MzalendoHalisi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2007
- 4,517
- 1,367
Vuia Ndo waziri kiongozi! yeye ameshatumia hekima ktk kujibu!
Wacha hao mawaziri wadogo waendelee kutumia jazba!
Wacha hao mawaziri wadogo waendelee kutumia jazba!
Vuia Ndo waziri kiongozi! yeye ameshatumia hekima ktk kujibu!
Wacha hao mawaziri wadogo waendelee kutumia jazba!
MIAFRIKA NDIVYO TULIVYO..
Ndugu zangu nadhani umefika muda nami niandike kitabu changu kuhusu Miafrika Ndivyo Tulivyo kisha nimlipe Nyani Ngabu fidia ya jina hili..
Hivi kusema kweli Ugonvi kati ya Zanzibar na bara, kitu gani haswa!.. Yaani kesho tukisema Zanzibar ni nchi, kitaongezeka kitu gani kwao zaidi ya PRIDE..kuwa sasa hivi zanzibar inajulikana kama nchi..Tangayika haipo na wala haijulikani hilo tatizo lao wenyewe wamependa iwe hivyo.. so what comes with this recognition! maanake kama ni serikali ya Zanzibar (SMZ) ipo na wana viongozi wao, bunge lao, utawala wao..na mfumo uliopo sasa hivi kama sikosei kwa wazanzibar ni Changu Changu, Chako Changu!..
Mapato yote ya Zanzibar ni ya Wazanzibar isipokuwa wanachogombea ni mkato zaidi toka serikali ya Muungano. sasa ikiwa chenu hakiwatoshi na sababu kubwa ya kuvunja muungano ni kile kinachotoka bara ktk serikali ya muungano mnagawiwa kama mkoa kinawauma, Mkijikata mtapata kipi zaidi na toka wapi? au hii kitu mafuta ndio inawatoeni roho!..What if mafuta hayo yapo kati ya Bara ya Zanzibar (offshore) nani mwenye mali hiyo na kipimo gani cha mipaka kimewekwa baina ya bara na Zanzibar ndani ya maji!..
Tanganyika imeua jina la nchi yake na kuwajulikana kwa mikoa tu, leo imekuwa sababu ya zanzibar kudai nchi ambayo tayari wanayo isipokuwa jina tu ndio halitumiki..Hii kitu gani jamani?..
Ama kweli naamini maneno ya CIA mmoja aliyejiuzuru alipohojiwa jinsi wanavyofanikiwa kuzigombanisha nchi maskini.. na akasema tefauti na matumizi ya FEAR kwa nchi za Ulaya, mwafrika mgombanishe kwa PRIDE..
alifafanua na kusema, Waafrika watauana wao kwa wao kwa sababu ndogo sana ya pride. Watagombea kipande cha ardhi ktk shamba kubwa hata iwe futi moja utafikiri kipoande hicho kina maana kubwa sana kwao, lakini ajabu siku ya mavuno utawakuta hao hao wagonvi waki share mavuno zaidi ya kipande kile cha ardhi..Ndio hayo ya kina Raila na huyo Morgan ambao wamesababisha maelfu kuliwa, walipopewa cheo tu wamesahau kabisa kile walichokuwa wakigombania..wanakula sahani moja na shetani.
Ukielewa jinsi Pride kuwa ndio kiini cha umaskini na magonvi yote ya mtu mweusi basi hili swala la Muungano halina tofauti kabisa, na hakika - Miafrika NDIVYO TULIVYO..
Mkuu wangu pengine wewe huelewi bajeti ya serikali mbili zilizoungana inakwenda vipi.. Na hii ndiyo tofauti ya kuelewa kwenu.Kwanini huwi muungwana na kukubali Wazanzibari watumie kilicho chao?
Hii kauli ya "Changu changu ... Chao changu " mbona unaigeuza?
Kwani Zanzibar ilishadai kitu gani kutoka bara kuwa ni chao? Kwa sasa bara wana madini, mapori na maziwa makubwa, jee ulisikia zanzibar ikidai ipatiwe mgao? Jee umesikia lini pato a inayoitwa Serikali ya Muungano likakasimiwa na kutiwa kwenye Bajeti ya Zanzibar? Ukisikia asilimia 4.5 ni kwa mapato ya misaada inayokuja kwa jina la Tanzania. Sasa wapi inapply hiyo chenu changu? Umeme zanzibar wanaadhiriwa kila siku kwa kuchelewa kulipa.
Naona hivi Muungwana huwa hanganganii ujinga wa mtu na kwa vile Wazanzibari ni wajinga kwa kungangania mafuta yasiopo basi nyie mlio sio wajinga ni bora mkawachia na ujinga wao na hapo mtakaspothibitisha ujinga wao itakuwa wakati mzuri wa kuwacheka lakini kwea sasa Wazanzibari wanataka chao na ni haki kupewa basi!
Ngekewa.
Sijasikia Zanzibar kuwa wana jeshi lao. Sijasikia kuwa Zanzibar wana polisi wao.Sijasikia kuwa Zanzibar wana balozi zao. Sijasikia kuwa wabunge kutoka Zanzibar wanalipiwa na SMZ. Sijasikia kuwa wazanzibari wakitibiwa Muhimbili wanalipa tofauti. Sijasikia kuwa wazanzibari wakisoma katika shule na vyuo vilivyoko bara wanalipishwa tofauti. Mambo yote haya yanagharamiwa na SMT ambayo mapato yake ni kutokana na hayo madini, mapori n.k. yaliyopo bara.Zanzibar walikuwa wanauziwa umeme kwa bei ya chini kuliko bara. Hiyo tofauti ilikuwa inalipwa na nani? Mnaposema Zanzibar haifaidiki na rasilmali zilizokuwepo bara mna mana gani? Mlitaka mfaidike vipi? Mfanyiwe kama Alaska, kila mzanzibari apewe mgao wa Tanzanite ndiyo mridhike? Mkandara hakukosea.
Amandla........