Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

babukijana,
Ulionena hapo hayana shaka, lazima tuelewe huu muungano ulikuwa ni wa Nchi sio Mikoa miwili, kila upande ukihisi haufanyiwi haki basi una haki kulalamika. Na ndugu zetu wa kibara iwapo mnaona malalamishi yameshakua mengina hakuna njia ya kuyatatua basi hata kwenye ndoa zetu za Ki-Islam Talaka imehalalishwa, na tunapofunga ndoa hua tunasomewa dua inayosema kua kuoana kwa wema na kutokana kwa Ehsan ( yaani kwa usalama) especially mshapo zaana. Na hata (hatuombi) muungano ukivunjika basi hatuwezi kua maadui kwani tumechanganya damu sio jana tu kwa muungano bali ni kwa karne. Wengi vizazi vya leo 35+years hawaijui historia ya znz ndio maana utasikia wengine wakisema " ooh muungano ukivunjika mutauwana au mtakufa njaa visiwani " Plse hebu someni history au waulizeni mababu waliobaki vipi ilikua znz kabla ya huo muungano au Mapinduzi.
 
Jamani shule shule shule .Hawa jamaa wana endekeza u mimi na udini na shule hawana .Wanadhani hata wao watalii wanao jazana kwao ni kwa kuwa ni Zanzibar ama ni Tanzania ? Jamaa hawa wana ndamu za kiarabu na akili za kitumwa they think no far from where they in their cage .
Leo Muungano ukifa hakuna sifa ya Zanzibar .Jamaa hawa wana matatizo sana .Ni wakati sasa wa Amiri jeshi Mkuu JK kusema ujinga mwisho na Karume fuata tunayo yasema .Yes we can do that .Sasa nimeona why CUF haitakaa itawale Zanzibar .

Hawa ni sehemu tu na ni mkoa waache wapike kelele .Pinda sema bwana labda JK mtu wa pwani mwenzao anawaonea haya .Mwaka Mkuu wa Majeshi yuko bara na anakohoa hadi kule ushenzini kwa wavivu wa kufikiri .
Tumechoshwa na vijitabia vya watu wavivu wa kazi hadi kufikiri .
Hakuna OIC , Kadhi undeni wenyewe na Muungano upo .Mkitaka tuone mko serious kuuvunja Wabunge wa Zanzibar wasije Dodoma wakae kule kwao waendelee na misimamo .Mnafanya nini huku ? Si mbakie kwenu muendelee kudai mnayo yataka ?
Samahani Mheshimiwa lakini nafikiri ni wewe ambaye shule yako ndogo. Sio Wazanzibari. Tena unawesema wote kwa ujumla-Kumradhi yakhe- aste aste.
 
Pinda
wapeni wazanzibar wanachokitaka hakuna haja ya kuwatisha tisha.Waiteni ,kae nao muwaulize muungano mnautaka ama humuutaki majibu yao myapeleke kwa wananchi wayapigie kura halali.
 
Pinda
wapeni wazanzibar wanachokitaka hakuna haja ya kuwatisha tisha.Waiteni ,kae nao muwaulize muungano mnautaka ama humuutaki majibu yao myapeleke kwa wananchi wayapigie kura halali.
Pinda . Sijui tumsemeje. Hivi hailewi ni nini Baraza la wawakilishi? Hivi haelewi ni nini SMZ Hana hata ule mtizamo mzuri kwa Mawaziri wanaotumikia SMZ. Sijui hiyo CCM anaionaje? sasa bosi huyu ni bosi gani? Kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni yetu sote nafikiri sisi wa upande wa kule tunaweza kusema - hatufai. Na hiyo ndiyo Katiba.
 
Jamani shule shule shule .Hawa jamaa wana endekeza u mimi na udini na shule hawana .Wanadhani hata wao watalii wanao jazana kwao ni kwa kuwa ni Zanzibar ama ni Tanzania ? Jamaa hawa wana ndamu za kiarabu na akili za kitumwa they think no far from where they in their cage .
Leo Muungano ukifa hakuna sifa ya Zanzibar .Jamaa hawa wana matatizo sana .Ni wakati sasa wa Amiri jeshi Mkuu JK kusema ujinga mwisho na Karume fuata tunayo yasema .Yes we can do that .Sasa nimeona why CUF haitakaa itawale Zanzibar .

