Pinda kashindwa kutoa tamko la serikali kuhusu bei ya sukari kagera

Kachocho T.K

Member
Feb 1, 2011
25
3
Pamoja na kuwepo watu kiduchu waliohudhuria mkutano wa waziri mkuu uliofanyika wiki iliyopita kwenye viwanja vya uhuru platform mjini Bukoba, maarufu kama mayunga, Bwana pinda alishindwa kutoa tamko la serikali kuhusu bei halisi ya sukari. Wananchi wakiwa wapweke na kuonekana kama wako sehemu ya ibada wakati yeye akihutubia mkutano wa hadhara, walibadilika na kushangilia pale pinda alipogusia suala la sukari kupanda bei mjini abukoba na maeneo mengine wakati kiwanda cha sukari kipo km 70 tu kutoka mjini Bukoba. Aliishia kusema haiingii akilini kuona kiwanda kipo km 70 kutoka hapa halafu wananchi wanunue sukari kwa sh 2,000 hadi elfu 2,200 wakati wakazi wa Dar. wanapata sukari kwa sh1,800 kwa sukari hiyo inayotoka kagera. Aliwavunja watu mbavu na kurudia hali ya kusononeka pale aliposema nimemwagiza mkuu wa mkoa kubaini wasambazaji wa sukari mkoani humu kisha wakae chini na kuangalia sababu za kupanda kwa bei ya sukari na kutafuta njia mbadala.
Hivi kweli kulikuwa na haja ya pinda kupanda jukwaani na kuwaambia wananchi maongezi yake na mkuu wa mkoa? Wananchi walitarajia serikali makini ingekuja na suruhisho la bei halisi wanayopashwa kutoa si maongezi yake na mkuu wa mkoa.
 
ahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaa kazi kwelikweli, wangembana zaidi angeanza kulia weeeeeeeeeeeeeeeee
 
Hata akitoa tamko nani atalitekeleza?? The guy is so useless I wound't vote him for my ward councilor position!
 
Na sasa angelia Kulio cha mtu mzima nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa mtoto wa mkulima kwishneeeeeeeeeeeeeeeee
 
wakati anatoa hayo maelezo hakulia kwel? Manake huyu mzee ana majonz ya karb. Oh sor i mean ana machoz ya kinafki. Ndo wale wale, machon km wa2!!
 
Mkuu huyo Pinda hana maana yoyote. Hawezi kutoa maamuzi yoyote. Sijui kama anafahamu powers alizonazo kama waziri mkuu!

Pia ni mwoga sana huyo jamaa! Yaani hata kumwajibisha mkurugenzi wa hapo Bukoba anashindwa wakati yupo chini ya mamlaka yake!

Hafai huyo mjomba!
 
Pinda kwa sasa kachafuliwa na bosi wake,Bosi mambo magumu anatapatapa tu.sio kama kashindwa ni kwamba kazi waliotumwa wameshindwa,
 
Mkuu huyo Pinda hana maana yoyote. Hawezi kutoa maamuzi yoyote. Sijui kama anafahamu powers alizonazo kama waziri mkuu!

Pia ni mwoga sana huyo jamaa! Yaani hata kumwajibisha mkurugenzi wa hapo Bukoba anashindwa wakati yupo chini ya mamlaka yake!

Hafai huyo mjomba!
pinda ni joka lisilo na SUMU
 
Sababu wanaijua ila wanapotezea watu muda wao.
Wapuuzeni hao mafisadi.
Dawa ni kuwang'oa tu,hilo ndilo suluhisho pekee.
 
Back
Top Bottom