi nisingesita hata punje kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kuangalia uwezekano wa kumwajibisha Spika Anna Makinda! Ningefanya hivyo kufuatia taarifa iliyotolewa na Ikulu hapo jana! Kwamba, Mheshimiwa Rais hakupandisha posho bali aliwaambia watumie busara katika suala la kupandisha posho hiyo!
Hata hivyo, nafahamu fika kwamba hata kama ningekuwa mimi ndie JK nisingekuwa na ubavu wa kuchukua maamuzi hayo hapo juu endapo:
Kwanini nasema hivyo?
IKiwa kweli rais aliagiza busara itumike, basi kutangaza upandaji wa posho muda huu ni ukosefu wa busara uliopita mipaka ingawaje yeye aliagiza kutumika kwa busara! Haiwezekani wakati nchi ipo katika hali tete ambapo wananchi wanakufa kutokana na mgomo wa madaktari wanaodai maslahi zaidi; Waziri Mkuu na Spika wanatangaza kuongezeka kwa viwango vya posho kwa Wabunge! Kama ni kweli Rais aliagiza busara kutumika basi iliyofanyika hapa ni HUJUMA dhidi yake kwa sababu hakuna chembe ya busara iliyotumika. Ni hujuma dhidi yake kwa sababu kauli ya Waziri Mkuu na Spika wa Bunge ni dhahiri imeamsha chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao hasa ukizingatia imetolewa wakati wananchi wanapoteza maisha kwa kukosa huduma toka kwa madaktari. Hii ni hujuma kwavile inaonesha dhahiri kwamba Waziri Mkuu na Spika wa Bunge wameamua kumfitinisha Rais na wananchi anaowaongoza.
Hivyo, ukiangalia mchanganuo huo hapo juu, utakuta ni lazima ama Rais awajibike, kwa kuudanganya umma! Na kama hajaudanganya umma, kwamba kauli ya Kurugenzi ni ya kweli, basi ni lazima Rais awawajibishe Waziri Mkuu na Spika kwa kumhujumu. Na kama Walichosema Waziri Mkuu na Spika ni sahii na kwamba Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema uongo, basi ni lazima Rweymamu ajiuzuru au afukuzwe kazi kwa kutoa kauli inayokinzana na matakwa ya bosi wake ambae ni Rais.

- Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano imeamua kuudanganya umma kwamba Rais hajapandisha posho isipokuwa amewaagiza wahusika kutumia busara. Hapa maana yake ni kwamba, Rais amebariki upandishwaji wa posho lakini anataka kukana kwamba hajafanya hivyo.
- Ikulu kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano pamoja na ushirikiano wao na Spika wa Bunge na Waziri Mkuu, wamefanya hivyo makusudi ili kucheza danadana na akili za Watanzania ili badala ya kujadili suala nyeti la mgomo wa madaktari, hivi sasa tuelekeze akili yetu kwenye suala la posho!