Hawa ni sehemu tu na ni mkoa waache wapike kelele .Pinda sema bwana labda JK mtu wa pwani mwenzao anawaonea haya .Mwaka Mkuu wa Majeshi yuko bara na anakohoa hadi kule ushenzini kwa wavivu wa kufikiri .
Tumechoshwa na vijitabia vya watu wavivu wa kazi hadi kufikiri .
Hakuna OIC , Kadhi undeni wenyewe na Muungano upo .Mkitaka tuone mko serious kuuvunja Wabunge wa Zanzibar wasije Dodoma wakae kule kwao waendelee na misimamo .Mnafanya nini huku ? Si mbakie kwenu muendelee kudai mnayo yataka ?


There is nothing to do with you!! kama wazenji wanadamu ya kiyarabu au kihindi ,kichina ,hilo halikuhusu wewe ,you sound desperate kama vile anavyo sound mchungaji wako pinda.
 
The Zanzibari want to go seprate ways. Honestly, I don't see how Tanganyika loses by letting them go. This Union thing and the discussion has been going in circles. Slowly everyone is losing their cool. Pinda, and Seleli for asking that question, have started taking the bull by its horns: the road towards separation... which, to my opinion, will be better for both, remember the majority were not invloved to begin with.
 
WATANGANYIKA KWELI MNA UBAVU MNATOKA MNAENDA NCHI YA WENZENU KISHA MNATAOA VITISHA HALAFU MNAONDOKA

KAZI KWELI KWELI

1626351307_7b7f94c0f1_b.jpg
 
Zanzibar will remain to be part of URT kwa sababu tangu mwaka 1964 sijasikia wazanzibari wakitaka kuvunja muungano kwa kutumia njia rasmi. Wazanzibari wanaihitaji bara kuliko bara inavyoihitaji Zanzibar.
Mwisho, historia ya Tanganyika na Zanzibar inadhihirisha wazi umuhimu wa muungano huo, kwani wengi waliopo sasa hivi visiwani humo ni jamii ya wabara waliohamishwa huko miaka mingi iliyopita.
 
Pinda anakurupuka sana katika kujibu mambo..hili atakuja kulia tena aseme alikuwa na uchungu sana
 
natamani sana hli swsala la muungano lifungwe kabisaaaa!
au la sivyo bora uvunjike kabisa, tumechushwa na maneno ya kila siku!
 
Ukweli ni kuwa hata wao wanauhitaji huu muungano na umewasaidia mambo mengi tu ndo maana umeweza kuwepo toka 1964. Isije kuwa imeonekana kwasababu ya uwezekano wa neema ya mafuta, wajanja wachache wanataka kucapitalize kwa gharama za wazanzibar wote.
Mimi naona muhimu ni kuondoa kasoro za muungano na kusonga mbele.Ila kama wenzetu wanaona hilo haliwezekani, basi watangaze tarehe ya lini wanataka kujitoa maana hizi kelele zinachosha sasa. Tukumbuke jinsi watu tulivyokaa sehemu mbalimbali bila shida za hili Tatizo la wapi unakotoka.Naona Pinda hajakosea kwa hili!! Ukimya nao una kiasi.
 
Jamani wana JF,
Pinda naona amejibu vizuri. Viongozi wa Zenji wangekuwa na nia ya kuuimarisha Muungano wasingeenda public bila kuwa na makubaliano na wale wa SMT.

Wakati wa kuambizana ukweli umefika. Kama hawataki kuungana wajaribu kukaa pekeyao.Hayo mambo wanayalilia walishiriki kuyaongeza kwenye Katiba. Hakuna haja ya kuwabembeleza, watajiona tunawatetemekea

Mungu ibariki Tanzania na raia wake. Ameni
 
ZNZ wanasingizia hawafaidiki chochote je sisi bara tunafaidika na nini ambavyo 90% ya wabara ni umaskini mtupu. Nadhani wanashindwa kupasua jipu kuwa rasilimali zote za TZ zimeingia mikononi mwa MAFISADI (Almasi, madini yote, BOT, Meremeta, mikataba ya mikosi, vitambulisho) sasa na wao wanataka kumiliki vyao kusudi wafaidike. Hawa watu wanauchungu sana na nchi yao na siyo kama sisi tunavyoteteana (Kiwira,Dowans) aibu iliyoje kama ungemsikia Ngeleja jana!!! Tena Bara tusiwaingilie hata kwenye Chaguzi kwani wizi wa kura wamefundishwa kutokea huku bara.
 
