Pinda: Madaktari wananisikitisha

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
Monday, 05 March 2012 10:13
0digg
pinda-mizengo-top.jpg
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda​
Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya madaktari kutishia kuanza mgomo mwingine, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema amesikitishwa na tishio hilo akisema kwa sasa Serikali ipo katika mchakato wa utekelezaji wa makubaliano mbalimbali na wanataaluma hao.

Pinda alitoa kauli hiyo jana aliokuwa akizungumzana katika mahojiano maalumu na Gazeti dada la Mwananchi, The Citizen na kusema hatua hiyo mpya ya madaktari inamsikitisha kwa kuwa Serikali ndiyo kwanza inaendelea na vikao kwa ajili ya kuangalia namna ya kutekeleza madai yao hayo.

“Siwezi kuzungumza chochote sasa wakati Serikali inaendelea kushughulikia mgogoro huo. Niseme tu kwa kweli wananisikitisha (madaktari). Ninasikitika kuona kwamba wakati bado tuko kwenye mazungumzo, wenzetu wanafanya vikao vingine,” alisema Pinda.

Akilihutubia taifa Februari 29 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alieleza kufurahishwa na hatua ambayo suala hilo limefikia akisema:“Nashukuru mgomo huo umekwisha lakini makovu yake yatabaki maisha katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.”

“Leo (Februari 29), Mheshimiwa Waziri Mkuu amenipa taarifa kuwa kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa yake kwake. Kuanzia kesho (Machi, Mosi), Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo. Ninawaomba ndugu zetu madaktari kuwa na moyo wa subira.”Rais Kikwete alisema Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi za madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya katika kulinda na kudumisha afya za Watanzania hivyo itajitahidi kuona kuwa inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mgomo haujirudii tena.

Hata hivyo, wakati Pinda akieleza kusikitishwa na hatua hiyo mpya ya madaktari, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Lucy Nkya alisema hawezi kujiuzulu kama madaktari hao wanavyotaka kwa kuwa suala hilo liko nje ya uwezo wake.“Hivi sasa siwezi kuzungumza chochote kwa kuwa suala hilo liko juu yangu na siwezi kujiuzulu,” alisema Dk Nkya.

Tishio la madaktari
Juzi, madaktari hao waliipa Serikali siku tatu kuanzia jana hadi Jumatano wiki hii kuhakikisha inawatimua kazi Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Naibu wake, Dk Nkya vinginevyo watatangaza mgomo mwingine waliouita wa kihistoria.

Pia, madaktari hao kupitia kwa wawakilishi wao waliopo katika kamati iliyoundwa na Pinda kujadili madai yao, wamekubaliana kutoendelea na majadiliano hadi hapo mawaziri hao watakapoondolewa kwenye nyadhifa zao.

Hatua hiyo imekuja zikiwa zimepita siku chache baada ya kikao kilichoitishwa na Serikali kujadili suala hilo kuvunjika huku kila upande ukituhumu mwingine kuhusika.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa madaktari hao ulifanyika Dar es Salaam juzi, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi alisema kama mawaziri hao wataendelea na nyadhifa zao hadi Jumatano, madaktari hawatakuwa tayari kuendelea na kazi.

“Madaktari wameona isingekuwa jambo jema kuendelea kujadiliana na kufikia uamuzi na Serikali huku Waziri na Naibu wake wakiendelea kushikilia nyadhifa zao, watu hao wanawajibika kwa kila kilichotokea? Nani asiyejua kuwa vifo vilitokea wakati wa mgomo?” alisema Dk Mkopi na kuongeza:

“Wananchi na makundi mbalimbali wanawataka wajiuzulu hata madaktari hawatajisikia vizuri kufanya kazi huku wakiendelea kuongozwa na mawaziri hao.”

Dk Mkopi alifafanua kuwa kamati iliyoteuliwa na Waziri Mkuu kushughulikia suala hilo, imeonyesha utayari wa kuwasikiliza na kufikia makubaliano, lakini kuendelea kuwepo mawaziri hao ambao ni sehemu ya watuhumiwa, ni kikwazo katika utekelezaji.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya alisema kitendo cha mawaziri hao wawili kushindwa kujiuzulu ni majaribu.

“Tangu watu walivyoanza kufa kutokana na mgomo wa madaktari uliotokea na wao kuendelea kung'ang'ania madaraka inashangaza nafikiri ni wakati sasa wajiuzulu,” alisema Nkya
 
Nice...Hii ni kielelezo kizuri sana cha nguvu ya wananchi versus Watawala!
 
Pinda sasa unakosea, kama ulijua mchakato ni mrefu kwa nini uliahidi kwa tarehe? si ungesema tu madai yenu yatatatuliwa mwezi march au april?

Na hata hilo la kuwaondoa kazini hao washukiwa nalo limekuwa zito??? mnabeep nyie!
 
Hata mimi madaktari sasa wanatia shaka! uadilifu wao kwa umma haupo tena ila uadilifu kwa matumbo yao ndio wanauona ni muhimu, hata kama kwa gharama za maisha ya watu wasio na hatia! Twafaa! as the saints are no more around!
 
Nalichukia sana hili neno mchakato
kila kitu serikali iko kwenye mchakato
Lini tutafanya mambo kwa uhakika tuachane na mchakato na upembuzi yakinifu
Ndo maana wenzetu wanatushinda kwa mengi
Kila siku mchakato, mchakato hata kama ni mwaka au miaka miwili mchakato
 
Pinda sasa unakosea, kama ulijua mchakato ni mrefu kwa nini uliahidi kwa tarehe? si ungesema tu madai yenu yatatatuliwa mwezi march au april?

Na hata hilo la kuwaondoa kazini hao washukiwa nalo limekuwa zito??? mnabeep nyie!

Ama kweli Uongozi sio kwenda kuuza sura ni kuwajibika kwa wananchi

“Leo (Februari 29), Mheshimiwa Waziri Mkuu amenipa taarifa kuwa kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa yake kwake. Kuanzia kesho (Machi, Mosi), Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo. Ninawaomba ndugu zetu madaktari kuwa na moyo wa subira.”Rais Kikwete alisema Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi za madaktari na watumishi wengine wa sekta ya afya katika kulinda na kudumisha afya za Watanzania hivyo itajitahidi kuona kuwa inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa mgomo haujirudii tena.

Kwenye blue hapo sentence hiyo ina ukweli ndani yake au ni unafiki tu ulio kithiri katika serikali ya JK? Ni miongo mingapi ya Marais Tanzania wamepita na kuthanini Afya ya watanzania?

Kikubwa katika miongo yote ya marais kumekuwa na ufujaji wa mali ya umma tuuu na ni viongoizi wa ngazi ya juu wana wanyonya wananchi, Mfano mzuri Marcus mwanahataraki juuzi kwenye radio Clouds FM alisema Pesa ya maendeleo ya wananchi itolewayo ni 34% na pesa inayo liwa kama rushwa katika sekat zote nadni ya nchi ni 33% sasa hapo serikali inafanya nini si unafki tuuu hapo.

Nadhani serikali imefika mahali haijitambui kabisa hata kutojua kinacho endelea ndani ya nchi ni kipi.

Nalichukia sana hili neno mchakato
kila kitu serikali iko kwenye mchakato
Lini tutafanya mambo kwa uhakika tuachane na mchakato na upembuzi yakinifu
Ndo maana wenzetu wanatushinda kwa mengi
Kila siku mchakato, mchakato hata kama ni mwaka au miaka miwili mchakato

Mkuu umesahau na neno CHANGAMOTO

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom