Pinda in his own words..."and I'm officially sad!"

Gustanza_The

Senior Member
Aug 6, 2008
126
7
2008-09-06 09:27:56
Na Abdallah Bawazir
NIPASHE

Pinda alisisitiza kuwa sekta binafsi inafaa kuungwa mkono na kuwezeshwa, kwani inatoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi na ndiyo maana serikali katika sera zake za mabadiliko ya kiuchumi imeamua kuishirikisha kwa kiasi kikubwa na kuisaidia ili iweze kukua. [Good point Pinda!]

Akionyesha kukerwa na maendeleo duni ya sekta hiyo, alisema anaumia anapokwenda katika nchi nyingine na kukuta sekta binafsi imeshamiri na kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi zao na kushangazwa kwa nini Tanzania isiwe kama nchi hizo. [Tukuulize wewe, Pinda!?]

``Hivi karibuni nilikuwa Shamal Sheikh (Misri). Mji huu zamani ulikuwa ni jangwa tupu, lakini sasa umebadilika kabisa, una maendeleo makubwa [ Kwasababu wamisri sio wasanii kama alivyo bosi wako Kikwete!] Nilitembelea fukwe zake zimejengwa mahoteli makubwa ya kitalii, nilipouliza nikaambiwa hii yote ni sekta binafsi, nikaumia sana. Nikajiuliza hivi sisi tuna nini, [Sisi tuna UJINGA!!!]`` alisema Pinda.

``Tubadili fikra na kuacha urasimu katika kushughulikia mambo haya, tumekalia taratibu na sheria tu, lakini wenzetu wao wanaangalia nini kinafaida kwa wananchi na kukishughulikia haraka,`` [Na kwanini sisi hatuangalii nini kinafaida kwa wananchi na kukishughulikia haraka?]

Pia aliyalaumu mataifa ya nje kuwa yamekuwa yakikwamisha baadhi ya miradi ya maendeleo nchini kwa kisingizio cha uharibufu wa mazingira. [ Pinda hebu nisaidie hapa, kwani Tanzania bado ni koloni?]

``Tulitaka kujenga barabara kwenye mbuga ya Serengeti tukaambiwa tunaharibu mazingira ya mbunga, kuna kampuni ya Kenya ilitaka kupewa bonde la Mara kwa ajili ya kilimo cha mpunga lakini lo! watu walipiga kelele utafikiri nini, ipo siku atatokea kiongozi kichaa atakataa tu haya,`` alisema Pinda. [Na nyie mlivyo wajinga mkakubaliana na hayo mataifa ya nje, ambayo sasa yanaimba "drill baby drill?" Mataifa ambayo yanatumia coal kuzalisha nishati ingawa coal yenyewe inaaminika kuwa kichafuzi namba one cha mazingira duniani? Give me a break, Pinda!!]

Fact: In case you forget, Pinda is our Prime minister.
 
``Tubadili fikra na kuacha urasimu katika kushughulikia mambo haya, tumekalia taratibu na sheria tu, lakini wenzetu wao wanaangalia nini kinafaida kwa wananchi na kukishughulikia haraka,``

``Tulitaka kujenga barabara kwenye mbuga ya Serengeti tukaambiwa tunaharibu mazingira ya mbunga, kuna kampuni ya Kenya ilitaka kupewa bonde la Mara kwa ajili ya kilimo cha mpunga lakini lo! watu walipiga kelele utafikiri nini, ipo siku atatokea kiongozi kichaa atakataa tu haya,``

Siamini Pinda kasema hivi vitu! Pinda anasema kuna kiongozi atakuja kukataa hivi vitu, ina maana anaamini Kikwete anachemsha!

Kasemaje, tunakalia sheria na taratibu? Huyu Pinda...?
 