Ipo siku tutafarakana na haipo mbali Mheshimiwa Pinda na Watanganyika wote waliomstari wa mbele katika kuididimiza Zanzibar na serikali yake ,siku haiko mbali waheshimiwa ,maana japo unasema ndio tutajua ni upande gani utaathirika ,ila kwa kukujulisha upande utakao athirika mwanzo ni upande wa Sultani CCM ,maana serikali yako itabidi ivunjike na kufanywa uchaguzi upya ,nina hakika huo ndio utakuwa mwisho wa ukiritimba wa Chama chako ,huo ndio utakuwa mwisho wa mafisadi kukingiwa ubavu na serikali yako ,utakuwa mwisho wa umasikini kuzidi na kuvuka mipaka hapa Tanzania.

Muungano huu ambao Pinda amesema kuna siku tutafarikiana ,utawaumiza sana vigogo waliomo serikalini ambao ni wezi na mafisadi. Wanaojificha chini ya mwevuli wa nchi ya amani na utulivu ,na sio WaZanzibari tu watakaoshindwa na amani na utulivu kwa taarifa yako hata huko Tanganyika uvumilivu na amani itawashinda.

Msione kuwa WaZanzibari peke yao ndio wanaoona ubaya mnaoufanya katika kuendesha nchi mbili hizi hata huko Tanganyika wanancho wahoi bin taaban kwa jinsi mnavyo iendesha nchi kienyeji na kirafiki. Hayo mabomu yanayolipuka humo bungeni mengi yanaihusu Tanganyika kama si yote ,maana sijasikia bomu likaigusa na Zanzibar ukichukulia madini si mambo ya muungano sasa hapo tu sijui ni ya nchi gani maana msemavyo Tanganyika ndio haipo ,weka kando hilo ,mabomu yote hayo yanaiathiri jamii ya WaTanganyika kwa kina zaidi na ndio yanayowafanya wawe masikini wa kutupwa na nafikiri Tanzania ni nchi ya mwisho kwa umasikini katika nchi ambazo eti zina amani na utulivu.

Hivyo MijiCCM kaeni tayari kuondoka kwenye vyeo vya serikali ,pindi Muungano ukikatika ,tunahitaji uchaguzi Mkuu si zaidi ya miezi sita uwe umeitishwa tuone kama CCM mtatawala tena nchi hii ,msahau.
 
Lunyungu na Mchukia UFISADI...kama huu ndio msimamo wenu juu ya ZNZ basi hata kile Mnachokipigania Bara ni Upuuzi Mtupu...Unaonekana kumtetea Pinda akiwasulubu ZNZ, huku ukimuona Pinda na Timu Mbaya wakiisulubu Chadema....!!!

LKN pia inaonekana Uwezo wenu wa Kufikiri na Kuchambua ni Mdogo sana....I do believe nyinyi wenyewe ELIMU yenu Kiduchu!!!

Pinda Tumsamehe hadi sasa tushajua HAMNA kitu....Kuropoka na Kuja kulia baadae. Nafikiri JK anakazi ya Kupata PM mzuri.
 
Pinda anakurupuka sana katika kujibu mambo..hili atakuja kulia tena aseme alikuwa na uchungu sana

Unajua saa ingine sijui ndio kunaitwa kujikaza ? Yaani Pinda na wenzake wa CCM wanajua wazi kabisa kuwa Muungano ukivunjika tu ,itawabidi waachie ngazi na ndani ya miezi sita ni kufunga virago na kuondoka katika nyumba za serikali na si vinginevyo.

Pinda na wenzake wa CCM wanaufahamu umuhimu wa muungano kwani ndio wanapopatia kula wao na vizazi vyao kwa kujinyakulia mishahara minono ,ikiwa spika ni 8000/- dolars sijui Pinda na wengine wanajitafunia ngapi ?

Pinda anajua wazi kabisa Muungano ndio uliomueka hapo alipo ukivunjika leo basi si yeye hata Raisi wake anapoteza kazi ,wanapokutana huko kwenye vikao kwa siri huwa wanapashana habari hii ndio ukaona wanatoka na kujibu ya kuwa wataulinda Muungano, jamani mnashindwa kulinda mauaji ya Albinoz yasitokee mtaweza kuulinda Muungano usivunjike wakati umma ukisimama kwa lengo moja tu ? Msikae mkidanganyana Mataifa makubwa yenye nguvu duniani nayo yameshindwa kulinda Muungano wamesambaratika kila mmoja na nchi yake ,itakuwa hapa penye majeshi wanaolipwa mshahara wa mkia wa mbuzi hata viatu vya buti mnashindwa kuwagharamia tunapishana nao njiani mtu kakuvalia sare ya jeshi chini ana yeboyebo ,sio utani wapo mitaani wamejaa tele,wengine wakifika kustaafu ndio anaanza kuonja joto la umasikini.

