Pinda: Karibu asilimia Tisini na Tisa (99%) ya Wanzanzibar ni Waislam

Status
Not open for further replies.
Haya makelele mnapiga humu JF ni buree tu, Wazanzibari wakristo wanajihifadhi kama waislam as part ya utamaduni wa Mzanzibari. We endelea kupiga kelele tu.

Mimi in two weeks to come nitakwenda Zanzibar, nikishuka tu bandari ya Malindi nitatembea kwa miguu hadi Michenzani huku nikila KARANGA zangu njia nzima na kunywa MAJI yangu ya Kilimanjaro. Halafu nione kama kuna mtu atathubutu kunishika na kushitaki. Hii sio utani, siku naondoka nitawaanga hapa JF.
 
Zanzibar is 70% Muslims, and the number is going down everyday, as new Zanzibaris are mostly Christians arriving from Europe of Africa (mengine ni blah blah)
 
Kinacho shangaza zaidi swala la zanzibar kuwa na waislam 99% kuwa sababu ya watu wachache kunyimwa haki zao! Kama kufunga sio lazima na kuna watu wana sababu za kuto kufunga tena ni waislam . Kwa nini mahotel na migahawa ifungwe?

Na shindwa kuelewa huyo mungu tuna yemtumikia ni yupi mpaka tuna shindwa kuwa hurumia na wenzetu wenye imani nyingine au wasio na uwezo wa kufunga.

na hilo ndo tatzo manake wapo ambao hawafungi kwa sababu maalum lkn ananyimwa haki hata ya kula anyway yawezekana ka imani yao basi wakawa hawaruhusiwi kula hadharan lkn vp wale ambao hawana imani hiyo?ama ndo kuwafanya watumwa kwenye nchi yao?
 
hiyo 99% ilikuwa tu sababu iliyotumika na kina Abeid Karume kumpindua kiongozi wa kwanza wa Zanzibar huru chini ya Mkiristo John Okello aliemtimua Sultani, ambe alikalia kimabavu Zanzibar kwa miaka kama 300 baada ya kuwashambulia na kuwauwa Watawala na Masista wa Kikatoliki (wajenzi wa Ngome Kongwe) waliokuwa wanatawala Zanzibar, Kilwa, Mombasa etc.
 
Wingi wao sio sababu ya kukandamiza haki za wengine wasio waislamu kwa kung'ang'aniza kufuatwa kwa masharti ya uislamu...pm kachemka kama kawaida yake tena

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Sidhani kama huo ukristo wako au upagani unakuruhusu kuvaa chupi hadharani, na wewe unajua kwa nini mnavaa nguo fupi, hata mila zetu za tanzania haziruhusu kuvaa nusu uchi, na unafahamu kwamba mwanaume akikuangalia huku umevaa nguo fupi na za kubana ili uoneshe masaburi yako unakuwa ume mtamanisha. Sasa kwa zanzibar watu wamefunga kwahiyo usiende kuonesha masaburi yako kule ni marufuku.
kisa nimesema ukweli???? siyo wote ni waislamu hata kidogo na wala uislam wangu ama wako haumfanyei mwingine akose uhuru hata kwa mambo yake binafsi. itakuwa si haki.
 
