Elections 2010 Pinda na Dr. Slaa wanapogonga kwa furaha

lnawezekana wanausalama wamtishia you never know.Labda wamempiga bit na wemetoa serious threat.Kuna rumours kwamba usalama wa taifa wana monitor nyendo zake na every move he makes.Anyway if that's the case then hao the so called wanausalama hawaewezi wakamtisha Mungu because He God will send them straight to hell for stealing our votes wewe waache wafanye watakavyo kama walishiriki kuiba na wanazuia habari hizo kutolewa then God will send them straight to the depth of hell.It's only a number of days before God send each one of them to the depth of hell wakaishi huko kuzimu na baba yao shetani maana wao wote ni mashetani wakubwa
 
mh, kila mtu ana lake la kusema juu ya hiyo picha, ila wote tujue siasa sio UADUI, SI VITA
 
abmizingoslaa.jpg


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mgombea urais wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa furaha kubwa

Source:Mwananchi
 
Siasa ni jukwaani, walikuwa wanatafuta kula yao na familia zao, uchaguzi umeisha wanaendelea na maisha kama kawaida. tatizo linabaki kwa washabiki ambayo wanaweka vinyongo visasi na kutukana watu wenye kupinga mawazo yao
 
chadema kelele zote zile ni ili wapate kuongoza upinzani bungeni na ruzuku na yote wameyapata sasa mchezo umeisha watu watakula na kufurahi kuonana ni 2015!!!!!!

Kadogoo amerudi. Mjadala utaishia kwenye dini. Ngoja nikimbie.
 
chadema kelele zote zile ni ili wapate kuongoza upinzani bungeni na ruzuku na yote wameyapata sasa mchezo umeisha watu watakula na kufurahi kuonana ni 2015!!!!!!

hahahahaha,tatizo umejaa mawazo ya ki-ccm jinsi wanavo watendea ndio maana!
pole sana,ila unapo leta duku duku kama hili nadhani zinasaidia kwa wao kujua wana wa nchi wanataka nini,haimaanishi kuwachukia ingawa pia chuki inajenga kwa mtu mwenye akili.

thenkisi
 
Mimi ninamtazamo tofauti: Slaa anamwambia Pinda, bahati yako sikuweka mgombea kwako, usingelikuwepo hapa! Pinda anasema, aisee ungelikuwepo bungeni mara hii, ungelitusambaratishaje?

Kusema kweli picha hii inaonyesha ukomavu wa siasa. Wapo wanaomchukulia Slaa kama adui. Hawa ni majambazi! Wapo wanaomchukulia Slaa kuwa ni mpinzani, hawa ni wanasiasa. Wapo wanasiasa wanaocheka na Slaa, hawa ni wanasiasa wa kweli. Wapo wanaomchukulia kila mwanasiasa ni ndugu, hawa ni wa Tanzania.....

Super wisdom We Can. Super.
 
abmizingoslaa.jpg


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na mgombea urais wa Chama Cha demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa furaha kubwa

Source:Mwananchi

Usiami kuwa chuki za siasa ni majukwaani, bali Amini kuwa HAKUNA UADUI WA MILELE.
 
siasa si uadui wala hakuna chuki binafsi. Siasa ya kweli ni ile yenye kutofautiana tu sera na pengine malengo lakini uadui haina sehemu. Ni mawazo0finyu kudhania CHADEMA wasicheka au kushirikiana na wenzao wa CCM kisa wametofautiana sera.
 
Hivi wewe ukipinga hoja ya manager wako ina maana baada ya kikao hicho hata mkikutana kwenye corridor au lunch ndio mzungumzi wala kusalimiana? Je, hujawahi kupinga wazo kwenye hata vikao vya harusi, kwa kumpinga bwana harusi na baadae unampa pongezi?
 
Pinda kicheko chake hakitoki moyoni lakini cha Dr. Slaa chatoka moyoni kabisaaaaaaaaaaa...........................Dr. Slaa ana mapenzi ya kweli na nchi lakini hawa CCM wao ni mlo tu upo mbele lakini siyo kulitumikia taifa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.................................


Hawa watu kiutendaji kwa namna fulani wanafanana, kwa jinsi navyo mfahamu mtoto wa mkulima, kama isngekuwa sheria ya baraza la mawaziri la uwajibikaji kwa pamoja, kwa hahika mtoto wa mkulima angekuwa juu, kwani kuna maamuzi ambayo angeweza kuyafanya kwa maslahi ya watanzania tena wale maskini, mfani mmoja tu, ni upunguzaji wa ununuzi wa magari ya kifahari, Land Cruiser VX and GX, pili upunguzaji wa warsha zisizo na msingi. kwa hivyo vichache tu, nadhani kwa kiasi fulani lugha zao zinaweza kufanana. Unawezaukakuta mtoto wa mkulima alikuwa anamwambia Dr. Hongera Sana kwa kusema ukweli, sis huku tunabanwa sana. Anyway wanavitu fulani in common.
 
Siasa sio vita,kusalimiana kwa pinda na slaa unaona hiko ni kitendo cha usaliti?! Ina maana wewe husalimiani na wana ccm kwa sababu uko chadema?
 
Kusema kweli picha hii inaonyesha ukomavu wa siasa. Wapo wanaomchukulia Slaa kama adui. Hawa ni majambazi! Wapo wanaomchukulia Slaa kuwa ni mpinzani, hawa ni wanasiasa. Wapo wanasiasa wanaocheka na Slaa, hawa ni wanasiasa wa kweli. Wapo wanaomchukulia kila mwanasiasa ni ndugu, hawa ni wa Tanzania.....
Hapo umenena Mkuu :smile-big:
 
Back
Top Bottom