Pinda kwa usalama wenu wa kuendelea kukaa mdarakani chini ya Sultani CCM basi msitake makubwa na kutoa maneno ya dharau ,nchi haitawiliki kwa furaha na amani kwa kutumia nguvu na maneno ya kejeli,hilo ni lazima ulielewe maana wananchi watakuwa hawana raha nanyi viongozi pia hamtakuwa na raha ,maana usingizi wenu utakuwa wa mapande.


Eti iko siku kutatokea mfarakano,na kwa maana hiyo watu watagawana mbao ,mimi nakwambieni ikitokea kugawana mbao basi siku ya pili mfunge virago mrudi makwenu,kuna vyama ambavyo hivi sasa vinaichungulia Ikulu kwa hamu kabisa na mate yanawatoka ,kuvunjika kwa Muungano ndio mwanzo wa Vyama hivyo kukenua.

Muungano ni jinamizi liloinamia vyama vya upinzani linalosaidiwa na Chama cha CCM. Sijui kwanini watanganyika hawalioni hili ,kuwa maendeleo yao yamebanwa kutokana na Muungano huu ,maana wanashindwa kuiona ile hoja ya kusambaratika kwa CCM iwapo Muungano huu utaenguliwa.
 
Lunyungu na Mchukia UFISADI...kama huu ndio msimamo wenu juu ya ZNZ basi hata kile Mnachokipigania Bara ni Upuuzi Mtupu...Unaonekana kumtetea Pinda akiwasulubu ZNZ, huku ukimuona Pinda na Timu Mbaya wakiisulubu Chadema....!!!

LKN pia inaonekana Uwezo wenu wa Kufikiri na Kuchambua ni Mdogo sana....I do believe nyinyi wenyewe ELIMU yenu Kiduchu!!!

Pinda Tumsamehe hadi sasa tushajua HAMNA kitu....Kuropoka na Kuja kulia baadae. Nafikiri JK anakazi ya Kupata PM mzuri.

Wako katika mission. Muungano hauwezi dumu kwa nguvu, kukaripiana ama kutishana. Suala ni majadiliano na kuweka mambo sawa, lakini kama tunataka meza ya mraba yenye miguu miwili isimame bila kuanguka, tunajidanganya. Kuna tatizo katika muungano, na ni haki kwa pande zote kujadili bila kutishwa.
 
sorry to say, huyu bwana huwa hana point kabisa. Anajitahidi kuchangia lakini mh, uwezo wa kuanalyse mambo ni mdogo. Kashambulia wazanzibar, waislam na matusi kibao. Changia hoja sio kushambulia watu. Na kama huna cha kuchangia tulia subiri watu watu waandike

mhh mbona umemuona huyu pekee kuna wengi hapa wametoka nje ya hoja!! Pia hayo ni mawazo yake kwani kuna tatizo kuhusu mtu kutoa maoni yake? Je wewe umetoa yapi ili tuone analysis?
 
Zanzibar tatizo ni kero za maisha sio za muungano, wanashindwa kugundua baina ya tatizo la muungano na tatizo la maisha, iwapo watapata ufumbuzi wa kero za maisha hakuna kero za muungano, SMT wajaribu kusaidia kutatua kero za maisha kule Zanzibar hatutosikia tena kero za muungano

Masanja umenikuna kwa wazo hili. Nami nimkuwa na mawazo hayo kwa muda mrefu. Maana ukitembelea Zanzibar Iwe Pmba au hata Unguja yenyewe hali ya maisha ya wanchi ni duni mno, afadhali hata ya bara! Lakini inapokuja kudai haki wanadai vitu ambavyo ni "too abstract" kuliko hali halisi ya shida walizo nazo. Madai kama ya OIC, Kutambuliwa FIFA, Mafuta ..... ni ya msingi lakini hayapaswi kuwa mahitaji yao ya msingi kwa matattizo ya wananchi wao.
 
waziri mkuu Pinda ni mmoja wa viongozi ambae amekuwa na uzowefu mkubwa katika siku za karibuni kuwa ni kipaza sauti cha kuusemea Muungano huu HARAMU ambao kila kukicha unazidi kuonekana athari zake, na kutowa harufu mbovu mbele ya Wazanzibari wenyewe !! Nashukuru sana kuwa hii leo tumefikia pahala ambapo hakuna Mzanzibari yoyote ambae hakuweza kuziona athari hizi, na harufu hizi, na kufikia kuzichukia !!