Wewe ni kilaza kweli hata huo ukristo pia huujui, nani alikwambia kwaresma watu wanafunga kula kama waislamu? look at you! watu wamedai takwimu mkashabikia hakuna haja, na thread za namna hii utaona zikichangiwa sana humu JF, kwahiyo kwakuwa zanziba si nchi basi mwende mkale mchana, ni haramu kwa zanzibar. Ile nchi inatakiwa iongozwe kiislam, mmeenda mkafanya vurugu na ukristo makanisa yakachomwa, bado tu hamuamni? let zanzibar be free hata sisi wengine wa bara tukafungie kule maana huku ni kero sana. watu ako uchi mabara barani. angalia mapovu hapa, kule Znz hakuna mfumo kanisa. Ni huku bara tu, nako hamtaki mjulikane idadi yenu. Sijui mnaogopa nini.
Pamoja na waziri mkuu kujibu swali la mbunge wa Iringa mjini leo asubuhi juu ya
matamshi ya waziri wa sheria na katiba wa zanzibar kuzuia Hotel zote zifungwe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na hata kuchukuliwa hatua hatua kwa mtu yeyote atakayeonekana anakula mchana zanzibar ni kitendo kisicho vumilika naasikitika kupingana na hoja hii kiimani kwani binafsi si muumini sana miongoni mwa wanao amini zaidi ya mapokeo ya kifamilia na kijamii.
Kitendo cha serikali kukubali kuwa hoja iliyotolewa na waziri zanzibar juu ya mwezi huu mtukufu unatutoa kwenye hatua moja ya kimaisha hadi hatua nyingine kwani nataraji siku moja kusikia wakristo nao wakidai kuwa kipindi cha kwaresima hotel zote zifungwe na atakayeonekana anakula mchana wakati wa kwaresima basi achuliwe hatua kali za kisheria (ipi?) kula mchana.
Hoja zangu za msingi hapa ni hizi zifuatazo
1. serikali haina Dini?
2.zanzibar ni nchi au siyo nchi
3.Zanzibar imo ndani ya muungano au nje ya muungano?
4.jibu lolote la swali la kwanza hapo juu jee mambo ya Dini ni mambo ya muungano au la?
5.Sensa ya kuwa Zanzibar ina idadi kubwa ya waislamu ilifanyika mwaka gani na takwimu zikoje?
6.wanaodai kipengele cha Dini kiwemo kwenye Dodoso la sensa mwaka huu wapo sahihi au hawapo sahihi?
Mwisho lakini si kwa umuhimu yeyote atakaye changia hoja hii ahakikishe aliangalia kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa hapo ya waziri mkuu leo asubuhi kwa kurejea swali lililouzwa na Mh Msigwa.
karibuni sana!
 
Tuache upotoshaji. kauli ya mh. Msigwa sio kauli ya CHADEMA. Mh.. Msigwa sijui kama anayaelewa mazingira ya Zanzibar na hata yale ya Mafia. Na sina uhakika kama Mh msigwa anaishi na wakristo tu huko Iringa. Mh Msigwa asijaribu kuwagombanisha watu wa dini mbalimbali kule Zanzibar. Tangazo hilo limetolewa bila shaka kuwapa taarifa watu wageni wa taratibu za mwezi wa Ramadhani kama kina Msigwa. Kwa wenyeji wa dini zote Zanzibar hili sio geni na wala haliwapi shida.

sio kweli linatupa shida sana....kwa nn dini yako iwe kikwazo kwangu km ww unafunga funga kwa imani yako na wala usitake watu wakujali sana au na wao wabadili tamaduni zao eti kisa ww uko kwenye mfungo,mwezi ukiisha mbona hatuwasikii km nyie ni wema sana....
 
Wenye akili hapo tulishajua kwamba muungano ulikufa na Mwl Nyerere, haya ya akina Pinda ni Si Hasa za kifisadi za ccm,
na kwamba ccm hawana tena uwezo wa kuingilia mambo ya znz, Hii ni aibu kubwa kwa ccm na serikali yake iliyoapa kuilinda na kuitetea katiba ya Tanzania. ccm imekosa uhalali wa kuendelea kutawala
Lakini ni sisi watanganyika ndio tunaubembeleza Muungano japo ni dhahiri kabisa kwamba Katiba ya Jamhuri imevunjwa.