Changing our mindset do not need foreign aid but foreign power - Asante Pinda kwa kudhibitisha hili
 
Hivi karibuni nilikuwa Shamal Sheikh (Misri). Mji huu zamani ulikuwa ni jangwa tupu, lakini sasa umebadilika kabisa, una maendeleo makubwa [ Kwasababu wamisri sio wasanii kama alivyo bosi wako Kikwete!] Nilitembelea fukwe zake zimejengwa mahoteli makubwa ya kitalii, nilipouliza nikaambiwa hii yote ni sekta binafsi, nikaumia sana. Nikajiuliza hivi sisi tuna nini, [Sisi tuna UJINGA!!!]`` alisema Pinda.

HEBU MH. PINDA TEMBELEA MBUGA ZETU ZA WANYAMA UKAULIZE MAHOTELI NA LODGES ZOTE ZA KITALII ZILIZOKUWA NDANI YA HIFADHI ZETU ZA TAIFA NI ZA NANI NDIPO UTAJUA URITHI WETU UMERITHIWA NA WATU WA NJE ASILIMIA 99! WATANZANIA TUMEKWISHA EE MUNGU TUSAIDIE.
 
...............``Tubadili fikra na kuacha urasimu katika kushughulikia mambo haya, tumekalia taratibu na sheria tu, lakini wenzetu wao wanaangalia nini kinafaida kwa wananchi na kukishughulikia haraka,`` [Na kwanini sisi hatuangalii nini kinafaida kwa wananchi na kukishughulikia haraka?]................. Ni kweli potentially viongozi wetu wanajua nini cha kufanya bila kelele za wananchi BUT kutokufanya si kosa la kikatiba na je they have no case to answer?
 
kwa jinsi ninavyomfahamu pinda, huenda yanayoendelea yanamuumiza, lakini atafanya nini wakati yeye ni mteuliwa wa kikwete wa mpito? yaani kikwete anajua wazi kuwa pinda siyo chagua lake, bali anasubiri vumbi litulie atuletee kATI YA WAFUATAO, ROSTAM, CHENGE, PETER SSERUKAMBA, LOWASA,MASHA,NK
 
Nilijua haka ka-ugonjwa ka-kujadili watu kama watu na wala sio hoja ni dhambi kubwa ni sawa na kula nyama ya mtu... hauwezi kuacha... Walianza kujadili Mh. Mkapa wakati wa Awamu ya Tatu, sasa Mh. JK, alafu Mh. Lowassa, alafu Mh. Pinda... baada ya hapo Mh. Mbowe, Mh. Dr. Slaa... etc.... wakiisha wanasiasa wataanza kuwajadili akina Kasheshe, Mwanakijiji, Field Marshall ES... etc... mpaka kufa kwao... maana kaugonjwa hakana tiba lakini kana chanjo angalau!

Heri yangu nina kinga/chanjo yake.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Mkuu,

Inajadiliwa hoja hapa na sio mtu. After-all hoja ina originated from mtu so the two are concomintantly related...
 
Sumaye, Kikwete now mizengo Pinda ---- the same!
Baada ya kutoka Boston Sumaye aligundua kwa nini Tanzania haiendelei!
Mr. Kikwete - alipokuwa France na kuulizwa na Economst Magazine- Hajui kwa nini Tanzania (Africa) haiendelei!
Now mizengo Pinda, kaja vile vile hakuamini kuwa sector binafsi wanaweza kufanya mambo makubwa kama yale!
Hi Mizengo; do you know before that Arusha Declaration; and before wealth nationalization most of those properties and facilities belonged to private sector?
What you have seen in Egypt is only the tip of iceberg; go to Hong Kong, Singapore, South Africa, New York etc most of the development is the result of private sector.
Make the banks and other financial institution service the people, implement good governmenance and the rule of law; educate your people; that is all!!
 
As i have always maintained the root of almost all of Tanzanias economic problems is poor leadership.