Waziri mkuu Pinda ametahadharisha kuelekea kuvunjika muungano huu endapo kutaendelezwa kuzungumziwa malumbano kuhusu mafuta na gesi asilia, na baada ya hatuwa hio akaonya kuwa baadae, upande mmoja utapata shida !! Bila ya kutaja upande gani, na shida za aina gani ambazo muheshimiwa huyu anatabiri kuwa itaupata upande huo !!Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka tu, mie ninaona kuwa waziri huyu hakutahadharisha kama alivyotaka Watanzania kwa umoja wao wamfahamu !! bali alichofanya ni kuutisha upande wa Zanzibar moja kwa moja !! na hakuishia hapo tu pia amechukuwa fursa ya kuwagawa Wazanzibari kwa kutamka kuwa [baadhi ya viongozi], wakati viongozi wote wa siasa na serikali ya Zanzibar ndio msimamo wao ndio huo!!



Ameendelea kuwataka Watanzania kulitizama jambo hili na kulichambuwa kwa kujuwa ni nani ambae ataathirika endapo jambo hili litafanyika !! Hili halina pazia !! hapana shaka yoyote kuwa Tanganyika ndio watakaoathirika endapo watakoseshwa kushirikishwa katika ghila hii ya mafuta, wakati wanaimezea mate !!

Na la pili ambalo hii leo linawatahayarisha zaidi ambalo haliepukiki, ni kule wao kuinyima Zanzibar kwa muda wote huu rasilmali za maadeni na gesi na mawe ya Kiwira !! jambo ambalo liliwatia uroho wa kufaidika pekeyao pasina kuhisi kuwa wana ushirika na wenzao kutoka visiwani Zanzibar !! iweje hii leo kwa uchimbaji wa mafuta iwe nongwa kwa wenzao kudai haki zao ? Na jambo la kustaajabisha zaidi kuwa Pinda na wenzake hii leo wako tayari kuitengeza katiba ili wafaidike na mafuta ya Zanzibar kwa kutamka tena bila ya kuona haya hii leo, kuwa wako tayari na maadeni kuyachanganya katika muungano!! Na huku wakisema kuwa hata hayo mafuta yenyewe hakuna tamaa kuwa yapo !! sasa tunamuuliza Pinda na wenzake, ikiwa hayo mafuta hayapo, mnayatakia nini? Si mungewaachia wenyewe Zanzibar wakahangaika nayo nyie mnayatakia nini ? halafu anajigamba kwa kusema kuwa ikiwa itawezekana kuliondowa jambo hili katika katiba kisheria itakuwa kheri !! Lakiniiiii si kuvunja muunganoooooo !!! mie nasema na kwanini kusiwe kuvujwa muungano wenyewe ambao nyie ndio munaoutumia kama silaha ya kuikaba Zanzibar???? Muungano uvujwe tu, ikiwa huo ndio unaokutieni kibri cha kutawala wenzenu kimabavu !!

Ikiwa kuambiwa wezi ni Noma !! basi hivyo ndivyo mlivyo!! Kwani kipo milichokibakisha Zanzibar???

Kuhusu katiba kulindwa ndio kamba yenu hio ya kutunyonga!! Lakini hivyo kweli ni katiba hii ambayo ilitakiwa kuiongoza Tanzania? Iweje kwa miaka nenda miaka rudi mkashindwa kuitisha mkutano wa kuundwa katiba ambayo ya kukubalika pande zote mbili? Wakati ndio makubaliano ya muungano huu?

Muheshimiwa Hamad Rashid ameshaweka wazi ubovu wa katiba hio!! Tena mantaka nini zaidi ya hilo? Kuilinda hio katiba muisemayo ni kuendelea kuikaba Zanzibar ambayo haiko tayari tena kuendelea kuikaba !! Wazanzibari shikeni uzi huo huo !! kurudi nyuma mwiko !! unganeni kwa kuikombowa Zanzibar na janga hili !! hao si wenzenu!!mweke pembeni vyama vyenu, muungane kwa maslaha ya Zanzibar !! wacheni kuuwana wenyewe kwa wenyewe kwa maslaha ya chama!! Gomeni kuingia katika chaguzi zisizoleta maana na kuukoroge mseto moja kwa moja!! Tuna killa la kijivunia Zanzibar!! Tuna airport, bandari, ghila ya karafuu, mwani, kombe,mafuta ya nazi, na hivi ndivyo Zanzibar ilivokuwa ikivitegemea !! NA ZAIDI YA YOTE TUNA UTU NA USTAARABU WETU KUTOKANA NA DINI YETU YA KIISLAMU .Wacheni uoga huo na kutishwa na akina Pinda na vibara vyake!! Watakaoumia si Zanzibar vijana !! watakaoumia ni hao ambao wanaokhofia mungano kuvunjika !!
 
Back
Top Bottom