Pima halijoto ilivyokuwa ukumbini wakati Msigwa anabishana na Waziri Mkuu. Kelele na vifijo zilirindima kutoka kwa wabunge wa Zanzibar mpaka ikabidi Msigwa aombe nafasi "jamani tuvumiliane, mbona nyinyi mkisema tunawavumilia"? Sasa wabunge wa Zanzibar ni minority ukumbini. Swali ni, hakuna Wabunge wa Bara walioona hoja ya Msigwa? Kwamba Katiba inavunjwa? Hakuna Wabunge wa Bara Wakristo walioguswa? Walikuwa wapi? Iweje kelele za kumzomea Msigwa kutoka kwa minority ziteke ukumbi, why? Wabara wanafyata mkia inapokuja kwenye Muungano!

Na baada ya Pinda kutoa maelezo yanayovunja Katiba (kwamba sehemu moja ya nchi inaweza kujiwekea utaratibu wa kujitawala kidini iwapo wengi wao ni wa dini moja) Spika Makinda akashindilia msumari wa mwisho kwa mpasho huu "...kama wenyewe wanataka nyinyi kinawauma nini?" Kwanza ni makosa kwa Spika Makinda kuchomekea pointi za kumkandamiza mchangiaji anaehojiana na Waziri Mkuu, not least because Makinda anatakiwa awe upande wa Bunge, sio serikali, amsaidie Mbunge ajibiwe hoja zake na serikali! Yote hii kubembeleza Wazanzibar.

Muungano umetushinda, tunadai sasa kila upande uwe ni dola huru yenye mamlaka yake kamili.
 
Sidhani kama huo ukristo wako au upagani unakuruhusu kuvaa chupi hadharani, na wewe unajua kwa nini mnavaa nguo fupi, hata mila zetu za tanzania haziruhusu kuvaa nusu uchi, na unafahamu kwamba mwanaume akikuangalia huku umevaa nguo fupi na za kubana ili uoneshe masaburi yako unakuwa ume mtamanisha. Sasa kwa zanzibar watu wamefunga kwahiyo usiende kuonesha masaburi yako kule ni marufuku.

hivi huku ytamanisha mnakokuongeleaga wanaume ni kwa aina gani? yaaani kumbe nyie akili zenu ni za kushkiwa? kwanza wakumbuka mila zetu asili ya watanganyika ni kuvaa nguo za ngozi ambazo zilificha mbele tu mgongo wazi na zilificha makalio kidogo tu. kama huamni kaangalie hata picha alizo piga bibi yako enzi hizo umini ulikuwa umuni kweli siyo siku hizi halafu eti mtatutamanisha himilini hisia zenu kama hamuwez mtazini sana na wengi kwa kutamani tu ................
 
Mimi ni mfuasi wa CCM wote mnanijua hapa JF,swali la Mch.Msigwa ni la msingi kabisa na hali siasa ya chama chake,hapa imedhilika serikali ya SMZ ni ya kidikteta na inakandamiza watu ambao sio waislamu,Pinda kaonesha umbumbu wa hali ya juu sana!
 
Hiyo imeandikwa kwenye vitabu vyenu sisi vyetu vinasisitiza mtu avae kwa kujistiri,sio avae anavyotaka'halafu hii amri yakufunga mahotel ni amri iko nchi zote karibu zenye idadi kubwa ya waislam jaribu kutembea uone'

swala si amri ndugu yangu....je ni sahihi kwa kuwa wewe unafunga basi ukataze wengine wasile.
 
kufunga ufunge wewe kwa faida yako halafu ukataze wenzako wasile hii ni imani gani? huku ni kufunga au kubadili masaa ya kula?
 
Kama wanajihifadhi kama waislam, hii amri imetoka wapi sasa? common sense inaniambia kama wangekuwa wanajihifadhi kama waislam hii amri isingekuwapo. Hivi kujihifadhi kama waislam nayo ni utamaduni wa Zanzibar? Ba...

tatizo wakristo hamuna heshima ,tangazo lipo wazi kuwaonya wale wanaojidai wao ni wakereketwa na watu waliojaa dharau ,wapo wakiristo waliowajeuri ,wanajua fika kuwa mtu fulani au waislamu wamefunga,basi atajileta Mr monkeyface na sigara yake aivute mbele ya mislamu au waislamu ,au atafika na ugali wake na mchuzi wa mlenda ale mbele ya waislamu au Muislamu ,anayafanya hayo kwa makusudi .

