Pinda haiamini Bodi Mikopo Elimu ya Juu

Mwanajamii

JF-Expert Member
Mar 5, 2008
7,063
68
Tuesday, 08 November 2011 21:33


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Habel Chidawali, Dodoma




WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema bado kuna kazi ya kufanya katika bodi ya mikopo ya elimu ya juu, kwani amekuwa akipokea malalamiko mengi kuhusu bodi hiyo.

Pia, Pinda alisema ipo tabia iliyojengeka kwa baadhi ya Watanzania wenye uwezo ambao hawataki kusema ukweli juu ya vipato vyao na wamekuwa wakihitaji mikopo ya watoto wao, jambo linaloziba nafasi ya watoto wanaotoka familia maskini.Akizungumza kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha St. John mwishoni mwa wiki iliyopita, Pinda alisema upungufu katika bodi hiyo haupaswi kuvumiliwa tena.

Alisema amekuwa akipokea malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania juu ya bodi ya mikopo, ambayo licha ya uwezo mdogo wa fedha ilio nao, mara nyingi fedha hizo hutolewa bila kuangalia makundi maalumu hivyo kutofanya kazi iliyokusudiwa.
Pinda alisema changamoto iliyopo katika bodi hiyo ni kuangalia upungufu huo na kuuondoa, ikiwamo kutoa mikopo kwa makundi yanayostahili siyo vinginevyo, ili wale wenye uwezo wasomeshe watoto kwa fedha zao.

“Mikopo lazima iangalie makundi hayo, kwani haifai kusikia hata mtoto wa waziri mkuu anasoma kwa kutegemea mkopo au mtu yeyote mwenye uwezo, hilo ni jambo la aibu ndugu zangu, hebu tuwe wakweli katika jambo hili,’’ alisema Pinda.
Kuhusu mafanikio ya chuo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Tanzania, Pinda aliwataka kuongeza bidii kwa kuboresha viwango vya elimu na kutafuta wataalamu zaidi.

“Niwapongeze St John kwa kuweka mfumo mzuri na kutokuwa na migomo kama ilivyo kwa vyuo vingine, pia niwakumbushe kuwa kutumia wataalam wa kutoka vyuo vingine ni sawa na nguo ya kuazima mwenye nayo anaweza kuichukua wakati wowote, somesheni wa kwenu,’’ alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha St. John, Askofu Donald Mtetemela, alisema chuo kimeweka mipango kamambe ambayo itakiwezesha kujipanua zaidi kutoa taaluma yenye ubora na viwango vinavyotakiwa.

Askofu Mtetemela alisema hadi sasa St John ina zaidi ya wanafunzi 5,000, watumishi wapatao 200 na kwamba, tangu mahafali ya kwanza yaliyofanyika mwaka jana na mwaka huu, tayari chuo kimeshatoa wasomi wasiopungua 1,700 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

chanzo cha taarifa hii ni gazeti la mwananchi
 
Pinda ni waziri mkuu ovyo kuliko wote waliomtangulia

Likimeo la kutupwa..juzi alinikera sana alipokua anatoa msisitizo wa kuupigia kura mlima kili'njaro..huyu ni mwanasheria wa namna gani?? kashinda kesi ngapi?? nikiwaza sana nazidi kumshusha thamani..masaburi alisema :"ukimchunguza bata hutomla"
 
kama pinda kakosa kwa hiyo huoni point hata moja katika maelezo yake kwa hiyo ulitaka pinda atufiche wananchi kwamba hana imani na bodi? hiyo ni hatua ya kwanza ya pili tunamuomba sasa achukue hatua kwa aliyoyaona kwenye bodi hiyo.
 
Back
Top Bottom