Pinda LIVE BUNGENI maswali ya papo kwa hapo..

Nakuunga mkono mkuu,Pia na Rostam ndiye aliyekuwa anaipiga jeki serikali sana jamaa kagoma anadai pesa zake.CHAMOTO SERIKALI HII hitakipata.Lakini ndo dawa na mwizi.?
 
Davidi Siinde kasema wampe wizara hiyo kwa miezi tuu atabadilisha kila kitu maana kama waziri ameshindwa kazi aliyokubali mwenyewe na hataki kuachia basi apewe yeye hadi Waziri Nundu mwenyewe kashika kcihwa kwa kucheka

Conchesta viti maalumu Chadema kasema hawawezi kulambishwa pipi na waziri mkuu kwa billioni 95 anasema lazima fedha zaidi zikatafutwe huko zilikofichwa manake zipo iweje kwa masaa tuu fedha iwe imeongezwa anasema ziongezwe kama Waziri Nundu alivyokuwa ameombwa anasema wamemtwisha Nundu mzigo lakini anastahili kuubeba
Kwa kweli wabunge jana na leo wanajitahidi
 
Nundu anatoa hoja zake na kujibu yale ambayo aliulizwa..magamba wanapiga makofi inaonekana hawa jamaa waapitisha bajeti tuu...
 
Kweli Nundu ni Nundu kweli..anasema hizo bilioni 95 zilizoongezwa na Pinda anakiri kwamba zitatimiza haja zote za wizara ya uchukuzi...haya bwana tutaona kama kweli utafanikiwa...
Ila magamba wanapiga makofi tu..zile hasira za wabunge wa ccm naona sasa wanacheka tu..huu si usaliti kweli?
 
Maadam issue ya Ufisadi - EPA, Richmond, rada, IPTL, Meremeta, madawa ya kulevya, mgao wa umeme na mengine mengi yamekuja na kupita na bado CCM imesimama imara chini ya uongozi wa JK...Basi haitatokea tena swala jingine lolote ambalo litaimaliza CCM. Yanayofanyika bungeni ni mchezo wa maigizo tu kwa sababu wabunge wetu hawana tofauti na wananchi ambao pamoja na adha zote walizopitia wameshindwa kusimama dhidi ya serikali yao kutokana na nidhamu ya woga. Na sidhani kama ni akili kusifia lolote ktk kujaza kapu lilotoboka!

The Emils, nimeipenda sana signature yako kama kuna ukweli - we ain't fit to live....
 
spika ananza kupitia kila hoja lakini wabunge wengi wa upinzani wamesimama kuonesha kutokukubaliana na vifungu flani hivyo lazima wapatiwe maelezo kwa kina..ccm wapo olesendeka, rage, kigwangala,..upinzani namwonq lissu, mnyika,..jamani naona wabunge wengi ngoja tuone kama itapita kweli..mbowe anaanza kuhoji
 
lissu ametamka wapi bilioni 95 zimetoka, amesema hizo pesa zimechukuliwa kutoka kwenye wizara ya magufuli..lukuvi kakubali ni kweli lakini watalitolea maelezo badae..lissu anataka apewe limefanyikaje kisheria? Kasimamishwa naibu waziri wa fedha amejibu ovyo tu, Mnyika kaomba kutoa tarifa, akaitwa Werema nae katoa maelezo kidogo..hivyo bungeni kumbe siasa chafu tu..
 
waziri anajibu maswali kisanii sana,hana hoja za nguvu na pia hana kauli za kiserikali.
 
walichomalizia ni ndioooo...duuuh kweli pinda amewalainisha wabunge na bilioni 95... Binafsi siungi hoja hiyo... That is the End for today..
 
Kindly tuwe watiifu na wakweli,PINDA ni mnafiki sijaona alichojibu hata kimoja.Inasikitisha sana.Pinda swali kugoma kuuza mafuta Dar es Salaam uliloulizwa na Mbowe hukujibu sasa huu mgomo ukiendelea hadi kesho mida kama hii usilaumu maamuzi tutakayochukua
 
Back
Top Bottom