You are absolutely right my man. This stuff is not rocket science and has been successfully implemented in many countries that have pulled themselves out of poverty. Korea went from being as poor as us 40 years ago to the 11th largest economy in the world. They invested in infrastructure (road, rail, etc,) and their people (education, health, etc). They are a small country with absolutely nothing but they saw how japan did it and basically emulated them. We do not need to reinvent the wheel but these idiots who run our country are completely incompetent, corrupt and could not care less.
 
HEBU MH. PINDA TEMBELEA MBUGA ZETU ZA WANYAMA UKAULIZE MAHOTELI NA LODGES ZOTE ZA KITALII ZILIZOKUWA NDANI YA HIFADHI ZETU ZA TAIFA NI ZA NANI NDIPO UTAJUA URITHI WETU UMERITHIWA NA WATU WA NJE ASILIMIA 99! WATANZANIA TUMEKWISHA EE MUNGU TUSAIDIE.

Oh yes, Mungu tusaidie... maana kama waziri mkuu anatoa utumbo kama huu kwenye vyombo vya habari, then hii serikali haijui inachokifanya. And it really sadden me ndugu wananchi... [kwa style hii, safari tunayo!]
 
As i have always maintained the root of almost all of Tanzanias economic problems is poor leadership.

You are absolutely right my man. This stuff is not rocket science and has been successfully implemented in many countries that have pulled themselves out of poverty. Korea went from being as poor as us 40 years ago to the 11th largest economy in the world. They invested in infrastructure (road, rail, etc,) and their people (education, health, etc). They are a small country with absolutely nothing but they saw how japan did it and basically emulated them. We do not need to reinvent the wheel but these idiots who run our country are completely incompetent, corrupt and could not care less.

Well said Alpha! I sincerely believe kwamba, Bongo inahitaji dictator. Kuna morons wengi sana walioko kwenye system ambao bila kuamurishwa nini wafanye, tutakuwa tunacheza makida kila siku. Niongezee tu kwa nchi ulizozitaja hapo juu: Malaysia. Hawa jamaa in the 70s & 80s, walikuwa wanategemea zao la Tin na rubber as primary source of revenue/foreign currency. Then mwishoni mwa miaka ya '90/mwanzoni mwa 2000 [baada ya economy yao kuingia kwenye deep recession], waliamua ku-invest heavily on education & high tech products [semi-conductors, chips, electonic gadgets etc]; na leo hii hawa jamaa ni miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa ku-export bidhaa za ICT.

Tatizo viongozi wetu hawana vision ni wapi wanataka kuichukua/peleka nchi. And as long as wapiga kura walio wengi bado wamelala usingizi, Bongo ina safari ndefu sana!
 
Baada ya kutoka Boston Sumaye aligundua kwa nini Tanzania haiendelei!
Mr. Kikwete - alipokuwa France na kuulizwa na Economst Magazine- Hajui kwa nini Tanzania (Africa) haiendelei!
Now mizengo Pinda, kaja vile vile hakuamini kuwa sector binafsi wanaweza kufanya mambo makubwa kama yale!

No offense fellas, but I think sasa muda umefika tutumie wasomi wa kibongo waliosoma nje, na tuachane na hawa wanaokariri hapa UDSM. See, kama waziri mkuu [Sumaye] anaweza kuongoza nchi kwa miaka 10 bila kugundua kwanini nchi haiendelei[piga hatua] mpaka pale tu anapoenda Boston, then something is wrong na mfumo wa elimu ya Tanzania.
 
Kweli tuna kazi! Sham al Sheikh ndiyo maendeleo? Maghorofa ndiyo maendeleo? Mahoteli ufukweni ndiyo maendeleo? Kujenga barabara kwenye mbuga ndiyo maendeleo? Kuharibu bonde ndiyo maendeleo? Huko anakokusifia juzi wamekufa watu kwa maporomoko ya mawe! Kila kukicha hayo maghorofa yanaanguka. Mji wake Mkuu ni mji mmoja wa miji yenye makelele duniani. Hivi karibuni walizuia watu kutembelea pyramids baada ya kugundua kuwa bila kudhibiti UHARIBIFU unaofanywa na watalii hiyo hazina itapotea hivi karibuni. Aulize wamisri wangapi wanafaidika na hayo mahoteli na pwani za Sham al Sheikh!

