Pinda Jiuzulu kazi imekushinda!

Yaani mambo mengine yanatia mashaka juu ya uwezo wenu wa kufikiri.mbona huthubutu kumtaja JK atoke madarakani kwa kuwa KAGODA ilitumika kuchukua pesa za EPA kwa ajili ya uchaguzi uliomuingiza madarakani?

Think BIG sio unaongea kwa chuki..
 
Mr Prime Minister you owe us an apology kabisa!! With such an altitude nina lazimika kuamini kwamba, mambo you have never taken serious any of the issues that have been spoken about Mafisadi (Him being one of them!)

Sidhani kama kuna Mbunge yeyote anaweza akasimama akasema sema maneno toka hewani tena anamjadili mtu wizi na ubadhilifu wa mali ya umma. Wabunge ni watu wenye akili timamu na wanabeba dhamana ya wananchi hivyo wanachokizungumza bungeni ni masula genuine ambayo yanahitaji ur attention.

Bahati mbaya wewe unawaona ni mabwege, wapiga porojo, wasio na lolote la msingi!


Ningekuwa mimi ningejihudhuru!!!
 
Watanzania tulishaambiwa huu ni mwaka wa siasa na si mwaka wa kufanya kazi hivyo kila mtu anafanya siasa!!
Aibu hii utuepushe nayo eeh Mungu ukaae kwenye kiti cha enzi.

Mungu isamehe Tanzania na kuipa baraka mpya.amen!!
 
Pinda Jiuzulu kazi imekushinda.


Hapo ndugu yangu unampigia mbuzi gitaa....dawa yao ni kuondolewa kwa nguvu na si kura! Kujidanganya kuwa tutawang'oa kupitia uchaguzi, ni ndoto za mchana....itachukua muda mrefu na nchi itakuwa ishapigika kisawasawa. Ila kasema sahihi kuwa bungeni ni porojo tu...anachomaanisha ni ule msemo "mtumikie kafiri upate mradi wako"...full stop!
 
Bunge kumbe ni mahali pa uzushi na umbeya basi inabidi bunge livunjwe kwa maana hela za walipa kodi zinapotea bure kwa ajili ya mambo ya uzushi na umbeya,sasa Pinda naye kumbe ni mbeya na mzushi kwani naye si mbunge jamani
 
Hivi, ina maana Pinda asingesema yale kule kwa RA, bado angekuwa waziri mkuu bora?

Hivi ni lini mtakaa chini na kukubali kuwa serikali hii yote imeoza pamoja na CCM yao?

Ukishaamini hivi, hivi Pinda kafanya la ajabu gani? mpaka mtoe machozi hivyo!
 
Mi niliposikia hiyo kauli sikuamini kama imetoka kwake muheshimiwa sana. By the way kwenye mchezo wa 'siasa' ni lazima uwe na rangi mbili zitakazo kutofautisha kulingana na matukio yaliyopo. Ukiwa hapa utazungumza hili,ukiwa pale utazungumza lile-ndo mambo yalivyo.
 
miye nilishakata tamaa naye; madaraka ni kitu kibaya sana hasa yakiwa mikononi mwa watu kama yeye..

Kaka yangu Pundit alisema from the very first day huyu bwana alipotoa acceptance speech bungeni kwamba Waziri Mkuu bomu huyu, watu eeeh, aaah.

Matokeo yake mnayaona sasa.
 
Bunge kumbe ni mahali pa uzushi na umbeya basi inabidi bunge livunjwe kwa maana hela za walipa kodi zinapotea bure kwa ajili ya mambo ya uzushi na umbeya,sasa Pinda naye kumbe ni mbeya na mzushi kwani naye si mbunge jamani

Si ndio hawa wanalipwa marupurupu ya 46 million baada ya kwenda kusinzia bungeni kwa kazi za umbeya na majungu. Then wakichaguliwa wanakomba nyingine 40 million za kununulia mashangingi. Kweli fweza ya walipa kodi inatafunwa from every corner.
 
Hivi ni lini mtakaa chini na kukubali kuwa serikali hii yote imeoza pamoja na CCM yao?

Nakubaliana na wewe mkuu asilimia mia, sioni mtendaji aliye bora na mwadilifu katika serikali hii - kwa ufupi tu CCM na serikali yake imeoza.

Tatizo la watanzania wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.
- mkaambiwa maisha bora kwa kila mdanganyika
- juzi mkaambiwa kilimo kwanza
- KAGODA mzimu usiojulina kabisa, ( kiumbe kisichoishi)
- juzi bungeni wakakaa kama makada wa CCM wakalimaliza la richard monduli - nani aliyekuwa
analipwa sh 152m kwa siku hadi leo hajulikani.
- Rada hadi serikali nyingine inachunguza kwa niaba yetu na kugundua kulikuwa na rushwa ila sisi
raha mustarehe - eti tunasubiri riport itoke "ungireza bungeni kwao" kwanza ili tuanze uchunguzi.
- sasa wameanza kusafishana majimboni kuelekea uchaguzi mkuu - mweee!! nitatapika nimikunywa chai
asa ivi.

yote haya na mengine mengi tu ndugu zangu hamuungani ya waberoya kwamba CCM na Serikali yao wote chungu kimoja? - wameoza? - fikeni pahala mseme " YATOSHA"
 
Nakubaliana na wewe mkuu asilimia mia, sioni mtendaji aliye bora na mwadilifu katika serikali hii - kwa ufupi tu CCM na serikali yake imeoza.

Tatizo la watanzania wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.
- mkaambiwa maisha bora kwa kila mdanganyika
- juzi mkaambiwa kilimo kwanza
- juzi bungeni wakakaa kama makada wa CCM wakalimaliza la richard monduli
- sasa wameanza kusafishana majimboni kuelekea uchaguzi mkuu - mweee!! nitatapika nimekunywa chai sasa hivi.

yote haya ndugu zangu hamuungani ya waberoya kwamba CCM na Serikali yao wote chungu kimoja? - wameoza?

Nashangaa mtu anakuja na li -title likuuubwa, eti amelitia taifa aibu, wakati kuwemo ndani ya CCM tu aibu tosha, kama kila siku wanatembea uchi na tuhuma kibao leo hii unashangaa nini? mtu yuko uchi unashangaa manyoya ya kifuani!!

Yaani unakuta Pinda na serikali yake hawaudhi , ila wale watu wenye matumaini na hii serikali ndio wanaokera na kuudhi humu!

We kama una matumaini na kiongozi yeyote wa CCM si lazima una matatizo ya akili.

ukiweka matumaini kwa hawa watu, uwe tayari kutiwa aibu kila siku! presha na hasira ziwapande mpaka mkome!
 
Mpaka kufikia hapo muheshimiwa ametuaibisha.

Mi naona ameonyesha 'his true colour' Siku zote kavaa ngozi ya kondoo mara mtoto wa mkulima, mara anamwaga chozi kwa albino kumbe wapi! mbele ya fisadi papa anasema kilichoko moyoni mwake kwamba bungeni pale ni blahblah tu!
 
Ni kweli Pinda amelitia aibu taifa lakini inawezekana katumwa na JK.Tena instinct zangu zinanimbia RA aliomba/ aliamrisha JK awepo ila kwa kutuzuga ili image yake iwe colured na isiwe distorted. Jk kamtuma Pinda.

Sasa Image ya Pinda inaanza kuwa Black and white . hahhahaha siasa bana.

Kwa mtazamo mwingine labda RA ni NYATI na MUWINDAJI( JK)mwenye Gobore( Pm PInda) kwa uoga bado anatafuta position ya kummaliza huyu NYATI. sasa usilaumu GOBORE kwa kumjeruhi NYATI mguuni badala ya kumuuua. Ingawa ni GOBORE MUWINDAJI akiwa jasiri, makini na nia ya kweli ya kumuua NYATI anaweza.
 
Wabunge mmesikia hayo? Mheshimiwa mbunge mwnzenu anasema mnapiga hadithi za kwenye kahawa tu humo mjengoni! Kweli?

Inawezekana, maana hata mlivyofyata juu ya Richmond report juzi, ni kweli mnazuga tu.
 
Back
Top Bottom