Waislamu hawaishi hapa Zanzibar tu ,wameenea dunia nzima ,kila nchi unayoijua wewe basi muislamu yupo ,Na nchi hizo waislamu hawafanyiwi ujinga lkama mnaowafanyia hapa ,Hivyo kuyakomesha hayo serikali ya Zanzibar imeamua ilivyo amua liwalo na liwe ,na wewe au jamaa yako kama ni hodari aende Zanzibar akafanye upuuzi wake aone sababu za moto kuwaka ndani ya maji.

Ishaamuliwa liwalo na liwe ,halafu waislamu wenzangu msipigishane nao sana hawa wanaojidai ni wakiristo sugu na ni sugu kweli maana wanapingana na bibilia kitabu chao wenyewe ,bibilia imewambia No one has seen God at any timeJohn 1:18
,wao wanasema wamemwona ,utawaeleza nini watu hao.
 


wanatakiwa waheshimu mwezi mtukufu kama kula kale nyumbani kwako.. Kama vinguo vya kipuuzi kamvalie mumemo mkiwa chumbani ...
kisa nyie mmefunga????sasa hapo umefunga au unakimbia kula...ungekuwa unafanya kazi kwenye mgahawa ungeacha au???maana watu wangekuwa wanakula mbele yako muda wote
 
kisa nyie mmefunga????sasa hapo umefunga au unakimbia kula...ungekuwa unafanya kazi kwenye mgahawa ungeacha au???maana watu wangekuwa wanakula mbele yako muda wote
Hii imenifurahisha...hata mimi najiuliza hivi wake/dada/wasaidizi wao wa ndani wanaowapikia futari huwa wanafanyaje? au futari na milo yote huanza kupikwa kuanzia saa kumi na mbili jioni? Nilikuwa nafikiri tu...
 
Leo bungeni katika hali ambayo imeshangaza wengi,Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Kayanza Peter Mizengo Pinda amejibu swali gumu kirahisi sana kwa maono yangu. Ameliuzwa kuhusu kauli iliyotolewa na viongozi wa kiislamu ,Zanzibar...kauli ambayo iliamuru kukomesha uvaaji wa nguo zisizoendana na uislamu pia wameamuru kukomesha vitendo vya watu kula (hovyo) katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Mhe, Pinda amedai kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa Zanzibar ni Waislamu (hilo silipingi) hivyo suala la sheria na kanuni za kiislamu kutumika siyo hoja. Je,ni sawa kanuni hizi zisizokuwemo kwenye katiba yetu kutumika huku ikijulikana nchi haina dini? Pili , Wakristo kuwa wachache Zanzibar ni kigezo cha kuwalazimisha kufanya hata kile wasichokipenda? Tatu, naomba wale wanaoijua katiba ya Zanzibar kama imeainisha kwamba zanzibar ni nchi ya kiislamu kinyume na katiba ya muungano..!


Mara kwa mara kauli za Waziri huyu zinaleta utata kwa sababu zinakuwa hazijakaa vema kabisa.... namshauri kwa sasa atoe hicho kipindi cha mwasali na majibu ya papo kwa hapo hadi hapo atakapojipanga upya..
 


wanatakiwa waheshimu mwezi mtukufu kama kula kale nyumbani kwako.. Kama vinguo vya kipuuzi kamvalie mumemo mkiwa chumbani ...
Mwezi mtukufu ukiisha, full kujiachi siyo?

Kwa hiyo dhambi kwa imani yao unaruhusiwa ispokuwa mwezi mtukufu?

Mimi nadhani hii marufuku yao ingeleta maana km ingefanyika throughout the year au ktk maisha yao yote. Hapo ndo ningeanimi kuwa kweli wanasimania imani yao haswa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom