Pinda Bungeni - Taarifa ya Mabomu kulipuka, Bunge laahirishwa

TAHADHARI: nilimsikia mwanajeshi mmoja akihojiwa na BBC - kuhusu ulipukaji wa mabomu yajo. Yeye alitoa sababu mbili:
1. Ukatikaji katikaji wa umeme
2. Mabomu yamechoka (yame-expire)

Sasa jamani TANZANIA KUNA MAGHALA MANGAPI YA SILAHA - MABOMU?? sasa kama mengine yaki-expire YANLIPUKA HOVYO .... ITAKUWAJE??

MBAGALA, GONGOLA MBOTO - LUGALO - MGULANI ............ na huko MIKOANI JE????

kama kweli sababu ni kuwa yame-expire - TUMEKWISHA - otherwise WANAJESHI WATUAMBIE KAMA NA WAO WAMECHOSHWA NA CCM
mbona yale yaliyo karibu na MAGOGONI ALIPO MKWERE yasimlipue yeye mwenyewe????

THIS TIME TUNATAKA UKWELI .................. au KAFARA ZA MKWERE na SHEIKH YAHYA??????????????????????????

WATANZANIA TUTAFAKARI NA KUCHUKUA HATUA....................................
 
Nasisitiza wakuu, waliohusika (1) WAWAJIBIKE (2) WAWAJIBISHWE KISHERIA full stop na sio mtu anaachia ngazi alafu anaendelea kula kuku na huku amesababisha hasara kubwa kwa Taifa.Tunasubiri wanafiki wakati tunakoma watu wawajibishwe watasema hayo ni majungu na siasa tu eti hatugusi matatizo ya wananchi ya maji,hospitali,kilimo! damn!!! Tutapiga kelele hadi kieleweke.
 
Ndugu yangu Maggid, unashauri Rais wetu achukue hatua gani? Nataka kuona uzalendo wako hapa!
 
what is better, kukaa bure kwa wabunge 357 dodoma wakilipwa stahili zote au kuendelea na mijadala na kuwataka serikali walete kauli ya tukio kesho? nani anabeba garama za kuendelea kuwaweka dodoma?

kweli hatuna uongozi hii nchi

yaani... Kama akili zao hazifikirii hata macho hayaoni.
Khaa!
 
Assurance of more days for sessions(extension), and hence more allowances for MPs!...Thats all i can dream!...huh!

PJ..umenena kweli! Tumepoteza maisha ya watu na mali nyingi...na tunaendelea kuwagharamia wabunge wetu kwa kukaa bure dodoma....wan hofu ya nini??? wangeendelea kujadili jinsi gani ya kuondokana na haya mauzembe.....:A S 20::A S 20::A S 20:
 
Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda anatoa taarifa bungeni kuhusu milipuko ya mabomu Gongo la Mboto

Azungumzia takriba watu 19 wafariki

Raisi kukutana na baraza la usalama la taifa

Bunge laahirishwa ..sababu ya hofu kubwa kwa wabunge

Ndugu Watanzania wenzangu naomba jambo hili tusilifanyie mzaha mzaha tutakwisha sote tusipo jipanga sawasawa. Ninamambo mawili naomba kufahamishwa;
1. Tume iliyoundwa baada ya milipuko ya mbagala ilitoa taarifa wapi na nini lilikuwa suluhisho la kudumu katika taarifa hiyo?.
2. Ni hatua gani madhubuti zilichukuliwa ili kudhibiti milipuko endelevu na serikali yetu likiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania?.
3. Nakumbuka Waziri aliyeko madarakani sasa katika Wizara hii ya Ulinzi Mh. Hussein Mwinyi ndiye yule aliyetuambia kila kitu kipo sawa sawa na Tanzania ni salama na kwamba hakutakuwa na milipuko endelevu tena hivyo wananchi tutulie, anasemaje tena katika hili la Gongo la Mboto?.

Naomba wote waliokuwepo katika Wizara hii ya Ulinzi wakati wa mabomu ya Mbagala na sasa bado wapo kwenye nyadhifa zao watafakari kwa makini jambo hili na kuchukua hatua thabiti ya kung'atuka nyadhifa zao maa hatuko tayari kuona Watanzania tunakufa kila siku bila hatia.

TANZANIA ITAJENGWA NA PIA ITALINDWA NA WENYE MOYO!.
 
jamani sasa umefika wakati wa sisi watanzania kukumbuka mambo muhimu kama vile bima za maisha na property zetu ...... tumesahau sana insurance covers .... tena sasa hivi sio gharama kubwa sana ..... tunalamba bia tuu hata kama zinapanda bei
 
Kwa nini bado wapo madarakani bado wanatakliwa kujiuzuru, kwa mara ya Kwanza Mbagala walisema haitatokea tena sasa imetokea hii ni sababu tosha kwao kujiuzuru;
1. Amiri Jeshi Mkuu Jakaya Kikwete
2. Waziri Mkuu Mizengo Pinda
3. Waziri wa Ulinzi HUsein Mwinyi
4. Mkuu wa Majeshi Gen Mboma
Hapo ni Gen Mwamunyange sio Mboma!
 
am so sad today.. more graves for poor innocent citizens and am sure nobody will be held accountable for those deaths!

shame on us everything is politics in this country...:crying:
 
Kwa kweli inasikitisha, Uzembe wa wakubwa wetu unawaua watu wasiokuwa na hatia kabisa.
Poleni wahanga wote.
 
Inauma sana aisee..kupoteza ndugu zetu ivivi kila wakati...
Si jui lini tutajifunza kutokana na makosa yetu?
Jeshi linapoleta siasa kwenye maslai ya nchi sijui tuende wapi....kuna wakati tutavamiwa then kwa kuwa wamezoea kutoa majibu mepesi bila kutafakari akaja mkuu wa majeshi na kusema ni "Bahati mbaya" tulikua hatuna taarifa...!!
Tatizo serikali ya kishikaji na ufisadi, kila kitu kwao tume na kuingiza mambo mhimu kuwa ya kisiasa zaidi....
 
Back
Top Bottom