Tunapenda mto njia za mkato! Maendeleo anayozungumzia sio sustainable. Hao wanaotuasi tusijenge huko kwenye mbuga yaliisha wapata! Leo tunavunja mji wetu kujenga maghorofa na malls ati kuvutia watalii! Leo tunaachia mji mkongwe wa Bagamoyo upotee ili tujenge mahoteli pawe kama Sham al Sheikh. Mtalii gani atakuja bongo kuangalia maghorofa na malls.

Sikio la kufa................................

Amandla!
 
Last edited:
Kweli tuna kazi! Sham al Sheikh ndiyo maendeleo? Maghorofa ndiyo maendeleo? Mahoteli ufukweni ndiyo maendeleo? Kujenga barabara kwenye mbuga ndiyo maendeleo? Kuharibu bonde ndiyo maendeleo? Huko anakokusifia juzi wamekufa watu kwa maporomoko ya mawe! Kila kukicha hayo maghorofa yanaanguka. Mji wake Mkuu ni mji mmoja wa miji ya makelele duniani. Hivi karibuni walizuia watu kutembelea pyramids baada ya kugundua kuwa bila kudhibiti UHARIBIFU unaofanywa na watalii hiyo hazina itapotea hivi karibuni. Aulize wamisri wangapi wanafaidika na hayo mahoteli na pwani za Sham al Asheikh!

Tunapenda mto njia za mkato! Maendeleo anayozungumzia sio sustainable. Hao wanaotuasi tusijenge huko kwenye mbuga yaliisha wapata! Leo tunavunja mji wetu kujenga maghorofa na malls ati kuvutia watalii! Leo tunaachia mji mkongwe wa Bagamoyo upotee ili tujenge mahoteli pawe kama Sham al Sheikh. Mtalii gani atakuja bongo kuangalia maghorofa na malls.

Sikio la kufa................................

Amandla!

Sikio la kufa, halisikii dawa.
 
Mawaziri pamoja na waziri mkuu wote hawajui kama wana madaraka makubwa nchi hii, wanalialia tu utafikiri kuna kuna uongozi wa juu zaidi yao tena. Si Pinda tu, ni mawaziri karibu wote ndivyo walivyo - hawawajibiki bali wanaongea kwa ubinafsi ili kujipatia umarufu usio na mbele wala nyuma. Si unajua waTZ tupo usingizini.
Huo ugonjwa wa kutowajibika upo kwa viongozi wa umma wa ngazi karibu zote, hakuna ajuaye wajibu wake.
Elimu yetu pia inachangia sana, wanaomaliza masomo wengi hawaandaliwi kuchangia mawazo mapya bali kufuata mkumbo wa utaratibu uliopo, kuwa myenyekevu na kutopinga mawazo ya mwenyekiti (- CCM of course).
 
Tatizo viongozi wetu hawana vision ni wapi wanataka kuichukua/peleka nchi. And as long as wapiga kura walio wengi bado wamelala usingizi, Bongo ina safari ndefu sana!

Samahani naopingana na wewe, viongozi wetu wengi wanayo vision ya muda wao waliopo madarakani, matamanio ya kurithisha vijana watakaoendelea kuwaabudu milele.

wananchi wenyewe, vision yetu ni ya kutaka shortcut, ndio sababu hata wakereketwa wanajenga hoja kutokana na nani kaisema. na sio kuiangali hoja yenyewe ina maslahi ya muda mrefu kwa taifa (sio mtoa hoja).
safari ni ndefu! nimekubali.
 
JK hivi karibuni kasema Siasa basi tuongoze nchi Kisayansi lets wait and see probably ndio maendeleo mapya though he is not a person to be trusted at all!
 
Back
Top Bottom