Pinda kapindisha makaomakuu ya wilaya ya Rorya-katangaza makao makuu kuwa Ingrii juu

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,942
428
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katangaza rasmi makao makuu ya wilaya ya Rorya kuwa INGRII JUU Tarafa ya Girango anapotokea aliyekuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa Rorya Mzee phielemon ologi sarungi,
uhamuzi wa waziri mkuu Pinda umewaacha wananchi wa wilaya ya Rorya nji panda kwani ingrii sio miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa na Tume iliyohundwa na waziri mkuu
 
Duuuu! Hebu tutanabaishe zaidi kuhusu uamuzi huo, hususan sababu za makao makuu kuwa hapo, na kama kuna miundombinu ya kutosha kama Rorya..maana isiwe ya kisiasa zaidi kiasi cha kutoleta tija. Hapa nakumbuka jinsi utawala wa awamu ya kwanza ulivyoamua makao makuu ya Mkoa wa Pwani kuwa Kibaha badala ya mji mkongwe wa bagamoyo uliosheheni kila sifa na miundombinu stahiki kwa wakati ule. Na tangu kutekelezwa kwa uamuzi huo, kwa maoni yangu si rahisi kushawishika kuamini kuwa uamuzi huo ulikuwa wa busara kwani mji wa Kibaha hadi sasa hauna sura ya kuwa makao makuu ya mkoa wa Pwani.
 
Hawa wa Rorya walishaamua kulifanya hili suala kuwa siasa, hayo ndio matokeo yake
 
Duuuu! ama kweli Bongo kuna maamuzi ya kisiasa sana, na hii inatokana kila kitu tunachokifanya kuchukuliwa kisiasa zaidi.
Toka Utegi to Ingri Juu ni 7au 8km, Toka Randa to Ingri ni 10km, Toka Shirati to Ingri ni around 35km.
Hapa kaamua wote wakose, Shirati, Utegi na Randa. Je miundombinu Ipo ya Kutosha??????? Kila la Kheri makao makuu ya wilaya ya Rorya.
Swali Je Wana Rorya wataacha sasa malumbano ya kisiasa yasiyokuwa na mwisho na kuamua kuijenga na kujiletea maendeleo ktk wilaya yao mpya?
Plz wana Rorya wote now fanyeni kazi, maamuzi ndo hayo yameshatolewa mkubali matokeo.
Kila la Kheri na mjitahidi kujiletea maendeleo.
 
Wangeamua tu makao makuu yawepo Shirati, kuna hospitali, kuna ofisi za serikali kama polisi, mahakama, uhamiaji, uvuvi, posta. Mitaa yake imekaa vizuri hasa Obwere hata Kabwana, manake watu miaka hiyo ya nyuma waliondolewa ziwani na sehemu nyingine na kupewa ardhi. Kuna maji ya uhakika na umeme upo. Sema na wajaluo kwa kushikilia koo (ukiwa koo ya ka Maganga, basi koo ya Sote hata ikifiwa hakuna kusikitika). Utegi na Randa hakujaendelea kama Shirati, sasa huko Ingri, kazi ipo katika maamuzi ya kisiasa bila kufuata ukweli.
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katangaza rasmi makao makuu ya wilaya ya Rorya kuwa INGRII JUU Tarafa ya Girango anapotokea aliyekuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa Rorya Mzee phielemon ologi sarungi,
uhamuzi wa waziri mkuu Pinda umewaacha wananchi wa wilaya ya Rorya nji panda kwani ingrii sio miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa na Tume iliyohundwa na waziri mkuu

Mkuu ahsante kwa taarifa. Ila mbona headline imekaa kiudaku zaidi??
Kapindisha kivipi? Ulikuwa na mategemeo gani au mlishapanga kwamba atangaze wapi??

Mi naona ili kuondoa mgogoro wa kisiasa kati ya Watu wa Shirati na Utegi ambao ndio ilionekana wanapingana vikali kabisa kuhusu suala la makao makuu ya wilaya Mh. Pinda kafanya maamuzi ya msingi kabisa. kilichobakia sasa ni wananchi wa Rorya waanze kujenga Wilaya yao.

Suala la Tarafa sijui Girango au Nyancha sio ishu hapa.
 
Wangeamua tu makao makuu yawepo Shirati, kuna hospitali, kuna ofisi za serikali kama polisi, mahakama, uhamiaji, uvuvi, posta. Mitaa yake imekaa vizuri hasa Obwere hata Kabwana, manake watu miaka hiyo ya nyuma waliondolewa ziwani na sehemu nyingine na kupewa ardhi. Kuna maji ya uhakika na umeme upo. Sema na wajaluo kwa kushikilia koo (ukiwa koo ya ka Maganga, basi koo ya Sote hata ikifiwa hakuna kusikitika). Utegi na Randa hakujaendelea kama Shirati, sasa huko Ingri, kazi ipo katika maamuzi ya kisiasa bila kufuata ukweli.

Geographically Shirati/Utegi are actually out of question.
Shirati ilikuwa na Hospitali sasa ivi ile hospitali hata reputation yake imeshuka sana imekuwa kama Shirati Secondary amabayo ilikufa kibudu.
Kuhusu kuwepo kwa ofisi za uvuvi na uhamiaji ni obvious kwamba pale ni ziwani na pia ni karibu kabisa na mpaka wa Tanzania na Kenya. Ndio maana ofisi za uhamiaji ziko pale.

Kwa wajaluo kushikilia koo hili ni kweli kabisa na ndo maana ni bora tu wakakosa wote ili hao ambao hawakuwa na taarifa wapewe nafasi ili wilaya ijengwe.

Hongereni watu wa Ingri maendeleo yamekuja mlangoni mwenu jikwamueni muijenge Rorya.
 
JF,

Maoni yangu hapa zinatafutwa kura za lazima, kwa wale ambao wako huko nyumbani...population ya Rorya na maeneo yanayopakana ni Kiasi gani? Yaani(wapiga kura) wenye data!

Isije ikatokea kuwa kuna mpango wa kuwagawanya wananchi wa maeneo husika, haswa Utegi.(Wakazi wenyewe)

Mshikamano unahitajika bila kujali itikadi za siasa, eneo hili haliwezwi kuachwa nyuma kimaendeleo kwasababu tu za kisiasa au kwa nani yuko chama gani, hayo ya siasa waachieni Kivukoni na Ocean road!

Na ni hivi, masuala ya kubadilisha makao ya wilaya yako chini ya Waziri Mkuu?

Kwanini isifanywe referendum na kuona wapi haswa pana wafaa wananchi/wakazi wa huko kuwa ndio Makao makuu ya wilaya?

Je bunge haliwezi kunusuru haya?

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom